Judi wa Kishua
JF-Expert Member
- Apr 15, 2012
- 1,066
- 1,048
Nimeamka asubuhi natoka kuelekea kazini. Nimefika kituoni nikakuta daladala imesimama inapakia abiria huku ikiwa tayari imejaa, nikaitwa nipande nikakumbuka AMRI ya serikali kwamba ni marufuku kusimamisha abiria.
Sikupanda nikasubiria nyingine nikazunguka nayo ndani ya daladala abiria tumejaa watu wamesimama hakuna ata pa kuweka mguu. Tunapita barabarani askari wa barabarani wanatutazama tofauti na nilivyohofu kwamba nikikutwa nimesimama nitapigwa faini na wala sioni anayejali.
Nafika ofisini nakuta magazeti tayari yameshafika naona vichwa vya habari waganga wa tiba asili wameigomea serikali na wanamkanya Waziri wa serikali aache kutaka sifa so hawapo tayari kutekeleza amri ya serikali, nikapekua habari iliyoandikwa ukurasa wa juu ya gazeti la mwananchi inaonyesha namna awa waganga wanavyotapeli wananchi..
Kwa habari hiyo ya uchunguzi inaonyesha kifaa ambacho kinatiliwa shaka kinauwezo wa kuchunguza mwili wa binadamu bila kuchukua damu wala kitu chochote mwilini na kutoa majibu ndani ya dakika tatu. Mwandishi kama sehemu ya uchunguzi anaonekana ana tatizo la ugumba ilihali ana watoto tayari alikuwa anawajaribu.
Nilishikwa na ganzi baada ya kusoma hiyo habari nikabaki najiuliza huu ujasiri wa kuigomea serikali wanautoa wapi? Na wanafanya utapeli kama huu bila woga?
Muda wa kazi ukafika tukaanza kufanya kazi ghafla nikakumbuka AMRI ya Waziri wa kazi kwa wafanyakazi wanaofanya bila vibali baada ya kumuona mfanyakazi mwenzangu kutoka Kenya akiendelea na kazi bila wasiwasi wowote na ukweli ni kwamba anafanya kazi bila ya vibali kuangalia around ofisi yote nakuta wale wakenya waliokuwa wanafanya kazi bila vibali bado wapo na hawana uoga wowote na boss wala hashtuki kuwatafutia vibali wapo zaidi ya ishirini(kumbuka deadline ya serikali imeshapita) .
Ndipo nikaanza kupatwa na hofu inamaana awa mawaziri wanapotoa matamko na maelekezo mbona yanapuuzwa? Wasiposikilizwa leo ni lini watasikilizwa? Tatizo ni maagizo hayatekelezeki au watanzania hawapo tayari kwa changes? Au mawaziri hawakujipanga kusimamia utekelezaji? Au Magufuli yupo ahead of time ambapo watanzania awako tayari kufika kwa sasa bado wanataka kufurahia comfort zone?
Sina mashaka kabisa na Magufuli katika kusimamia mambo yake sababu ana historia hiyo ila nimeanza kupata mashaka na mawaziri kama haya mambo ya kusimamia taratibu wataweza au wanajilazimisha ila hawawezi.
Ni hayo tu, kazi njema!