Sisi watanzania tutakuwa na matatizo sana jamani
Tuna matatizo kibao yanaendelea nchi mwetu lakini cha ajabu ni kuwa
kwanza ni wepesi wa kusahau mambo, ukiuliza hapa mambo ya majina ya wauza unga na majambazi aliyosema President anayo na akaahidi kuwashugulikia, utashangaa, watu wameshasahau
Sasa leo hii tunaambiwa kuwa Balali amekufa, na nyie mnaamini na kuanza kutoa pole
Kuna vielezo vyovyote vinavyoonyesha kuwa balali amakufa? tusipende kusimamia kwenye kauli bila vigezo jamani, na ndio maana hata hawa jamaa wanatuona wajinga, mkipelekwa hivi mnaenda tu, sasa amchelewi kuambiwa kuwa Jeet patel naye kafa!!!
Pili hakuna haja ya kutoa pole (kama kafa kweli)kwa mtu kama balali, au ndio nyie mnajifanya kumpenda mtu akisha kuwa marehemu, kwani yeye kasababisha vifo vya watu wengine?
Tuwe tunakasumba ya kupenda kutumia vigezo katika kufanya na kuamua mambo jamani, la sivyo tutaendelea kuwa (ndivyo tulivyo siku zote)