Hiyo ni fake!

Hiyo ni fake!

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
6,710
Reaction score
20,706
We mdada, hilo pochi ulilobeba kubwa kama kapu la kuendea sokoni na lina manembo ya LV, GUCCI n.k halafu umelinunua elfu 60 za kitanzania, hilo ni FEKI..!! Huwezi kupata WALLET mpya original ya GUCCI au LV kwa chini ya Tsh 150,000 achilia mbali pochi. We libebe tu, ila ushajua..

Bro, hiyo buti uliyopiga yenye chata ya Timberland halafu umeuziwa Tsh. 70,000.. hiyo ni FEKI bro.. Huwezi pata original Tims kwa chini ya Tsh. 300,000 hapa duniani..!

Kijana, hakuna JEANS orijino yenye nembo kama LEE, LEVIS n.k ambayo inauzwa Tsh.45,000! Acha kuchekesha. Jeans orijino ni kuanzia Tsh. 180,000 na kuendelea.. We ukiona umeipenda nunua tu, ila ujue ni FEKI!

Jamani, hata ufanyeje huwezi kukuta MAWANI (sijui miwani?) ya jua orijino yenye nembo kama RayBan, inauzwa 30,000!! We ukikuta hiyo jua tu ni FEKI..! Tena jitahidi uwe unaivaa usiku.. wajanja wasikuone

Tuseme tuu ukweli. Karibu SAA zote za mikononi zinazouzwa madukani hapa bongo ni FEKI!! Eti unakuta ROLEX inauzwa Tsh 250,000.. ROLEX!!

Bandugu, hakuna SUBWOOFER mpya ya SONY, au BOSE inayouzwa elfu themanini za kitanzania ambayo ni orijino! Hebu acheni vituko..?

Kuna hizi raba simple hizi CONVERSE. Kila mtu anavaa siku hizi. Sasa ni hivi.. Converse orijino kiwandani ni kuanzia US $40 na kuendelea.. Ukikuta sehem wanaziuza Tsh 25,000 we nunua tu, ila ni FEKI hizo!

Braza, ni vigumu kupita maelezo kukuta koti la suti la LEATHER, au CORDUROY (kodrai) au VELVET dukani na liwe orijino. Kama unataka aina hiyo ya makoti tafuta kwenye mitumba. Vinginevyo utaishia kuuziwa FEKI tu, tena kwa bei ghali..!

GODORO orijino la Tanfoam la 5 kwa 6 haliwezi kamwe kupatikana popote nchini Tanzania kwa Tsh 75,000. Unauziwa FEKI!

Kuwa makini sana na hizi PERFUME zenye majina kama Lacoste, Hugo Boss, Polo, Gucci, Armani, Paco Rabbane n.k ambazo zinauzwa mitaani. Nyingi ni FEKI! Kwa wastani, bei ya perfume hizo tajwa original sio chini ya Tsh 150,000 kwa 30mls. We nunua hiyo ya 25,000 ila ujue ni FEKI!

Ukiona sehemu wanauza FENICHA.. na katika kuangaza angaza macho huoni MAFUNDI wenye zana kama RANDA, MISUMENO au PATASI hapo karibu, ujue kuna uwezekano mkubwa ukawa unanunua FEKI!

PIGA UA huwezi kupata earphones orijino za ibeats kwa Tsh 15,000 mahali popote duniani! Hizo ni FEKI!
 
duuu
mkuu magar na vitu vitu vingine vipi, ongezea ongezea vitu pendwa vingne.
 
huwezi tafuta vitu original kwenye nchi ambayo tunadumu tu hatuishi.

kuna vitu inabidi uwe unaongea na kina tibaijuka nk.
tusiponunua hivyo feki wafanyabiashara wetu wataacha kwenda china hivyo maskini tutakuwa wengi.
 
............Daaah! sisi wenyewe FEKI, kwa nini tusiuziwe vitu FEKI. Mkuu, umeongea ukweli mchungu.
 
duuu
mkuu magar na vitu vitu vingine vipi, ongezea ongezea vitu pendwa vingne.

Hahaaa.. mkuu hauwezi kusema umenunua gari JIPYA wakati ODOMETER inasoma kilometa 80,000! Na umelinunua USD 1800. Hilo ni USED mkuu.. Toyota Vits mpya orijino inauzwa takriban USD 20,000 kabla ya usafiri na kodi..!
 
Kila kitu ni feki siku hizi, hata bikra zipo feki.

Hata wowowo zipo feki nyingi.

Hata ........... nazo ni feki.
 
Katika vyooooooote..........nimependa kodrai.......dadeki nina langu nikipiga. ........utadhani ni mmoja wa members wa Boney M......... hilo nililitoa kiborloni.......sh 2800.......nadhani ni full original.......... .
 
tumeanza kutumia fake tangu wachanga is our culture
 
Bidhaa znatengenezwa kulingana na soko husika.
Pia Cocacola ya tz uwezi linganisha na ya UK au USA, je ni FAKE ?
 
Lengo lako kuanzisha huu uzi ni nini???
 
hata papuchi siku hizi zipo feki kibao tu ila cha ajabu utamu ni ule ule tu.

manyonyo nayo feki,

wowowo nazo ni feki,

ngozi feki,

nywele feki,

meno feki,

macho feki,

pua feki,

midomo feki,

kucha feki,

miguu feki,

bado utumbo tu.
 
Back
Top Bottom