Hizbollah; Israel kuanzia sasa ikishambulia itapata majibu makali zama zake za kukaliwa kimya zimepita

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,064
18,053
Hizbullah: Zama za Israel kufanya mashambulizi bila majibu zimepita
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, zile zama za utawala wa Kizayuni wa Israel kufanya mashambulizi na kuachiwa vivi hivi bila ya majibu zimeisha na kuanzia sasa shambulio lolote la Wazayuni litajibiwa vikali.
Sheikh Naim Qassim amesema hayo baada ya jeshi la Syria kutungua ndege ya kisasa ya Israel aina ya F-16 ikiwa ni mara kwanza kabisa kutunguliwa ndege ya Israel tangu utawala huo pandikizi ulipoanzisha mashambulizi dhidi ya Lebanon mwaka 1982.
Jumamosi asubuhi ndege za kivita za utawala wa Kizayuni ziliingia kinyume cha sheria katika anga ya Syria kama kawaida yake kwa muda mrefu sasa, na kushambulia baadhi ya maeneo katika viunga vya Damascus, kusini mwa Syria. Kikosi cha makombora cha jeshi la Syria kilijibu uvamizi huo kwa kuzishambulia ndege hizo za utawala dhalimu wa Israel na kufanikiwa kuzipiga ndege mbili za kivita za utawala wa Kizayuni ambapo ndege moja ilianguka na kuteketea kabisa.
Shirika la habari la IRNA limemnukuu Sheikh Naim Qassim akisema kuwa, kutunguliwa ndege hiyo ya Israel kunatoa ujumbe muhimu wa kwamba kuanzia sasa hakuna shambulio lolote la Israel litakaloachiwa vivi hivi bilal y kujibiwa.
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni hivi sasa uko katika wakati mgumu zaidi kwani uamuzi wowote wa vita hauna matokeo yaliyo wazi kwa Israel. Ameongeza kuwa, leo hii Lebanon imekuwa imara zaidi kuliko huko nyuma kwa baraka za wanamapambano wa muqawama.
Amesema, lau kama kambi ya muqawama isingelikuwepo, leo hii utawala wa Kizayuni wa Israel ungelikuwa umeingia katika nchi zote za eneo hili.
 
Back
Top Bottom