Maalim Seif: Lipumba anatumika na Chama Tawala(CCM) kudhoofisha Upinzani

Sep 29, 2016
34
83
KATIBU MKUU, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA HOTELI YA RAMADA:

=========

WhatsApp Image 2017-04-09 at 11.35.02.jpeg


11:30: Maalim anaanza kuzungumza

Nimekuja kufichua mbinu chafu za Lipumba"

Takriban wiki sasa nimekuwa na ziara ya kuimarisha chama Unguja na Pemba. ⁠⁠⁠Nimekatisha ziara ili kuja kuzungumza nanyi na dunia kwa ujumla.

⁠⁠⁠Hii hali inayoendelea inaweza kuingiza nchi yetu katika mgogoro mkubwa.

Mgogoro wa CUF ni hujuma zinazofanywa na chama Tawala. Ni hujuma zinazopangwa na kuendeshwa na dola ili kuua upinzani nchini na kunyamazisha kila kauli inayothubutu kuikosoa Serikali.

⁠⁠⁠⁠Lengo la mkakati huu sio CUF bali ni kuua UKAWA na upinzani. Hujuma hizi zinaelekezwa kwa bunge, vyma vya siasa, na taasisi zinazosimamia haki, watumiaji mitandao ya kijamii, wasanii, vyombo vya habari na wanasiasa wanaothubutu kusimamia wanachokiamini.

⁠⁠⁠⁠Kuthibitisha ninayosema tuangalie mtiririko wa njama ovu za kutaka kuua demokrasia kwa kunyamazisha wote wanaokosoa utawala wa 2015
⁠⁠⁠⁠
1. Kupiga marufuku mikutano ya hadhara.

2. Kuzuia live bungeni.
⁠⁠⁠⁠
3. Kufinya bajeti za shughuli za bunge hasa kamati iki zishindwe kuibana serikali.
⁠⁠⁠⁠
4. Kuwakamata na kuwalaza ndani wabunge wa upinzani hasa wale wanaoonekana ni mwiba kwa serikali.
⁠⁠⁠⁠
5. Kuzipa mahakama maagizo hadharani jinsi ya kuamua kesi na kuwaahidi fedha kama watekeleza matakwa ya watawala
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠6. Kuwakamata na kuwaweka ndani watumiaji ya mitandao ya kijamii wanaokosoa watawala kwa kutumia sheria ya cybercrime
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠7. Kuwatisha waandishi wa habari na vyombo vinavyoikosoa Serikali. Tumeshuhudia watawala wakivamia vituo vya redio

8. Kuwatisha na kuwakamata wasanii wanaowakosoa watawala
⁠⁠⁠⁠
9. Kuzitisha jumuia za kiraia zinazotetea haki za binadamu ili kuzitisha kutimiza wajibu wao mfano TLS ambayo ilitishwa na Waziri kukifuta. Mawakili wametishwa hasa wale wanaowatetea watu fulani.

⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠10. Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kujipa mamlaka wasio kuwa nayo mambo ambayo yamelalamikiwa na Dad Rajabu
⁠⁠⁠⁠
Haya mambo yameharibu taswira ya nchi yetu.⁠⁠⁠⁠ ⁠⁠⁠Vyombo vya habari vya kimataifa vinaandika kutekwa kwa binadamu na ⁠⁠⁠Tanzania imetajwa kama nchi inayogandamizwa haki za binadamu.
⁠⁠⁠⁠
Hujuma hizi hazikuviacha vyama vya siasa vilivyo makini. Wabunge kukamatwa na kufunguliwa mashtaka hasa viongozi wengi wa vyama hutishwa na kuwekwa ndani.

⁠⁠⁠⁠Katika njama za kudhoofisha upinzania, Chama cha CUF wanamtumia Lipumba.

Hii ni baada ya kuona CUF HAIYUMBI.

⁠⁠⁠CUF kimejipambanua kuwatetea wanyonge. Kwa upande wa Zanzibar kila mtu anajua kwamba zaidi ya nusu ya wazanzibar wanatuunga mkono. Uchaguzi wa 2015 unadhihirisha hilo.

⁠⁠⁠⁠Walitumia nguvu za kijeshi na kumtumia Jecha kuyapindua matokeo ya uchaguzi lakini bado wananchi wa Zanzibar wanaiunga mkono CUF ndo maana watawala wanatishika hivyo wakaamua kumtumia CUF.

Njama hizi zimeanza wakati Lipumba alivyokaribishwa ikulu mwaka jana. Nyote mnakumbuka sinema ya Lipumba baada ya ziara yake ya ikulu. ⁠⁠⁠Alianza kwa kutushawishi kukubali kurudia uchaguzi wa Zanzibar eti nitaendelea kuwa Makamu wa Rais.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠Alivamia vikao vya chama, alimtumia msajili wa vyama, alivamia ofisi za chama, alitengua viongozi wa chama wakati yeye si mwanachama
⁠⁠⁠⁠
Tokea Mutungi amejipa mamlaka asiyokuwa nayo ya kumtambua Lipumba, kuna hujuma zinaendela kufanyika ambazo ni:-
⁠⁠⁠⁠
1. Kutumia vyombo vya dola kumzua Maalim Seif kufanya siasa bara huku Lipumba akiruhusiwa
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠2. Lipumba ameteka na kuvamia ofisi za chama za wilaya mbalimbali chini ya ulinzi wa dola. ⁠⁠⁠Leo amevamia ofisi za Vingunguti kavunja milango
⁠⁠⁠⁠
3. Kuiba fedha za chama zaidi ya mil 300 NMB

⁠⁠⁠4. Njama za kumuengua Maalim Seif

⁠⁠⁠5. Bunge kupokea wabunge feki wa Bunge la EAC. ⁠⁠⁠Mnyaa hajapitishwa na chama wala kupitishwa na Katibu na alishafukuzwa uwanachama na tawi lake la Mkanyageni
⁠⁠⁠⁠
Haya yote yanafanya kupitia taasisi za umma kama Msajili wa Vyama vya Siasa, Hazina, Polisi na hivi sasa Bunge.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Yote haya ni kunyanyasa Maalim Seif kisa tu alishinda urais. ⁠⁠⁠⁠Na hii ni kwa sababu UKAWA unautisha utawala wa CCM.

⁠⁠⁠⁠Njama za kuitumia RITA kuhitimisha mpango wao zimeonekana. Sasa dola imeamuru kuitumia Wakala wa Udhamini na Ufilisi ili kuiangamiza CUF.
⁠Bodi ya wadhamini imechukua hatua madhubutui za kukilinda chama kupitia mahakama, sasa dola inataka kukitoa hiki kikwazo.

⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Tunazo taarifa kwamba RITA wanataka kusajili majina feki ya bodi ya udhamini ili kuiua bodi iliyopo. Nimepata taarifa kesho kuna kikao maalum cha RITA kuwataka asajili Bodi ya Lipumba na Jumanne itangazwe.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Kwa taarifa, Bodi ya wadhamini ilishasajiliwa tangu 1993. Tunachofanya ni kubadilisha wajumbe. CUF kupitia uongozi wa kitaifa, imefanya mabadiliko machache ya wadhamini na kuwashirikisha RITA na kupokelewa na kupata risiti.

⁠⁠⁠Sasa na Lipumba ametakiwa apeleke majina yake. ⁠⁠⁠Wanaitaka hii Bodi ili iweze kufuta kesi zote dhidi ya Lipumba. Lengo la pili ni kufungua account mpya ya CUF na wanadhani kwa hili wataweza kuwa wameidhibiti CUF.
⁠⁠⁠⁠
Wanajidanganya kwamba ushindi alioupata Seif Zanzibar utakuwa umeishia hapo na wanajiaminisha kwamba wakifanikiwa hilo CUF itasambaratika.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Msajili wa Vyama vya Siasa ndiye anayeshinikiza RITA wasajili bodi hiyo.

Ujumbe wetu na mwelekeo wetu
⁠⁠⁠⁠

⁠⁠⁠⁠CUF ni taasisi imara na imepita misukosuko mingi kufikia hapa. Nawaambia watawala walio nyuma ya huu msukosuko kwamba tutavuka salama. Zile zama za watawala kusema peke yao na kuwatisha watu zimeshapita na hazitarudi tena.

Huu ni wakati wa Tanzania kusimama pamoja na kulinda demokrasia yetu.

MASWALI

WhatsApp Image 2017-04-09 at 12.29.10.jpeg


⁠⁠⁠⁠SWALI 1: ⁠⁠⁠Umeongea kwa hisia sana, tunapenda kujua. Umeeleza hujuma nyingi. Endapo RITA watafanya hicho kinachotaka kutokea, nini mtafanya?
⁠⁠⁠⁠
JIBU: ⁠⁠⁠Kama rita wataisajili hiyo bodi ya Lipumba watakuwa wanakiuka sheria yao wenyewe sababu Bodi ipo tangu 1993 na tunacho cheti cha kusajiliwa. ⁠⁠⁠Bodi haifi watu ndo wanabadilishwa tu. ⁠⁠⁠Kama itasajiliwa huyo Afisa Msajili ajue atakuwa anavunja sheria, sio wafuate maelekezo tu bila kuangalia sheria inasema nini. ⁠⁠⁠Kama atamtambua Lipumba, litakalotokea watawala watabeba dhamana.

Ni kweli sisi tumekuwa wapole na ndo uungwana, sisi tunatunza amani. Tungetaka machafuko yangeshatokea, wanaotunza amani ni CUF sio vyombo vya dola. Huwezi kuua watanzania wote, mtamtia ndani Maalim Seif lakini wapo wengi sana. Wapo wengi ambao wananilaumu kwamba nawachelewesha. Mimi nawabembeleza nikitegemea upande wa pili wataona hilo, sisi tunafanya wajibu wetu na wao watafanya wajibu wao.

SWALI 2: Kuhusu fedha za Ruzuku zaidi ya Mil 300, tunaweza kupata documment za mchakato mzima ulivyofanyika tujiridhishe?

JIBU: Kwa utaratibu ambao unajulikana,Hazina inapewa ruzuku kupitia kwa Msajili wa vyama vya siasa. ⁠⁠⁠Katiba ya CUF ipo wazi kwamba dhamana ya mali zote zipo kwa Katibu Mkuu. Msajili wa vyama vya siasa alituandikia makatibu wakuu wote kila chama kifungue account moja ya kuingiza ruzuku tu. Na bodi iliniletea account nikampelekea msajili.

Msajili tangu mwezi wa nane hatupi ruzuku. Nikamuuliza kwanini ruzuku hatupatii? Akasema nimezuia ruzuku yenu kwa sababu mna mgogoro, mgogoro ukiisha nitawapatia.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Magdalena Sakaya na Lipumba walipewa mil369 sio kwenye account ya bodi wa wadhamini, hela iliweka kwenye account ya wilaya ya Temeke. Wale watia saini wa Temeke wakafukuzwa wakaletwa wa Buguruni na siku ile ile wakina Sakaya wakazitoa wakaziweka kwenye account ya mtu binafsi ya Mhina Omary wa Handeni. ⁠⁠⁠Hela zote na benk haishituki. Na siku ya pili hela zote zikatolewa, huoni hapo kuna mchezo? Tumewaandikia barua kuwachallenge NMB kwanini wamefanya hivyo, hawajajibu. Mimi sihusiki na pesa hizo na nimewaandikia hazina.
⁠⁠⁠⁠
Kulikuwa na njama nyingine walitaka kufungua account Lipumba na Msajili kwenye bank nyingine tatu tukapata taarifa tukablock. ⁠⁠⁠Msajili anajua Katiba za chama na NMB hawezi kujitetea. Ndio maana wanataka kusajili Bodi ya wadhamini RITA ili haya mambo yafutwe. Sisi ndo maana tukakimbilia mahakamani. Watu wameokotwa ADC leo wanataka kupewa bodi.

SWALI 3: Sasa hivi kuna CUF ya Lipunba na CUF ya Maalim, hamuoni kurudisha kwa wanachama hili swala? Ulikuwa unamanisha nini msitusukume kwenye ukuta? Serikali za mitaa zinakaribia mna mpango gani? Lipumba alisema Katibu asipotokea ofisini ana mamlaka ya kumteua mtu mwingine. Unasemaje kwa hilo?

JIBU: ⁠⁠⁠Kama unafikiri kuna CUF Lipumba na CUF Seif hilo sio sahihi. CUF ni moja, ⁠⁠⁠hakuna CUF Bara wala CUF Zanzibar. Ina Baraza Kuu moja na Mkutano Mkuu mmoja. Kilichotokea hapa kuna mtu na kikundi chake wameasi chama na wameshachukuliwa hatua na vyombo vya chama vya kumchukulia hatua.

Aug 21 Mkutano Mkuu uliidhinisha kujiuzulu kwa Prof. Lipumba. Alifanya fujo Buguruni CUF ikamfukuza uanachama, kabla ya hapo alikuwa mwanachama wa kawaida. ⁠⁠⁠Alishafukuzwa, nikae na Lipumba kufanya nini? Sio mwanachama wetu. Mimi ni Katibu Mkuu, kazi yangu ni kutunza kumbukumbu za vikao, sina uwezo wa kubadilisha maamuzi ya vikao vikubwa vya chama. Hii inaweza pelekea kukiuka maamuzi ya vikao
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Kutusukuma ukutani ina maana gani, tumefanyiwa mabaya mengi tumevumilia. Leo RITA wahodhi makao makuu. Vijana hawatavumilia nami sitaweza kuwazuia.

⁠⁠⁠⁠Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 tutakuwa tushaumaliza mgogoro huu. Chama kinachotoka kwenye mgogoro huwa kinakuja juu sana.

Hivi ni kweli Katibu Mkuu ameshindwa kufanya shughuli zake? Ninyi hamuoni shughuli hizi? Nafanya pamoja na polisi kunizuia. Nikimaliza Zanzibar nafanya ziara Dar es Salaam. Sio nmeshindwa kufanya kazi zangu, polisi wananizuia. Buguruni niende kufanya nini? Pale kuna wahuni, kuingia Buguruni ni kuwaunga mkono wahuni. Lipumba kaingizwa na polisi, si Mwenyekiti si Mwanachama. Hata angekuwa ni Mwenyekiti wa kweli hana mamlaka wa kunivua nafasi yangu. ⁠⁠⁠Baraza Kuu la taifa ndo wanaweza kunisimamisha sio Mwenyekiti, ⁠⁠⁠nasimamishwa na kikao sio mtu.

Jambo la ajabu ni huyu msajili. Eti watu tunaamua mambo bila kuwasikiliza, leo amenihukumu bila kunisikiliza. Mimi sijashindwa kazi, naendelea na kazi na mimi ndio Katibu Mkuu. Hadi nisimamishwe na Baraza Kuu halali au nifukuzwe na mkutano mkuu halali.
⁠⁠⁠⁠

SWALI 4: Katika awamu hii kumekuwa na malalamiko kwamba dola imekuwa ikiingilia mahakama na bunge, je mnategemea mahakamani mtaipata haki?
⁠⁠⁠⁠Ulikuwa unasema hatima ya CUF ipo mikononi mwa msajili, unasemaje?

JIBU: ⁠Mahakama pamoja na shinikizo, kuna mifano imetokea hivi karibuni. Angalieni kesi ya TLS, serikali ilisema haitaki lakini Mahakama za Dodoma na Dar wakaruhusu mkutano uendelee. Tutapeleka ushahidi na kumbukumbu, hawa wengine Lipumba kapata wapi?

Tulisema swala hili lipo mikononi mwa msajili. Wakati ule niliandikiwa barua kwamba nilipata malalamiko haya, chama kinasemaje? Nikamjibu nikampelekea. Sisi tulidhani kwa sababu ana uzoefu wa Mahakama Kuu atafanya mambo kisheria.

⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Sheria namba tano ya 1992, ⁠⁠⁠imetaja majukumu ya msajili
⁠⁠⁠⁠1. Kusajili chama.

2. Kufuta chama.

3. Kutunza kumbukumbu za vyama.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Hakuna sehemu inamruhusu kuingilia vikao halali vya chama. ⁠⁠⁠Kuna kesi kubwa haijaamuliwa wao wanaendelea. Wanataka RITA iwasaidie kwasababu wanajua hawana uwezo wa kushinda katika kesi hizo. Huyu wa RITA akifuata sheria tutashukuru, hatutaki kumuingilia.

MWISHO
 
Propesa lipumb atajificha leo, ngoja aumbuliwe

Maalim ni Tapeli la Kisiasa la karne hii kuwahi kutokea Barani Africa!

kila Siku anawadanganya Wapemba wenzie eti soon atapewa Urais wake wa Zanzibar lakin sasa yupo Busy kutetea Ukatibu Mkuu wake uliosimamishwa na Prof Lipumba!

Hatogombea Tena Urais wa Zanzibar kupitia CUF Hilo mnatakiwa mtambue Wafuasi wake
 
Ivi hebu tujiulize kati ya

Maalim Seif
Na

Lipumba

Nani tapeli? Tutumie akili ya kawaida tena ambayo ni bashite kabisa tuwaangalie hao watu wawili.

Tapeli ni alieteuliwa na CCM kuwa Kiongozi wa Serikal inayoongozwa na CCM na kutekeleza Ilani ya CCM huku akijifanya mwana kindaki ndaki wa CUF
 
Maalim ni Tapeli la Kisiasa la karne hii kuwahi kutokea Barani Africa!

kila Siku anawadanganya Wapemba wenzie eti soon atapewa Urais wake wa Zanzibar lakin sasa yupo Busy kutetea Ukatibu Mkuu wake uliosimamishwa na Prof Lipumba!

Hatogombea Tena Urais wa Zanzibar kupitia CUF Hilo mnatakiwa mtambue Wafuasi wake

Sawa mvurugaji wa vyama vya siasa.
 
Maalim ni Tapeli la Kisiasa la karne hii kuwahi kutokea Barani Africa!

kila Siku anawadanganya Wapemba wenzie eti soon atapewa Urais wake wa Zanzibar lakin sasa yupo Busy kutetea Ukatibu Mkuu wake uliosimamishwa na Prof Lipumba!

Hatogombea Tena Urais wa Zanzibar kupitia CUF Hilo mnatakiwa mtambue Wafuasi wake
nenda kavute bangi mzee
 
Maalim ni Tapeli la Kisiasa la karne hii kuwahi kutokea Barani Africa!

kila Siku anawadanganya Wapemba wenzie eti soon atapewa Urais wake wa Zanzibar lakin sasa yupo Busy kutetea Ukatibu Mkuu wake uliosimamishwa na Prof Lipumba!

Hatogombea Tena Urais wa Zanzibar kupitia CUF Hilo mnatakiwa mtambue Wafuasi wake
Shushia na juice ya Malimao
We Mdada siku hizi unaongea pumba sana umekua kama lile pandikizi lenu.
 
Kuna watu hakika akili au ubongo upo makalioni, lipumba na maalim tapeli nani hasa? Hivi kumbe mlikuwa mnstudanganya et lipumba ni msomi eti anafundisha uchumi marekani, msomi gani mpuuzi kiasi chake? Kujiuzulu na kurudi cuf kwa mabavu ni moja ya ukosefu wa akili, hivi huu uprofesa wa kipindi kipi? Na profesa mwingine kule eti alidai uteuzi wa maprofesa na madaktari haupo sahihi, Leo kateuliwa amesahau kama aliongea au alisemewa.
 
Back
Top Bottom