Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
MAFUTA na gesi asilia ni rasilimali ambazo zimekuwa mkombozi kwa mataifa mengi ya Afrika ingawa mataifa ya Magharibi yamekuwa yakinufaika zaidi kuliko hata nchi zilizo na rasilimali hizo.
Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba, rasilimali hizo, kama ilivyo kwa madini, zimeanza kutafutwa na mataifa ya Ulaya tangu bara hilo likiwa bado linatawaliwa na wakoloni ambao wana utaalamu kuliko nchi za Afrika.
Pamoja na kukosa utaalamu ama kuwa na wataalamu wachache, lakini mataifa ya Afrika yenye kuzalisha mafuta na gesi yameweka misingi ya kusimamia rasilimali hizo ikiwemo sheria na kanuni mbalimbali.
Tanzania, kama miongoni mwa nchi zenye rasilimali hizo, nayo imeweka taratibu mbalimbali za kusimamia mafuta na gesi asilia ambayo mpaka sasa imegundulika kiasi cha futi za ujazo trilioni 57.
Kwa habari zaidi, soma hapa => http://www.fikrapevu.com/hizi-ndizo-sheria-zinazosimamia-mafuta-na-gesi-asilia-katika-nchi-za-afrika/