Hizi Ndio Ndimi Mbili za Freeman Mbowe

Hizi Ndio Ndimi Mbili za Freeman Mbowe

Sipingi utetezi wako boss, na tunajua uchochezi wanaofanya sukuma gang ili kumfanya Magufuli abaki relevant. Je Mbowe hakutamka maneno ya watu kuandamana tena katika hali ya kuonyesha kutokukubaliana nayo? Ni mara moja au mbili Mbowe aliwahi kuhamasisha watu kuandamana huko nyuma?

Unataka watu waandamane kisa Mbowe kukamatwa, au kila mtu ahudhurie kesi ya Mbowe. Kwani kila mfuasi wa CDM aliyekamatwa Mbowe aliandamana au kuhudhuria kesi zao? Alipokuwa anatumia gari la umma na kupata mshahara wa ubunge na KUB, watu walikuwa wanamfuata na kufaidi alichofaidi? Walioweza kuhudhuria kesi ya Mbowe walihudhuria kutokana na nafasi zao, na mahali kesi ilipokuwa ikiendeshwa. Labda kama ulitaka wafuasi wote wa CDM waende hapo mahakamani.

Wote tunajua Samia ni tofauti na Magufuli, ila anachofanya Mbowe sasa ni kujiweka upande wa kujinyenyekeza zaidi kuliko kukaa eneo la kupata haki. Kuna mazingira makubwa Samia akamtumia sasa ili kutawala kwenye kipindi chake bila pressure kubwa. Lakini akitoka mambo yakaendelea vile vile. Tunachokataa ni Mbowe kutaka kujionyesha kwa serikali kuwa yeye ni mnyenyekevu, lakini wafuasi wa CDM ndio wenye tatizo. Kwa sasa Mbowe ushawishi wake uko chini, ni vyema akaacha wengine waongee kwani bado tuna imani nao. Mbowe ale alichopewa sio kulazimisha kuburuza watu huko atakako.
Ok mimi sio mwanachama wa CHADEMA, ila Mbowe alikaa muda mrefu sana gerezani hata kama alitoka.. Yaania alipokamatwa CHADEMA wangetakiwa kuonyesha reaction kubwa sana sio mtandaoni tu bali na mtaani
Kesi yake ilipokuwa inaendeshwa wangekuwa wanahudhuria hata watu 10,000 tu kushinikiza aachiwe na hata kama polisi wangewazingua wasingeweza kukabiliana nao, Mbowe asingemaliza hata mwezi gerezani angeachiwa, Polisi hawawezi kuua watu 10,000 wala kuwapeleka mahabusu, maana hazitatosha. na wangewajaribu kukabiliana nao hiyo ingekuwa ni aibu klubwa sana kwa Samia na angemuachia tu

Na sio lazima kiongozi aitishe maandamano, wanachama wanaojiongeza wakiona kiongozi wao au mwanchama wa kawaida tu anafanyiwa injustice wanajiongeza wenyewe kushinikiza hiyo injustice ikome haraka iwezekanavyo

Sasa unaposema na yeye kwani wanachama wanapokamatwa hakuhudhurii kesi zao, mbona anahudhuria nyingi tu, Sugu alipokamatwa, Mdude alipokamatwa, Lema na wanachama wengine Mbowe alikuwa akiwatembelea gerezani.
Alipokamatwa kama watu wangekuwa wakitia pressure aachiwe pale mahakamani ile kesi wala isingeedelea kwa muda mrefu ville

Unaposema mshahara wake sijui na gari lake alilopewa akiwa KUB hamkugawa, hapa ndio nakuona empty set tu, sasa Mbowe alikuwa hachangii chama? Mbowe amepoteza biashara zake kiasi gani kutokana na msimamo wake wa kisiasa? Hakuharibiwa mashamba yake kule Hai? hakubomolewa jengo la Bilcnas Dar? Account zake za benki hazikufungwa? yaani haya hayatoshi inatakiwa tena awe anawagawia mshahara? Na ni kiongozi wa chama gani ambaye anagawa gari na mshahara kwa wanachama?

Hivi jamaa angeamua kuungana na CCM na kutumia connection hizo kuomba favour kwa biashara zake kwani kuliko kutegemea huo mshahara wa KUB na gari ni ipi ingekuwa bora zaidi kwake kifedha?
 
Ok mimi sio mwanachama wa CHADEMA, ila Mbowe alikaa muda mrefu sana gerezani hata kama alitoka.. Yaania alipokamatwa CHADEMA wangetakiwa kuonyesha reaction kubwa sana sio mtandaoni tu bali na mtaani
Kesi yake ilipokuwa inaendeshwa wangekuwa wanahudhuria hata watu 10,000 tu kushinikiza aachiwe na kukabiliana na polisi waliokuwa wanawazingua, Mbowe asingemaliza hata mwezi gerezani angeachiwa, Polisi hawawezi kuua watu 10,000 wala kuwapeleka mahabusu, maana hazitatosha. na hiyo ningekuwa ni aibu klubwa sana kwa Samia na angemuachia tu

Na sio lazima kiongozi aitishe maandamano, wanachama wanaojiongeza wakiona kiongozi wao au mwanchama wa kawaida tu anafanyiwa injustice wanajiongeza wenyewe kushinikiza hiyo injustice ikome haraka iwezekanavyo

Sasa unaposema na yeye kwani wanachama wanaokamatwa hakuhudhurii kesi zao, mbona anahudhuria nyingi tu, Sugu alipokamatwa, Mdude alipokamatwa, Lema na wanachama wengine Mbowe alikuwa akiwatembelea gerezani.
Alipokamatwa kama watu wangekuwa wakitia pressure aachiwe pale mahakamani ile kesi wala isingeedelea kwa muda mrefu ville

Unaposema mshahara wake sijui na gari lake alilopewa akiwa KUB hamkugawa, hapa ndio nbakuona empty set tu, sasa Mbowe alikuwa hachangii chama? Mbowe amepoteza biashara zake kiasi gani kutokana na msimamo wake wa kisiasa? Hakuharibiwa mashamba yake kule Hai? hakubomolewa jengo la Bilcnas Dar? Account zake za benki hazikufungwa? yaani haya hayatoshi inatakiwa tena awe anawagawia mshahara?

Hivi jamaa angeamua kuungana na CCM na kutumia connection hizo kuomba favour kwa biashara zake kwani kuliko kutegemea huo mshahara wa KUB na gari ni ipi ingekuwa bora zaidi kwake kifedha?

Mbowe alipokuwa gerezani sisi wafuasi wake tulionyesha reaction kuanzia mahakamani, mpaka kwenye platfoam kelele zinakoweza kupazwa ikiwemo social media, na pressure ilifika. Ama unataka pressure iwe maandamano tu? Sio mara moja au 2 wafuasi wa CDM wameonyesha mshikamano kwa viongozi wao wanapopatwa na matatizo ikiwepo kuchangiwa fedha, na ushahidi wa hayo uooa wazi. Kuandamana ni jambo linalohitaji ujasiri sana, hasa kwenye hizi nchi zetu ambazo viongozi hawaoni hatari kutumia vyombo vya dola kufanya mauaji.

Hilo la kuhudhuria mahakamani, watu wengi wamekuwa wakihudhuria hiyo kesi japo mazingira sio mazuri. Je ulitaka kila mmoja aache shughuli zake, au watu wasafiri toka mikoani kila siku kwenda hapo mahakamani? Kwa tulifanikiwa kwenda hata kama sio kila siku, bado tumeonesha mshikamano wetu. Unaweza kufananisha umati uliokuwa unajitokeza kwenye kesi ya Mbowe na ya Sabaya? Huo ushirikiano ulioonyeshwa na wafuasi wa CDM unaashiria msukumo.

Hilo la kula mshahara wake mwenyewe, ww umetaka kuonyesha kwamba watu wamefaidika sana na Mbowe, hivyo wanatakiwa kila akipata changamoto basi watu wawepo pembeni yake. Ndio nikakuambia kwani huo mshahara wake tulikuwa tunakula wote, kiasi kwamba akipata uonevu basi tuache shughuli nyingine zote tukasimame naye huko mahakamani. Mawakili walikuwepo na tulichanga chochote tulichoweza, ulitaka wafuasi wote wa CDM wakaishi naye gerezani? Hizo biashara zake zilihujumiwa na wafuasi wa CDM, mpaka uziweke kwenye huu utetezi wako? Kama ni kufaidika na CDM, basi Mbowe ni mmoja ya wafaidika wakuu, hata akipata madhila kuhusiana na CDM ndio sehemu ya changamoto ya wito wake.

Kama akiona connection huko CCM anaweza kuendelea nazo kwani hakuna anayemzuia. Tunachojua akitoka nje ya mstari tunampotezea kama tulivyowapotezea wengine. Hapa naona unatumia historia yake kumtetea. Sisi lawama zetu kwake ni huu utapeli uitwao maridhiano, na sio hizo historia zake. Na kwa taarifa yako anaweza kuwa KUB kama ni lazima awe KUB kwa njia za haki, na sio hizo za kujinyenyekeza kwa Ccm.
 
wewe sijui unaelewa hoja ninayosema ama unazunguka tu, kuwa watanzania ni waoga na huwezi kuwategema kwenye harakati za kisiasa

Mfano Chadema ina wanachama active wangapi kwa mkoa kama Dar? labda tuchulie hata ni laki moja, kati ya hao laki moja, wangejitokeza hata watu 10,000 kwa siku mahakamani, Mbowe asingekaa hata mwezi pale, Polisi hawawezi kukamata watu 10,000 achilia mbali kuwaua, kelele za mtandaoni hazina effect ndio maana kiongozi mkubwa wa chama anakamatwa na kupewa mashataka bogus kama yale na kukaa gerezani karibia mwaka, Na serikali inaweza kumfanyia yoyote vile kama iliweza kufanya kwa mbowe na hakuna itakachofanywa

Mbowe ana matatizo yake binafsi ukiachana na haya ya kisiasa, anaweza kufiwa, kuuguliwa na ndugu ama vinginevyo, haya ni matatizo binafsi amabayo wanachama hawana ulazima wa kusimama nae, lakini matatizo kama ya kupelekwa jela na kufunguliwa kesi bogus za kisiasa hayo ni matatizo ya kisiasa na chama pamoja na wanachama wake wana wajibu wa kusimama nae kama hicho chama kinataka kuendelea kubaki na uhai, ama kim,eshajifia kama mawazo ya wanachama wake ndio haya

Wanachama wa wa CHADEMA ni madebe matupu mtandaoni, ambao kiongozi wao akipatwa na tatizo kutokana na msimamo wa chama, basi wanachama wanasema tuna shughuli za kufanya hatuwezi kwenda mahakamani, kwanza mshahara wake hatugawani hiki sio chama tena

Tubaki tu na CCM tulinde amani yetu.
 
Ukiacha uoga wa wanacdm, watanzania wote kwa ujumla wetu tuna nguvu gani ya kudai jambo na serikali ikaogopa? Tumepandishiwa Tozo kwa hadhithi kuwa ni za kujengea madarasa, hospitali nk, zaidi ya kelele ni nini tumefanya, wakati pesa za madarasa tumeenda kukopa na hakuna maelezo yoyote ya maana tumepewa?

Umeme kila mara unakatika, mbona hatujaona wanaccm wakiandamana kudai huduma bora ya umeme kama wanacdm ni waoga? Nenda huko mabarabarani, misafara ya viongozi ikipita watu wanasimamishwa hata masaa matatu mpaka kiongozi apite, zaidi ya wananchi kulalamika ni hatua gani wamechukua? Wafanyakazi hawakupandishiwa mishahara miaka 6 kinyume na sheria, ni nini walifanya? Wakulima wanapangiwa ama kuzuiliwa kuuza mazao yao watakako, mpaka yanaharibika, ni hatua gani wamechukua hadi serikali iogope? Wakulima wa korosho wameporwa korosho zao, ni kipi walifanya mpaka serekali ikaogopa?

Ni reaction ipi unaona ina
kosekana kwa CDM tu, ila kwa makundi mengine ya watanzania ipo? Amani iliyopo hapa nchini hailetwi na ccm, bali automatically watanzania ni makondoo.
 
Nimekuelewa
 
Attachments

  • IMG_20220605_081520.jpg
    IMG_20220605_081520.jpg
    57 KB · Views: 10
Naona Mbowe kabadili swaga kutokana na aina ya uongozi uliopo, ameamua kuendana na haiba ya mtawala aliyepo, nina wasiwasi anazubaishwa akija kushtuka 2024 hakuna chochote kilichofanyika ndipo atarudi tena kwa wananchi kulalamika, it will be too late.
 
Back
Top Bottom