Mangi flani hivi
JF-Expert Member
- Jan 2, 2016
- 2,026
- 3,104
Katika kutimiza haja zangu za kirijali leo nimejikuta namtupia mistari binti mmoja maarufu humu ukumbini kwa mfumo wa PM. Sikupata adha ya kuporomoshewa mitusi Kama wadau wengine wanavyolalamikaga kuwa ukimPM binti humu ndani anakumwagia mitusi. Hali ilikuwa shwari mpaka ulipowadia Muda wa kubadilishana contact. Nilipoiweka namba yake kwenye kisemeo changu, lahaula...kumbe ni ni ndugu kabisaaaa...Hali kadhalika na kwake. Tumeombana misamaha na ninaamini yatabaki pale pale. Tuwe makini wadau unaweza tongoza Mkeo. Naamini anaisoma hii sredi, sister..nimeiweka hapa ili iwe fundisho kwa wengine.