Hizi ndege ziendelee kukamatwa tu mpaka pale tutapojenga nidhamu na utamaduni wa kulipa madeni ya watu wakiwemo na watumishi wa ummaM

Salary Slip acha wakunyooshee vidole lakini ndio ukweli, kesi hii imetutia aibu kama nchi.
Naibu waziri wa mambo ya nje kaenda kukaa huko wiki nzima kwa sababu ya kukomboa Mali yetu iliyoshikwa sio kwa uonevu, bali kwa kutaka kudhulumu deni tusilipe.
Huku nyumbani tunawadhulumu waalimu, waganga na makandarasi tunaona sifa na kwa vile huu ni utawala wa kiimla kama Korea Kaskazini hawana la kufanyà.
Kukamatwa kwa ndege sio mwisho bali ni mwanzo tuu kwani madeni huko nje ni mengi mno
Tumekuwa taifa la watu wa ajabu tunaothamini vitu kuliko utu.

Mimi siwezi kuunga mkono hali hii hata kidogo.
 
Wewe Mwenyewe Maliza kwanza deni lako la HESLB
Mimi nashauri wale wote wenye madai halali dhidi ya serikali kulingana na makubaliano/mikataba tulioingia waendelee tu kukamati hizi ndege kama njia ya kulazimisha hii serikali kulipa madeni ya watu mpaka pale tutakopojenga nidhamu na utamaduni wa kulipa madai na haki za watu kwa wakati.

Aibu tunayopata labda itatufanya tubadilike kwani kutolipa watu haki zao kwa wakati ni kitendo cha dhuluma hivyo ni sahihi tu zikamatwe tupate aibu ila tujifunze.

Watumishi wa umma ni kundi la watu wanaoathirika sana na utaratibu wa serikali za CCM kulipa madeni ya watumishi kwa jinsi wao wanavyoona inafaa hata kama itachukua miaka kadhaa tena bila kuwafidia usumbufu wanaousababish kwa maana ya kulipa na adhabu.

Nimetoa mfano wa watumishi wa umma kuonyesha ni jinsi gani hizi serikali za CCM zisivyoona umuhimu wa kulipa madeni kwa wakati ila wewe mwananchi ole wako usilipe kodi ya serikali utashughulikiwa mpaka ukome.

Kuna watu/watumishi wanadai serikali kwa miaka kadhaa na mpaka wanafariki hawajalipwa madai yao(namfahamu mmoja) hivyo njia sahihi ni kutumia tu mbinu kama hizi za kukamata mali za serikali.

Hapa tusisahau na wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao nao tumeona wakillalamika kutolipwa haki zao kwa miaka mingi tu na mpaka sijui hata nini kinaendelea kuhusu malipo ya hawa wazee.

Kwasababu tunaumizwa zaidi na ndege kukamatwa kuliko kuumizwa na taba za watu wanaosotea madai yao kutoka serikalini,wacha tu hizi ndege ziendelee kukamatwa ili na uppande wa pili nao wafili maumivu kama wengine.

Hata tukishinda kesi za mali zetu kukamatwa teyari ni aibu tosha na deni bado linakuwa pale pale huku dunia nzima inajua tunadaiwa na kuhisi pengine tulitaka kudhulumu haki za watu(aibu)!!.

Uzalendo wa kinafiki kwangu hauna nafasi.
 
Chadema mnamawazo ya kiuaji sana dhid ya taifa hili kwakweli mtaendelea kuwekwa benchi hadi muwe na uzalendo
 
Eti tumenunua kwa pesa zetu.

Ni Mtanzania gani aliyeiona / kuijua mikataba ya ununuzi wa hizo ndege?

CAG jicho la Watanzania, BUNGE ndiyo Watanzania, je, wanaruhusiwa kuhoji juu ya hizo ndege?

TAFAKARI, CHUKUA HATUA.
 
Tupo njiani tunakuja home. Nyumbu jinyongeni kwa makamasi...
IMG-20190904-WA0020.jpeg
 
Acha ujinga wewe kabla ujapost shirikisha ubongo nawatu wenye akiri walio karbu nawe
Hana akili huyo. Unapoteza muda wako bure. Mwache kama alivyo.
Umekosa uzalendo ndugu yangu. Hizi ndege tumenunua watanzania wote kwa kodi zetu, ni mali yetu wote. Sasa zikikamatwa unamkomoa nani?
Kuna tofauti kati ya mtoa hoja na mtoa povu, wewe ni mtoa povu
Hamjalazimishwa kukubaliana na mawazo yake nyie Kima.....
 
Hahahahaha labda aamue kuachia $33 millions zake lakini akienda hapo London kwenye korti ya Kimataifa na kuonyesha hukumu ya Tanzania ya kuitaka Tanzania kumlipa fidia na Tanzania ilikuwa imeshaanza kumlipa hadi 2014 na kuiomba mahakama hiyo ya Kimataifa imsaidie apate haki yake ya $33 millions kesi inarudi pale pale na ATCL wataanza kwenda London karibuni ndege hiyo ipo hatarini kukamatwa tena.

Mkulima wenu analipa gharama za kesi na deni lote linaishia hapo!
 
Ukizikamata ushinde na hiyo kesi yenyewe, kama nawaona hao watanzania waliojitia kiherehere kufungua kesi S.A, tayari walikuwa wanasubiriwa kwa kesi ya uhujumu uchumi ata kama wangeshinda.

Sasa tena ushindwe na huko ulipopeleka madai uamriwe uilipe serikari yako, jamaa wakifanya mchezo serikari inakomba asset zao zote kufidia deni walilojitafutia including nyumba zao. Bado na kesi ya uhujumu uchumi juu kasheshe.
 
Kuna mambo yanasikitisha sana...

Kuna makampuni yanafanya biashara na serikali, na hayajalipwa hata senti...

Cc: mahondaw
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom