Hizi methali zina maana gani??

Hizi methali zina maana gani??

brigedia mafia

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2016
Posts
2,260
Reaction score
2,279
1:Mlilala handingwa handingwa mwenye macho haambiwi tule



2: Pema usijapo pema ukipema si pema tena


3:Mwenda tezi na omo marejeo ngamani


4:Oteo ulisemaje, nipe nikupe


5:Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno


6:Utamu wa funza kukata kidole

7:Konzi mwana mandanda kulala njaa kupenda


8:Maji ya kifuu ni bahari ya chungu

9:Mchama ago hanyeli


10:Shimo la ulimi mkono haufutiki
 
3 : matumizi , mtu ataruka ruka sana Ila atarudia pale pale sehemu muhimu.( tezi , omo ngama ni sehemu za jahazi)
5 : Chungu /nyenyere/ sisimizi : mtu ukifanya jambo Na kuliona la kawaida mwenzio akilifanya hilo hilo kwake huliona kubwa.
8 : maji kidogo kwako ni mengi kwa mwengine ( kifuu kwa mtu ni kidogo Ila kwa sisimizi ni mengi.
9 : mcha mago hanyele hwenda akawia papo !! ( Anaeondoka sehemu asitukane, pengine atarudia hapo hapo ).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom