Hizi ndizo ndoa zetu wanaJF?

Aliekuambia kuoa ndio mwisho wa kula hotelini nani? Na umejuaje km hawana matatizo ndani ya mahusiano yao?
 
Inasikitisha sana mtu kaoa tena ndoa ya kimungu na kwa heshima kubwa halafu unamkuta kwenye madanguro na mausiku klabu, kikubwa anatafuta malaya na hana ugomvi na mkewe kisa tamaa tu. kuna mana gani ya kuoa halafu unakuwa na tamaa kibao za wanawake wengine, ki ukweli hili linanichefua sana tena sana. wanaJF tuungane kuwashauri wanandoa wenye akili mbovu kama hizi....
Ni nani huyo? Lini alifanya hivyo? Wapi na kwa nani? Sema tumchape...!
 
Wewe ni HE au SHE?, umeoa/olewa?!. Ukiona baba anamucha mwenza kitandani na kwenda kwa wajasiliamali ujue huyu aliyeachwa ndani is a problem too.

sikubaliani na wewe hata kidogo gama wanaume wamekuwa na tamaa sana hata wawe na kitu kizuri wapii na hata wangekuwa na akili badala ya kukaa na kutafuta suluhu ndani anaendakutafuta malaya .so huwa wanaruka mkojo na kukanyaga mavi
 
kwa hiyo unamaanisha ndoa ni sex? na ukioa ukamkuta mkeo au mmeo hakuna ile kitu ndo mnaachana? au akipata ajali akawa functionless ndio ndoa inavunjika?

au unamaanisha wasiokuwa na ndoa ni sawa kwenda kwenye madanguro na kuchukua malaya? huyo Mungu anayeruhusu haya na kukataza yale ni yupi?
unazungumzia very very complicated subject which certainly you know nothing about it!

nani kakwambia mungu anaruhusu umalaya shauri yako
 
Sio wakware, tumekuwa wepesi kulaumu matatizo yanayoonekana ambayo chanzo chake huwa hakionekani na wengi hawapendelei kusema. Mtu tangu utotoni kazoe kamchezo ka kuwa na wanawake wengi, leo akitaka kuoa atatakiwa kulipa mafungu ya kumi tu, akifunga ndoa huo mchezo wa zamani anaacha kwa mechanism gani?

kuna sababu nyingi sana na kama ni GT inabidi kuangalia mzizi wa tatizo

1.malezi
2. kampani
3. saikolojia
4. financial
5. frustration za ndani ya nyumba na nje
6. Nature

wengine ni nature tu, I would say 99% of african male/men are born to bonkey many many women, that was before christianity and muslim to come ove to our continents

ukiangalia nature za mababu wetu walikuwa wanaona wake sita saba mpaka basi, vile vinasaba vyao vile viko mpaka leo hii na watu utakuta wana vinyumba vidogo tunawalaumu tu

Ili nature ibadilike wa kutatua ni kumpa Yesu maisha yako ili akuumbe upya , nje ya hapo is just wasting time tu kujadili topic ambayo hata mleta maada anajua fika na yeye ina mgusa.

muulize mtoa maada kama ameoa, muulize kama bado ameisha lala na wenzi wangapi, na kama ameoa alishalala nao wangapi hapo kabla! INATISHA!

yaaap ukweli mtupu kabisa only God is the solution to this problem hofu ya mungu hubadili hata yasiyowezekana kubadilika ur right budy
 
Tumwombe Mungu atuepushe na mambo mabaya. Na kama mtu hajaoa haruhusiwi kuchangia hii mada make haimhusu, asubiri mpaka atakapooa.
 
[QUOTE
=Elungata;2591935]aaha..ndoa kitu gani bana...upuuzi mtupu peoples are supposed to be free from flooshness called marriage[/QUOTE]


nadhani waombe radhi waliofunga ndoa. Huwezi kuwatukana watu kwamba ndoa ujinga! sidhani una akili sawa
 
mtoa mada ameweka shida yake hapa jamvini ili tumpe ushauri na maoni yetu, ninachoshindwa kuelewa, ni kwa nini badala ya kumsadiia tunajibu kwa namna ya kudhihaki?
Ninaungana na wengi waliosema kuwa suala la ndoa ni mtambuka kwa maana kwamba wengi hawajui. Wengine hudhani ndoa umuhimu wake ni tendo la ndoa, wengine watoto na wengine kula, kuvaa, kuishi vema na mambo kama hayo.
kwa msaada wa wengi, kwa mara nyingine na bila kuchoka, nawaomba mkitafute kitabu kiitwacho NDOA YANGU, NINGEJUA popote katika maduka ya vitabu, mtajua sababu ya watu wengi wanaolia leo ni ipi na kipi cha kufanya
 
Daa!!!!ndoa!!!!!!!!!!si rahisi kuisemea kwa kulaumu kama unavyosema,tena kwa kulaumu wanaume kwani hakuna wanawake wanaofanya hivyo???wewe ndio umeileta mada hii twambie ulifanya nini baada ya kuwaona/kumwona kwenye hizo sehemu uliwapa ushauri gani??mimi nimetanguliza kusema sio rahisi kihivyo maana wapo pia wanaolipiza visasi baada ya kupata taarifa za uhakika kuwa wake zao wana wanaume nje ya ndoa na wengine wamewafumania badala ya kuendesha kesi huamua kulipiza ili kumkomoa huyo mwanamke.Kwa mtu aliyepata masaibu hayo mara nyingi hawashauriki,bora wewe uliyewaona kwenye madangulo na wale wanaoishia na wapenzi wao wa nje ya ndoa kwenye mahoteli utawajuaje si nao wafanya uasherati?????kuna jirani yangu mmoja aliamua kufanya kama unavyoshauri aliishia kuambiwa ''wewe unatembea na mke wangu taarifa hizo ninazo''Jirani aliondoka kichwa chini.Yaliyomo ndani ya moyo wa mtu huwezi kuyatambua anasema hivi na anatenda vingine.
 
Pole saana ndugu yangu hakika inakera, maana huyu sio kwamba anapepo la ngono yeye ni pepo hati. watu wa haina hiyo wanahitaji maombi ya nguvu
 
bado sijaoa lakini hili suala linanikera sana, lakini mimekuelewa sana mungu akuongezee busara
 
Inasikitisha sana mtu kaoa tena ndoa ya kimungu na kwa heshima kubwa halafu unamkuta kwenye madanguro na mausiku klabu, kikubwa anatafuta malaya na hana ugomvi na mkewe kisa tamaa tu. kuna mana gani ya kuoa halafu unakuwa na tamaa kibao za wanawake wengine, ki ukweli hili linanichefua sana tena sana. wanaJF tuungane kuwashauri wanandoa wenye akili mbovu kama hizi....

watu wenye wivu mara nyingi ni mahawara, inawezekana wewe ni mmoja wao.
 
Back
Top Bottom