Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
Leo nilikuwa matembezini mjini, maana mshahara wa December sikununua hata lipstick, ulikabwa na mahitaji ya shule. Ninapumua mwezi huu, niliamua kisafisha macho kwenye department store mjini Mlimani City.
Alikuja shost kuniomba ushauri, alikuwa na handbags mbili mkononi aliomba ushauri kama ingekuwa mimi ningependa ipi. Mimi nilimjibu inategemea na matumizi, basi shost aliniambia ni ya bint wake wa miaka 19 ambae yuko chuo kikuu mwaka wa kwanza.
Aliniambia mtoto huyu anakaa nyumbani, asubuhi huamka saa kumi kuhakikisha chai ya wadogo zake iko tayari. Si mtu wa tamaa , chochote unachomnunulia atavaa, ukimpa laki tatu leo baada ya miezi mitatu atakwambia bado ninayo ninaitumia taratibu. Sasa kwa furaha mama anataka binti huyu nae awe lady.
Nilijiuliza wenzetu wanaleaje?