Hizi ndizo sababu za wanasiasa wengi kudai katiba mpya; kuipinga

machashi

Member
Aug 17, 2019
15
5
Hizi ndizo sababu za wanasiasa wengi kuidai katiba mpya/ kuipinga

Ni wazi na kweli kabisa kwamba watu wengi hususan wanasiasa, wamekuwa wakiidai katiba mpya ya tanzania kwa nguvu zote.

Hata hivyo, itakumbukwa wakati Samia anaapishwa kuwa Rais, alisema anajua kuwa miongoni mwa mahitaji ya Watanzania ni Katiba mpya, “lakini wasubiri kwanza.”

Ukweli ni kwamba mama alitoa kauli njema lakini ni vema tukatafakari maana kuna watu wana mawazo kwamba hatakubali katiba mpya!

Ubaya ni kwamba kuna mawazo potofu hasa ya mahafidhina kwamba kila mtu ni mtaalamu wa kutengeneza Katiba.

Wengine wanafikiri Katiba ni kama Mahakama na wengine wanafikiri Katiba ndiyo jibu la kila kitu huku wengine wakiiogopa katika ya Jaji Joseph Sinde Warioba ambayo kwa maoni yangu ndio katiba ambayo wananchi waliitaka.

Jibu la Rais Samia kuwa tusubiri kwanza, lina maana kubwa na Watanzania wanapaswa kulitafakari kwa kina. vinginevyo tutachanganyikiwa hata kabla ya kumaliza kazi yenyewe ya kutengeneza Katiba hiyo.

Swali la msingi la kujiuliza ni je, tunaitaka Katiba ya Pendekezwa au Katiba ya Jaji Warioba?

Tujiulize, tunaitaka Katiba ya kuwalinda watu fulani yaani ile Pendekezwa, au ya kukipendelea chama fulani cha siasa au kuipendelea dini fulani?

Ni wazi majibu yatakuwa hapana, bali tunataka Katiba ya wananchi iliyoandikwa na kamati ya Jaji Joseph Sinde Warioba.

Safari ya mchakato wa kupata katiba mpya ya Tanzania ulianza tangu mwaka 2010, wakati Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete alipoamua kuutangazia umma dhamira na nia ya serikali ya kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya.

Mchakato ukaanza rasmi mwaka 2011 kwa kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Na. 83/2011 na baadaye ikatungwa Sheria nyingine ya Kura ya Maoni Na. 11/2013.

Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilitamka kuanzishwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilianzishwa chini ya Waziri mkuu wa zamani, Jaji Joseph Sinde Warioba, ikaratibu mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa rasimu ya kwanza ya katiba ambayo kupitia uhariri wa Mabaraza ya Katiba ikapatikana Rasimu ya Pili ya Katiba.

Rasimu hii ya pili ambayo ni maarufu kama Rasimu ya Warioba ikawasilishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba (BMK) ambalo kwa kiasi kikubwa lilikuwa na wajumbe wengi kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi -Zanzibar.

Kwenye bunge hili la Katiba, ambalo Makamu Mweyekiti wake alikua Samia Suluhu, ambaye ni ndiye Rais wa Tanzania kwa sasa, ndiko joto na mivutano mikali kuhusu masuala kadhaa yaliyomo kwenye katiba ilipoanzia. Baadhi ya wajumbe wa bunge hilo hasa kutoka upinzani waliamua kujitoa na kususia mchakato.

Hata hivyo waliobaki waliendela na ikapatikana Katiba pendekezwa ambayo wengi waliiona kama imekosa muafaka na maridhiano ambayo yanaonekana kama ndio msingi wa kupata Katiba bora ya kitaifa yenye kukubalika na wengi.

Mchakato ukaishia hapo, ilikuwa mwaka 2014, na mpaka leo kumekuwa na mkwamo usiojulikana ni lini utakwamuka. Kumeanza kufanyika harakati tangu kuingia madarakani kwa Rais Samia za kutaka mchakato wa Katiba mpya ufufuliwe.

Kwa mfano chama cha upinzani cha CHADEMA kimeitisha mkutano mkubwa kuhusu Katiba mpya, huku harakati zingine zikiendelea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, ikihusisha baadhi ya wanaharakati, wanasiasa, wasomi na watu wa kawaida.

Zipo sababu nyingi za kubashirika kuhusu kwa nini nchi iamue kuandika upya Katiba yake, moja kubwa ni kupitwa kwa baadhi ya mambo ambayo hayaonekani kwenda na maisha ya sasa wa wananchi husika, lakini pia kujitokeza masuala ambayo yanahitaji kuwekewa misingi ya kikatiba.

Katiba ya sasa ya Tanzania ina umri wa karibu miaka 41 sasa, ilitungwa mwaka mwaka 1977.

Kwa sababu Katiba hii na katiba zote tano zilizopita tangu katiba ya uhuru ya mwaka 1961, ikaja ya 1962,ya 1964, 1965 mpaka katiba ya kudumu ya mwaka 1977, pamoja na marekebisho yake yote 14 kumekuwa na malalamiko kwamba wananchi hawakushirikishwa kikamilifu kuzitunga katiba hizo wakati zinahusu maisha yao. Hivyo ukaundwa mfumo ambao ungeruhusu ushiriki wa wananchi katika kupata katiba bora ambao umeishia njiani.

Kwa wanaotaka sasa Katiba mpya baada ya kukwama kwa zaidi ya miaka 6 ukiwauliza watakwambia wanataka kwa sababu ni hitaji lao kama wananchi wakisema kuna masuala muhimu ya ayopaswa kuwepo katika katiba yao ama kurekebishwa, na katika hilo hawahitaji hisani kutoka kwa mtu yoyote wakiwemo viongozi.

“Katiba ni hitaji kuu, katiba bora ni msingi imara wa maendeleo endelevu, Rais Samia bila katiba bora hutaweza kujenga uchumi imara Tanzania,” aliandika mwanaharakati Ananilea Nkya, ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi mtendaji wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA).

Wengine wanasema Katiba ya sasa iliundwa wakati wa mfumo wa chama kimoja lakini sasa nchi iko kwenye mfumo wa vyama vingi hivyo, katiba ya mwaka 1977 haiwezi kuwa muafaka wa kitaifa wa vyama vingi, kwa sababu ilisimamia misingi ya muafaka wa chama kimoja, lakini sasa kuna misingi ya vyama vingi, kuna mahitaji mapya ya kisiasa, mazingira mapya ya kisiasa na zipo changamoto mpya.

Kwa mantiki hiyo ili kuleta muafaka wa kitaifa, katiba mpya itakayopatikana inapaswa kuwa ndiyo medani ya kuleta muafaka wa kitaifa, amani na upendo nchini.

Ujio wa awamu ya Tano ya Serikali, ulionyeshakwa kauli kwamba mchakato wa mabadiliko ya Katiba sio kipaumbele cha Serikali ya awamu hiyo, kauli ambayo pia imerejewa na Rais wa awamu ya sita, Samia Suluhu alipozungumza na wanahabari hivi karibuni akisema "Nipeni muda tuimarishe uchumi kwanza kisha tuyashughulikie mambo ya katiba na mengine ya siasa'.

Kauli hii imeibua hisia tofauti miongoni mwa watu wanaounga mkono kuanzishwa ama kuendelezwa kwa mchakato wa katiba mpya, ambo waliamini kuingia madarakani kwa Rais Samia kungebadili uelekeo wa serikali ya awamu ya tano na kuifanya katiba kuwa miongoni mwa vipaumbele muhimu.

Uhuru wa watu kujieleza uliodhihirika katika siku 100 za kwanza za utawala wa Rais Samia, pia unatajwa kuchagiza kurejesha mjadala kuhusu katiba mpya, ingawa wapo wachache wanaoosema uongozi wa awamu iliyopita chini ya Rais John Magufuli, umeonyesha ilivyo muhimu kupunguza mamlaka ya Rais, kwa sababu Katiba ya sasa inampa Rais Mamlaka makubwa sana.

Sote tukishughulika na Utanzania na katiba mpya, Tanzania yenye neema inawezekana leo, kesho na keshokutwa.

Tanzania yenye neema kwa vizazi vijavyo inawezekana pia ikiwa tutakuwa na katiba mpya.

Hivyo ni muhimu kwetu sote kukazana kuisaka katiba mpya yenye kutuletea mwanga na kututoa gizani.

Hoja pana ni kwamba, kama tunatengeneza Katiba ya vivuli itadumu muda mfupi na kutokomea kusikojulikana au kutuletea machafuko.

Lakini kama tunatengeneza Katiba ya vitu halisi; mfano Katiba ya upendo badala ya wapendanao; Katiba ya heshima badala ya wanaoheshimiana; katiba isiyojali itikadi ya chama fulani itadumu vizazi na vizazi.

Nina imani Rais Samia anapoendelea na majukumu yake, ataendelea kufikiria namna njema ya kuuendeleza mchakato wa kutafuta Katiba Mpya uliokwama, ili kukata kiu ya Watanzania.

Ni vyema kuwashirikisha watu wote juu ya Katiba. Ni vyema kwamba makundi mbalimbali yakatoa maoni juu ya Katiba. Lakini ni lazima tufike mahali tukubali kwamba si kila mtu anaweza kutengeneza Katiba.

Jopo la waliotengeneza Rasimu ya Katiba ya Warioba ni wazalendo wa kweli na hawakupendelea chama au mtu yeyote, walitengeneza kutokana na matakwa ya Watanzania wote.

Ukweli ni kwamba watu wa kada mbalimbali nchini Tanzania ni kama wameanzisha vuguvugu la kudai Katiba Mpya kama tunavyoona kwenye vyama vya siasa pinzani na hata kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwa lengo la kuishinikiza Serikali kuendelea na mchakato huo.

Kupitia vuguvugu hilo lililopewa jina la “KatibaMpyaMovement”, wananchi wamekuwa wakitoa maoni yao tofauti kueleza umuhimu wa kuwa na katiba mpya hapa nchini na wameitaka Serikali kurejesha mchakato huo.

Katiba Mpya ni moja ya ajenda za vyama mbalimbali vya siasa nchini kikiwemo Chadema na NCCR Mageuzi na CUF ambavyo vimekuwa vikipigania mabadiliko hayo kuwa pamoja na kuwa rais atapunguziwa madaraka, haki itatendeka katika chaguzi.

Gervas Sulle ameandika katika ukurasa wake twitter ,”katika Tanzania tulihitaji katiba kwa nyakati mbalimbali kwa kuwa ni muhimu. Kwa sasa katiba mpya ya wananchi ni lazima na sio ombi kwa maendeleo ya Taifa letu.

Anayekataa Katiba Mpya anataka tubaki na mtazamo wa maendeleo wa 1977. Ni CCM tu wanahofu kwa maslahi yao ya kisiasa.”

Nimewahi kusoma kitabu na ni vema nikanukuu maneno katika kitabu cha Hayati Benjamin Mkapa cha My Life, My Purpose ameandika, “Iundwe tume huru ya uchaguzi itakayokubalika na vyama vyote vya siasa ndio chachu hasa ya kulea na kukuza demokrasia nchini.”

Hakuna Katiba Mpya kwa sasa kwa sababu wengi wamaanini kwamba CCM wapo radhi kwa chochote wabaki na katiba hii inayolinda maslahi yao ya kiutawala na kiuchumi.

Wasomi wa vyuo vikuu wana wajibu mkubwa wa kuamsha umma kudai katiba mpya kwa njia ya amani. Katiba mpya sio matakwa ya Serikali ni matakwa ya wananchi kama alivyosema Jaji Warioba.

Ni wakati sasa vyuo vikuu kutoka walipojifungia na kupaza sauti Kuhusu Katiba mpya.

Nchini mwetu malalamiko makubwa yapo kwenye uchaguzi wa aina yoyote unahohusisha vyama vingi. Rasimu inapendekezwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Huru Uchaguzi wathibitishwe na Bunge. Rasimu pia inaweka sifa za watu wanaoweza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume.

Tume Huru ya Uchaguzi ni chombo muhimu katika mfumo wa utawala wa kidemokrasia kupitia uchaguzi huru na wa haki. Mapendekezo haya yamezingatia misingi inayokubalika duniani kuhusu umuhimu wa kuwepo vyombo huru vya usimamizi wa uchaguzi. Misingi hiyo ni uhuru, uadilifu, uwajibikaji na uwazi.

Ni wazi kwamba yeyote ambaye anapingana na hoja hizo walizoona wazee wetu waliofanya kazi ya kutengeneza kRasimu ya Katiba Mpya ya Tanzania ni maadui wa taifa hili.
 
Back
Top Bottom