We mdada, hilo pochi ulilobeba kubwa kama kapu la kuendea sokoni na lina manembo ya LV, GUCCI n.k halafu umelinunua elfu 60 za kitanzania, hilo ni FEKI..!! Huwezi kupata WALLET mpya original ya GUCCI au LV kwa chini ya Tsh 150,000 achilia mbali pochi. We libebe tu, ila ushajua..
Bro, hiyo buti uliyopiga yenye chata ya Timberland halafu umeuziwa Tsh. 70,000.. hiyo ni FEKI bro.. Huwezi pata original Tims kwa chini ya Tsh. 300,000 hapa duniani..!
Kijana, hakuna JEANS orijino yenye nembo kama LEE, LEVIS n.k ambayo inauzwa Tsh.45,000! Acha kuchekesha. Jeans orijino ni kuanzia Tsh. 180,000 na kuendelea.. We ukiona umeipenda nunua tu, ila ujue ni FEKI!
Jamani, hata ufanyeje huwezi kukuta MAWANI (sijui miwani?) ya jua orijino yenye nembo kama RayBan, inauzwa 30,000!! We ukikuta hiyo jua tu ni FEKI..! Tena jitahidi uwe unaivaa usiku.. wajanja wasikuone
Tuseme tuu ukweli. Karibu SAA zote za mikononi zinazouzwa madukani hapa bongo ni FEKI!! Eti unakuta ROLEX inauzwa Tsh 250,000.. ROLEX!!
Bandugu, hakuna SUBWOOFER mpya ya SONY, au BOSE inayouzwa elfu themanini za kitanzania ambayo ni orijino! Hebu acheni vituko..?
Kuna hizi raba simple hizi CONVERSE. Kila mtu anavaa siku hizi. Sasa ni hivi.. Converse orijino kiwandani ni kuanzia US $40 na kuendelea.. Ukikuta sehem wanaziuza Tsh 25,000 we nunua tu, ila ni FEKI hizo!
Braza, ni vigumu kupita maelezo kukuta koti la suti la LEATHER, au CORDUROY (kodrai) au VELVET dukani na liwe orijino. Kama unataka aina hiyo ya makoti tafuta kwenye mitumba. Vinginevyo utaishia kuuziwa FEKI tu, tena kwa bei ghali..!
GODORO orijino la Tanfoam la 5 kwa 6 haliwezi kamwe kupatikana popote nchini Tanzania kwa Tsh 75,000. Unauziwa FEKI!
Kuwa makini sana na hizi PERFUME zenye majina kama Lacoste, Hugo Boss, Polo, Gucci, Armani, Paco Rabbane n.k ambazo zinauzwa mitaani. Nyingi ni FEKI! Kwa wastani, bei ya perfume hizo tajwa original sio chini ya Tsh 150,000 kwa 30mls. We nunua hiyo ya 25,000 ila ujue ni FEKI!
Ukiona sehemu wanauza FENICHA.. na katika kuangaza angaza macho huoni MAFUNDI wenye zana kama RANDA, MISUMENO au PATASI hapo karibu, ujue kuna uwezekano mkubwa ukawa unanunua FEKI!
PIGA UA huwezi kupata earphones orijino za ibeats kwa Tsh 15,000 mahali popote duniani! Hizo ni FEKI!