Elections 2010 Hivi zenji nako ushindi wa rais ulikuwa wa cuf ukaporwa na ccm?

Nov 6, 2010
8
0
Inasemekana na Zenji, maalim Seif Shariff Hamad alikuwa ameshinda kiti cha urais akalazimishwa kukubali matokeo na JK na jeshi ndipo akaanguka saini kukubali ye ni wa pili, kuepusha usalama wake na maafa kwa Wazanzibar, uku akiahidiwa dili kedekede.

Na ndo maana maalim siku ile alipotangazwa Shein mshindi alisema hamna mshindi, akimaanisha ye pia ni mshindi!

Pia eti CUF na CCM eti ni damudamu. Dugu moja!

Is it true?
 
Duh!Inawezekana!Mh!Kama ni kweli.Mungu saidia,manake Tanzania itakuwa imetafunwa kabisa na CCM mafisadi na!
 
Maalim seif sharif hamad wa cuf alishinda kwa kura 211000,na shein wa ccm akapata kura 161000 huo ndio ukweli usio na chembe ya shaka,seif tokea uchaguz wa 1995 anashinda chaguz zote ila wanamuibia kura wanampora wanatangaza wa ccm,aliamua yaishe kwamana ccm walikua tayari kwalolote hata kwavita kuua watu,muungwana seif akaona akubali kuepusha janga na balaa ktk nchiyao ya zenj,nihakika muungwana huyu hana uroho wa madaraka,taifa mbele tamaa baadae.mungu yupo inshaalah atamlipia.
 
ccm walisema mapema ushindi ni lazima, hamkuwauliza kwanini mnatoa kauli hiyo! mapinduzi daima! basi hayo ndio waliokusudia.
 
Hili nalo bana, kesho utaliona linacheka na akina CCM hao hao wanao mfanya kitu mbaya kila miaka 5.

Dr wa kweli sasa hivi hacheki nao na utaona moto unaowaka.

Safari nyingine sidhani kama watathubutu. Ukicheka nao wao wanakuumiza mwisho wa siku.

Maalim naamini maneno ya Mwanakijiji kuwa "anaihitaji zaidi CCM kuliko CCM inavyomuhitaji yeye....."

Anauhitaji pia Muungano zaidi ya sisi Watanganyika. Sijajua tu hadi leo kwa nini iko hivyo.

Kama kweli CUF wangelinguwa ni UPINZANI, ungeliona wanavyoshiriki na Chadema.

Ila utashangaa akina Mwiba kuja kumshambulia hapa Slaa na kesho wanalialia kuwa wanaibiwa.

Walikubali KULA kidogo na sasa Acha na wao waliwe saaana. Slaa U-Angican hautaki kabisaa.

8D6U9904.JPG
 
Ninavyoona mimi hii nchi ni ya mfumo wa chama kimoja ktk sura ya vyama vingi.
Ccm ndio watawala wa maisha ktk ngazi ya uraisi.
 
Bwana Mwera hapa naona umenipa mwanga nilioutaka. Yaani hii ni kiboko kweli! Tofauti na miaka ya nyuma, mwaka huu CUF walikaa kimya tulii, kwa ajili ya muafaka waliowekeana Zanzibar, wanajua nao ulaji wataupata. Na sasa kwa mtaji huo inanifanya niamini hata bara huku Dr Slaa alishinda! CCM hawashindwi lolote lile. Lakini kwa upande mwingine CUF hawakutakiwa kukubalikudhulumiwa eti kisa ni kulinda amani, hii inaonyesha kuwa viongozi CUF nao pia ni njaa kali. Kama waliamua kulinda amani walitakiwa waweke wazi ili umma wa Wazanzibari wajue kuwa mshindi alikuwa ni Seif na si Shein! Kweli pesa na madaraka ni sabuni ya roho! CUF sahivi kimya na tuli, wamemegewa pande la keki nao wakauza utu, haki na uhuru wao. Je mnategemea maslahi ya Wazanzibar yatatetewa iwapo CUF ishanunuliwa na CCM?
 
Kwenye RED: Hata sitegemei!!
 
Ninavyoona mimi hii nchi ni ya mfumo wa chama kimoja ktk sura ya vyama vingi.
Ccm ndio watawala wa maisha ktk ngazi ya uraisi.
Mungu akuongezee busara uzidi kuona mbali zaidi ya hapo, wasioona hilo ndio wale niliosema WANA UPOFU WA MOYO:glasses-nerdy:
 
ni wazi kwamba maalim seif alikua ameshinda, na safari hii tume haikua na kazi sana, coz seif mwenyewe alishataarifiwa kuwa ameshinda ila atapokwa ushindi.

na kielelezo cha msingi zaidi ni kwamba dr. Shein amemteua aliyekua makamu mkuu wa tume ya uchaguzi kuwa mwanasheria mkuu wa zanzibar, bila shaka ni kulipa fadhila..
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom