Hivi "Young" ni sawa na "Yanga"?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,573
2,000
Yanga imetokana na Young?, Kwanini "Young" ya Kiingereza haikuwa "Vijana" kwa Kiswahili?

Yanga ni kitu gani? Ni kukosea? Ni kutokujua? Ni sahihi kuita timu ya Dar es Salaam Young Afrika kwa jina la YANGA?
 
TEAM B-13

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
1,536
2,000
Yanga imetokana na Young?, Kwanini "Young" ya Kiingereza haikuwa "Vijana" kwa Kiswahili?

Yanga ni kitu gani? Ni kukosea? Ni kutokujua? Ni sahihi kuita timu ya Dar es Salaam Young Afrika kwa jina la YANGA?
Yanga daima mbele nyuma mwiko
 
MGILEADI

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,626
2,000
Barca sio jina rasmi tofauti na Yanga
Dar Young Africans ndiyo jina rasmi sio hili la Yanga. Ni sawa na the Blues, the Gunners, the Reds, Cosmo kwa iliyokuwa Cosmospolitans. Ilianza kwa sababu wapenzi hawakuweza kutamka kwa ufasaha Young Africans wakawa wanasema Yanga Afrika. Umekataa Barca kwa Barcelona bure tu. Hata simba ilipokuwa Sunderland tuliita "Sanda." Vitabu vya hiyo Yanga yako hata Klabuni ubao sharti uandikwe Dar Young Africans. Zamani akina Mshindo Mkeyenge, Abdul Masoud walikuwa wakitangaza mpira Yanga walikuwa wakiita Dar Young Africans. "Wasikilizaji mpira unapigwa kuelekea goli la Dar Young Africans!!!" Muulize mwanachama wa "Yanga" yoyote kwa msajili jina gani limeandikwa. Kama ni Yanga basi wamebadili majuzi tu.
 
kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,573
2,000
Dar Young Africans ndiyo jina rasmi sio hili la Yanga. Ni sawa na the Blues, the Gunners, the Reds, Cosmo kwa iliyokuwa Cosmospolitans. Ilianza kwa sababu wapenzi hawakuweza kutamka kwa ufasaha Young Africans wakawa wanasema Yanga Afrika. Umekataa Barca kwa Barcelona bure tu. Hata simba ilipokuwa Sunderland tuliita "Sanda." Vitabu vya hiyo Yanga yako hata Klabuni ubao sharti uandikwe Dar Young Africans. Zamani akina Mshindo Mkeyenge, Abdul Masoud walikuwa wakitangaza mpira Yanga walikuwa wakiita Dar Younng Africans. "Wasikilizaji mpira unapigwa kuelekea goli la Dar Young Africans!!!" Muulize mwanachama wa "Yanga" yoyote kwa msaijli jina gani limeandikwa. Kama ni Yanga basi wamebadili majuzi tu.
Mifano yako kama barca, the blues, the gunners haifani na Yanga kwa Young, ni heri wangeita greens, yellows, au vijana. Maana Yanga sio sio kifupi cha Young na wala sio Vijana. Yanga ni jina ambalo halina maana yoyote. The blues kwakuwa jezi yao ni Rangi ya blue, the gunners wanatunza ghala la silaha, Barca ni kifupi cha Barcelona, Yanga ni nini?
 
MGILEADI

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,626
2,000
Mifano yako kama barca, the blues, the gunners haifani na Yanga kwa Young, ni heri wangeita greens, yellows, au vijana. Maana Yanga sio sio kifupi cha Young na wala sio Vijana. Yanga ni jina ambalo halina maana yoyote. The blues kwakuwa jezi yao ni Rangi ya blue, the gunners wanatunza ghala la silaha, Barca ni kifupi cha Barcelona, Yanga ni nini?
Barca ina maana gani? Dar in maana gani: Ama Ronaldinho kwa Ronaldo ina maana Gani? Ama Jair kwa Jairzinho ina maana gani? Unajua nickname wewe? Nimetumia mifano ile ili uelewe nini kinachoendelea hapo. Watumie Greens wao Waingereza?

Barca kwa Barcelona inalink kwa jina hilo tu. Katika Espagnol halina maana yoyote nje ya Barcelona. Ndivyo ilivyo Yanga. Maana yake inlink kwa jina Young tu. Ukikuta majina kama Ernestito utalaumu watu wewe kwa nini hamumuiti Ernesti!

Kwa kuongezea, miaka hiyo timu hizi mbili Young Africans na Sunderland zilijipa miji. Yanga wakachukua Kuala Lumpur, Malaysia na Sunderland wakajitwalia Abidjan, Ivory Coast. Sunderland wakishinda utasikia mashabiki wakishangilia; "Abidjan oyeee! Lumpa ziiii!".Young Africans wakishindia utasikia "Lumpa oyeee! Abidjan ziiii!" Lumpa ikawa jinsi walivyoutamka na kuandika mji wao Kuala Lumpur. Sunderland waliwaita Young Africans kiutani "Makuala hao" kutokana na jina la Kuala Lumpur ama "Lumpa". Mashabiki wakiulizana hata shuleni tuliposoma:"Wee timu gani bwana?" Mtu alijibu ama Lumpa ama Abidjan".

Linganisha na Cavaliers wa NBA huitwa "Cavs"; Juventus na "Juve", Paul Gascoigne na "Gazza", Ramadhani na "Rama", Bakari na "Beka". Kwa mfano tu. Khalikh na "Likky". Juve ina maana gani? Likky ina maana gani? Cavs ina maana gani? Gazza ina maana gani? Au kwa sababu Waswahili wamejipatia nickname yao wewe hutaki kuelewa mpaka iwe Barca ndiyo nikname? Yanga ni nickname ya Young. Wameswahilisha Young. Wako sawa tu.
 
MGILEADI

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,626
2,000
Ni sawa na lile soko la marikiti Zanzibar,wenyeji walishindwa kutamka market wakawa wanaita marikiti ndio mpaka leo ikawa ni soko la marikiti.!! Yanga ni matamshi ya kuitaja Young ndio ikazaa jina Yanga.
Sawa kabisa. Ndiyo maana kuna mapinduzi makubwa sana ulimwenguni ya kitamaduni kurejea asili. Toka Burma hadi Myanmar, toka Peking hadi Beijing, Toka Bombay hadi Mumbai. Yanga sasa limekuwa Jina linalokubalika hata wakiamua kufuta Dar Young Africans wakaandika Yanga kwa Msajili rukhsa. Akiambiwa Cosmospolitans walijulikana kama Cosmo zamani atabisha tu.
 
The Icebreaker

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
5,330
2,000
Sawa kabisa. Ndiyo maana kuna mapinduzi makubwa sana ulimwenguni ya kitamaduni kurejea asili. Toka Burma hadi Myanmar, toka Peking hadi Beijing, Toka Bombay hadi Mumbai. Yanga sasa limekuwa Jina linalokubalika hata wakiamua kufuta Dar Young Africans wakaandika Yanga kwa Msajili rukhsa. Akiambiwa Cosmospolitans walijulikana kama Cosmo zamani atabisha tu.
Nisawa na jina KARIAKOO lilipatikana kwa wenyeji kutamka CARRIER CORPS,ndio ikawa Kariakoo mpaka leo,sasa mleta mada iko siku atauliza nini maana ya Kariakoo?!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom