Bwana Mwera hapa naona umenipa mwanga nilioutaka. Yaani hii ni kiboko kweli! Tofauti na miaka ya nyuma, mwaka huu CUF walikaa kimya tulii, kwa ajili ya muafaka waliowekeana Zanzibar, wanajua nao ulaji wataupata. Na sasa kwa mtaji huo inanifanya niamini hata bara huku Dr Slaa alishinda! CCM hawashindwi lolote lile. Lakini kwa upande mwingine CUF hawakutakiwa kukubalikudhulumiwa eti kisa ni kulinda amani, hii inaonyesha kuwa viongozi CUF nao pia ni njaa kali. Kama waliamua kulinda amani walitakiwa waweke wazi ili umma wa Wazanzibari wajue kuwa mshindi alikuwa ni Seif na si Shein! Kweli pesa na madaraka ni sabuni ya roho! CUF sahivi kimya na tuli, wamemegewa pande la keki nao wakauza utu, haki na uhuru wao. Je mnategemea maslahi ya Wazanzibar yatatetewa iwapo CUF ishanunuliwa na CCM?