Hizi Home theatre zinatengenezwa kwa teknolojia gani?

Aiseeee, mziki ukiwa mzuri unavutia asikwambie mtu
Hiyo ni Sound systerm miziki yote mizuri inategemea una sound systerm gani unaweza ukenda pahali ukasikia nyimbo utafikiria debe bovu na vile vile unaweza kwenda sehemu ukasikia nyimbo utafikiria unaelea hewani ukajikuta unacheza bila kutaka na mpk muimbaji ukata kujua nani huyu.
 
Mkuu hapa kwa kuwa mada ni HT inabidi uchangie kwa upande huo , ila honestly hata mie Sijawahi kuzikubali Home theatre, nyingi wame focus kwenye details za high na low , sio midi. kwa hapa bongo , mie ni muumimi wa maredio flan ya mtumba kutoka japan hayanaga sura na si rafiki sana kwenye bill za umeme Ila they rock!!
Get bluetooth aptx receiver na Hilo dude halafu upate na madilu system album , unaeza fikiria madilu mwenyewe ndo yupo sebuleni kwako anakutumbuiza
 
Zinapatikana wapi mzee?
Hizo zitanifaa. Mimi ni kijana mdogo najihusisha na kazi za muziki pia ila hua nikijisikiliza kwenye redio yangu hua nakata tamaa kabisa. Ila studio nikijiskiloza hua ni fresh tu
 
Hivi siku hizi hamna FM zenye stereo. Maana ile taa siku hizi haiwaki ilikuwa inawaka kipindi kile radio one ya kina Mike Mhagama na kina Flora Nducha
Niliwahi kummuliza jamaa mmoja wa Rfa kuhusu music quality wa radio yao kiss fm , Kama unakumbuka haikuwa na quality nzuri kulinganisha naradio zingine, alichoniambia ni kuwa ni gharama sana kutangaza sterio broadcasts, inawezekana radio nyingi zimeachana nayo.
 
Zinapatikana wapi mzee?
Hizo zitanifaa. Mimi ni kijana mdogo najihusisha na kazi za muziki pia ila hua nikijisikiliza kwenye redio yangu hua nakata tamaa kabisa. Ila studio nikijiskiloza hua ni fresh tu
Kariakooo Kuna mkongo mmoja anaziletaga , Ila wakati fulani zinaishia na unaweza kukuta ni za kusubiri .
Zamani zilikuwa nyingi sana niliinunua moja mwaka 2007 Hadi leo ipo na ya mwisho nimenunua mwaka 2014 , nilienda tena mwaka juzi baada ya speaker moja kuliwa na panya , akaniuzia pair moja,
 
Naomba picha inisaidie kuifaham nataka niitafte mkuu
 
Tatizo Home theater nying saiz za kariakoo feki...huenda na yako sio..au kama yenyew basi kuset imekutoa nishai..mcheki Extrovert akusaidie

Sent from my SM-G920P using JamiiForums mobile app
 
Wala haja overate hyo jbl..kaongea ukwel vitu inafanya hyo kampuni...hizi brand zote kubwa ni wakali...yani bose,jbl, Harman,denon,sonos,kliepch etc hao wote maninja wa mziki

Sent from my SM-G920P using JamiiForums mobile app
 
Wala haja overate hyo jbl..kaongea ukwel vitu inafanya hyo kampuni...hizi brand zote kubwa ni wakali...yani bose,jbl, Harman,denon,sonos,kliepch etc hao wote maninja wa mziki

Sent from my SM-G920P using JamiiForums mobile app
Nadhani hujanielewa , sijakata kuwa Jbl ni za kibabe , nilichokuwa najaribu kusema sio jbl pekee ,bali Kuna wababe wengine

Ukitaka kuprove hilo jaribu kuchunguza expensive cars zinafungwa music sytem ya bose au B&o for reasons, Jbl as music system Mara nyingi naiona inakuja kwenye gari za japan
 
Mziki wa kukupa hizi detail ni lazima uwe na Dedicated Amp, sio zile integrated Amps.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…