Hivi Watanzania tukoje jamani?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Watanzania tukoje jamani??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BabaH, May 21, 2008.

 1. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sisi watanzania tutakuwa na matatizo sana jamani
  Tuna matatizo kibao yanaendelea nchi mwetu lakini cha ajabu ni kuwa
  kwanza ni wepesi wa kusahau mambo, ukiuliza hapa mambo ya majina ya wauza unga na majambazi aliyosema President anayo na akaahidi kuwashugulikia, utashangaa, watu wameshasahau

  Sasa leo hii tunaambiwa kuwa Balali amekufa, na nyie mnaamini na kuanza kutoa pole

  Kuna vielezo vyovyote vinavyoonyesha kuwa balali amakufa? tusipende kusimamia kwenye kauli bila vigezo jamani, na ndio maana hata hawa jamaa wanatuona wajinga, mkipelekwa hivi mnaenda tu, sasa amchelewi kuambiwa kuwa Jeet patel naye kafa!!!

  Pili hakuna haja ya kutoa pole (kama kafa kweli)kwa mtu kama balali, au ndio nyie mnajifanya kumpenda mtu akisha kuwa marehemu, kwani yeye kasababisha vifo vya watu wengine?


  Tuwe tunakasumba ya kupenda kutumia vigezo katika kufanya na kuamua mambo jamani, la sivyo tutaendelea kuwa (ndivyo tulivyo siku zote)
   
 2. S

  Sra Member

  #2
  May 21, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Inaonekana bado una malue lue ya usingizi mkuu, inakupasa uendele kulala km huitaji kutoa matongo tongo na kuona vizuri
   
 3. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tumia busara zako,
  kama kuna typing error unaitaji kusema tu,na sio kutoa lugha chafu wewe!! tukitoleana lugha chafu wote hapa si tutageuza maana halisi ya JF?

  Soma welcome notes then kisha act kutokana na instruction hizo, najua sio kosa lako, ugeni wako na ukutaka kusoma sheria za jamvi.

  Karibu sana, pole pole lakini
   
 4. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Baba H,

  Kweli jamaa (Sra) ana jazba, na si vema kuripuka kama kifuu cha nazi, anaposema maneno ya kejeli kama haya inafaa akuombe msamaha,lakini tupe data vipi umemuona huko Balali hadi useme tunadanganywa? Na ni kweli sisi watz asili yetu ni kuamini hata kama hatujaona , sasa kama umemuona huko muipue
   
 5. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hilo ndilo swali ndugu
  Concept ni hii binadamu anaendelea kuishi mpaka pale atakapokufa, na hili swala la kufa linaitaji vielelezo vya kutuakikishia kuwa huyu binadamu kafa.
  Sasa basi mimi ninaamini kuwa balali yu mzima, lakini aliyesema Balali kafa ndiye anatakiwa kutuwekea vielelezo vya kifo na si vinginevyo ndugu

  Nadhani hapo umenipata ndugu
   
 6. t

  tibwilitibwili Senior Member

  #6
  May 21, 2008
  Joined: Sep 12, 2006
  Messages: 181
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Baba H nakubaliana nawe.Wewe ni mtu makini sana hapa na mtu na kuanza kukuvaa hatutakubali .Kama kachoka anaweza kondoka .Kuna blog za wahuni anaweza kwenda huyu mtu huko kuna mfaa .
   
 7. K

  Kalalangambo Member

  #7
  May 21, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ''Kuna vielezo vyovyote vinavyoonyesha kuwa balali amakufa?''

  Kwanza Naungana na 'Baba H'. Hatutaamini mpaka tuthibitishiwe kweli kafa. Wewe unayekejeli maoni ya wenzako usitake kubadili maana na mwelekeo wa mada hii.

  Watanzania tunalipuka kama mlima 'Olodonyongai' then tunasahau kabisa. Kabla sijasema ninalotaka kusema nisije nikasahau, kweli kama amekufa, wakati wa mazishi kuna kusoma CV ya marehemu. Sasa tutahitaji pia kusikia kwamba' Marehemu alikuwa fisadi namba moja kama sio mbili' na alipendelea sana Watanzania waendelee kuwa masikini wa kutupwa katika dunia hii. Kama watasema alikuwa muadilifu itabidi kwanza waushawishi umma wa watanzania.

  Nilikuwa nataka kusema kwamba kama jamaa kafa (sio kufariki, wanaofariki ni wenye utu na wanaojali wengine), kuna mambo mengi yanayozunguka kifo chake; First, Mafisadi wenzake huenda wamemuua kupoteza ushahidi. Second, kajinyonga. third, yupo ila wanatufanya wajinga kama jamaa alivyosema ili tuamini na kumuacha aendelee kutesa na fedha za watanzania huko ughaibuni.

  Kufa sote tutakufa, lakini ni mazingira gani utakayofia. Kama ukifa jamii yote inalia kwa uliyoyafanya sijui kama huko kwa God utanusa pua yako. Fikiria kitendo cha kupoteza (kuiba) mabilioni, matatizo ni yepi? first, Huduma muhimu hazikununuliwa kama za afya na hivyo maisha ya akina mama wajawazito na watoto yamepotea. Second, Huduma za elimu hazikupatikana hivyo kwa kipindi chake huyo mfu amezalisha vihiyo kibao. third, Huduma za barabara ni hovyo yaani mashimo tupu, ajali zimeua wengi na hayo naendelea kumtwika huyo fisadi. Achilia mbali Huduma kibao ambazo zingeboresha kama hizo bilioni zisingechukuliwa.

  Haya wakulaumu, midomo ni yenu endeleeni. Wakusahau maovu tunayofanyiwa na hao jamaa vichwa ni vyenu endeleeni kusahau tu. Wenye kukejeli, kwanza hao ndio sitawajali kabisa nitawaita makopo na bendera fuata upepo.

  Mwisho, wasilete maiti waliyofanyia surgery na wakamwita balali. Balali is stil existing and is not dead. I will agree his death until is proved beyond reasobale doubt.
  ------------------------------------------------------------------------------
  MOYO KABLA YA SIRAHA
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,818
  Likes Received: 83,217
  Trophy Points: 280
  Babah, mimi baada ya kuitafakari hii habari ya kufa kwa Ballali sasa naamini kwamba hii habari ina walakini. Ballali pamoja na familia yake wana uwezo mkubwa wa kuusafirisha mwili wa marehemu kwa sala na kuagwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wazazi wake ambao nasikia wako hai.

  Hivyo sioni sababu zozote za Ballali kuzikwa kinyemela US, halafu pia inadaiwa kwamba amekufa muda kidogo uliopita. Hivyo nina wasiwasi na ukweli wa habari hii, zaidi linalofanyika hapa ni kumpatia huyu jamaa jina jipya na vitambulisho vyenye jina jipya ili aendelee kuishi maisha ya raha na asiwajibike tena kutoa ushahidi kuhusiana na wizi mkubwa wa mabilioni ya shilingi plaw BoTunaowahusisha viongozi wa juu wa sirikali katika awamu ya tatu na ya nne.
   
 9. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Babah, mimi baada ya kuitafakari hii habari ya kufa kwa Ballali sasa naamini kwamba hii habari ina walakini. Ballali pamoja na familia yake wana uwezo mkubwa wa kuusafirisha mwili wa marehemu kwa sala na kuagwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wazazi wake ambao nasikia wako hai.

  Hivyo sioni sababu zozote za Ballali kuzikwa kinyemela US, halafu pia inadaiwa kwamba amekufa muda kidogo uliopita. Hivyo nina wasiwasi na ukweli wa habari hii, zaidi linalofanyika hapa ni kumpatia huyu jamaa jina jipya na vitambulisho vyenye jina jipya ili aendelee kuishi maisha ya raha na asiwajibike tena kutoa ushahidi kuhusiana na wizi mkubwa wa mabilioni ya shilingi plaw BoTunaowahusisha viongozi wa juu wa sirikali katika awamu ya tatu na ya nne


  Ni kweli unayosema ....hata kama si ndugu wenye uwezo, Serikali inaweza kusaidia kwa kusafirisha mwili....si alikuwa mtanzania. Mara nyingi tunaona watu wakiomba michango kwa ajili ya jukumu hilo pia kwenye blog mbalimbali za watanzania. Inaonekana kuna namna namna kwenye hili suala ........
   
Loading...