Hivi watendaji wa dawasco ni machizi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi watendaji wa dawasco ni machizi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mchajikobe, Sep 6, 2009.

 1. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,364
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Hii imenifanya niamini kuwa hapa Tanzania hakuna umuhimu wa elimu,sababu wengi waliobarikiwa kuipata hawaitumii matokeo yake wanayoyafanya ni aibu na dharau kwa taifa kwaujumla.Embu fikirieni wana JF katika mitaa ya kinondoni kuna baadhi ya watu walikuwa wanauza maji kwa watu wa mikokoteni,baada ya kampeni ya DAWASCO ya kutupatia maji wakazi wote wa jijini,kweli maji tuliyapata na tulishukuru kwa hilo,lakini kinachoshangaza ni kwamba hawa DAWSCO badala ya kuwadhibiti hawa wanaouza maji bila vibali,walichokifanya ki kukatisha huduma ya maji kwa wananchi wote wa maeneo haya,sasa huu kama sio ukichaa ni nini?Wanatakiwa wajue kuwa watu wanalipia ankara zao hivyo wanastahili huduma hii!!
   
 2. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  hao mnawachekea inatakiwa wao wakikata maji nyie mnang'oa hadi mipira/mabomba yao yote
   
 3. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Dawasco mimi nadhani wanahitaji kuelimishwa zaidi kuwa mishahara yao inatokana na bill tunazolipa! Sioni kwa nini wakate maji ili watu wasilipe bill tena wakati wao ndo chanzo cha matatizo maana kwa akili yao wamefunga mita lakini kwa UZEMBE wao hawazisomi. Wanakadria vitu ambavyo havipo, eti bill ya mwezi laki!!! DAWASCO amkeni kwenye usingizi, hii karne ya 21! Ohoo!
   
 4. P

  Preacher JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nilidhani ni baadhi ya WATZ wanapata hili tatizo - DAWASCO wanakadiria mno bill zao hivi alternative nyingine ya maji ni ipi?? haya maji ya kununua kwenye malorry ni salama?? naomba ushauri kwani estimation ya zaidi ya 50,000 kwa maji usiyotumia ni WIZI MTUPU
   
 5. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dawasco hamna wasomi kuna vishoka tu,wataalamu hupelekwa wizarani na manispaa.

  "our lives begin to end the day we become silent about things that matter"
   
 6. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Inawezekana kupata maji mazuri kabisa:
  1. Kuvuna maji ya mvua, kuya-treat na kuyahifadhi mwaka mzima - gharama zaidi hapa ni za kuhifadhi
  2. Kuchimba kisima na ku-pump. Lazima upate wataalamu wa-assess eneo lako kama lina maji na kama yanafaa kwa matumizi ya binadamu. Waone wizara ya maji pale ubungo.
   
 7. S

  Sendeu Member

  #7
  Sep 7, 2009
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dawasco ni kichefuchefu jamani ebu wajiulize kwa nini kimara kuna tabu ya maji ilhal maji yanapitia huko kuja mjin??? AIBU KUBWA wamefukia mabomba bila maji jaman
   
 8. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2009
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Miaka nenda rudi hawa DAWASCO sijui wanakula na walanguzi wa maji. Mfano kule Masaki maji hayajawahi kupatikana tangu enzi. Yale malori yanayoleta maji huenda dawasco wanayo hisa. Utakuta vijana binafsi wana miundo mbinu yao ya kuwapa watu maji wanaokubaliana nao. Inakuwaje vijana hawa wawe na uwezo wa kuleta maji ilhali shirika kubwa kama Dawasco wanashindwa? Hizi ni njama au ufisadi fulani?
   
 9. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkuu kwa sheria za mipango miji na hata kiafya huruhusiwi kuchimba kisima mijini!
   
Loading...