Hizi ndiyo shule zetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi ndiyo shule zetu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Nyani Ngabu, Mar 17, 2012.

 1. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hata mitaala ikibadilishwa namna gani, kama miundo mbinu itaendelea kuwa yenye hali kama hiyo inayoonyeshwa kwenye hicho kipande cha taarifa ya habari hapo chini, mabadiliko hayo yatakuwa ni kazi bure.

  Haya mazingira ni mabaya kupindukia. Si kwa wanafunzi tu bali hata walimu. Ni mtoto gani atakuwa na shauku ya kurudi shuleni kila asubuhi kujifunza mambo mapya? Ni mwalimu gani anapenda kufanya kazi kwenye mazingira kama hayo ambapo hata vyoo hakuna? Walimu na wanafunzi wanajisaidia vichakani. Daaaah!!!!!

  Kwa mfano tu, ili kuandika wanafunzi inawabidi wapige magoti na wapindishe migongo. Hayo ni mateso.Hakuna kitakachoingia akilini na kubaki.

  Halafu tunashangaa kwa nini wanafunzi wanafeli sana mitihani ya taifa wakati asilimia kubwa ya majibu tunayo. Hivi sisi ni nini tunachokiweza?

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Umesema kweli, hata tufanye kitu gani as long as tunaongozwa na watu wasiokuwa na nia ya dhati hatutakuwa na maendeleo. Inatia uchungu sana ukijaribu kujiweka katika adha wanazopata watoto hawa hapo ni shuleni tu bado hujafikiri mazingira ya nyumbani wanayoishi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. rwamashugi

  rwamashugi Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kodi za Makampuni ya Tumbaku ya Tabora zinepelekwa wapi???????????

  Inauma sana......
   
Loading...