Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,156
Tulimsikia wenyewe Rais wetu Magufuli akiwaahidi wajasiriamali wa samaki pale Ferry kuwa atawaletea pesa shilingi milioni 20 ili ziwaaaidie katika kuinua msingi wa biashara yao
Hapo hapo tukamsikia Mama yetu Janeth Magufuli naye akiahidi kutoa shilingi milioni 5 kwa wajasiriamali hao
Swali ninalojiuliza hivi hizo pesa zitatoka mifukoni mwao au zinatoka kwenye Hazina yetu ya Taifa?
Ikiwa pesa hizo zinatoka kwenye hazina yetu ya Taifa atueleze Mheshimiwa Rais ni lini Bunge letu liliidhinisha pesa hiyo kutolewa kwa wajasiriamali hao?
Kama pesa hizo zinatoka mifukoni mwake Mheshimiwa Magufuli, basi yeye ni mtu mwenye ukwasi mkubwa hapa nchini
Na kama pesa hizo zitakuwa zinatoka kwenye Hazina yetu ya Taifa bila kuidhinishwa na Bunge letu, hayo ni matumizi mabaya kabisa ya madaraka kwa Rais wetu na hapo ndipo hata ile hoja ya Mheshimiwa Zitto Kabwe inazidi kupata nguvu........
Kutumia ibara ya 37(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2005
YAJAYO YANASIKITISHA SANA!