Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,932
Leo katika taarifa ya habari ya Star TV ya saa mbili usiku nimemuona Mwigulu Nchemba akihutubia wananchi akikaripia kuhusu kukwepa kodi na hasa zaidi misamaha ya kodi. Kilichonishangaza zaidi ni pale aliposema hawezi kukubali kuona watu wachache wanakaa Dodoma na kuamua kutoa misamaha ya kodi wakati wananchi hawana maendeleo.
Nilishangaa kwani serikali hiyo hiyo ya ccm ndiyo inayokaa Dodoma na kutoa misamaha ya kodi, na wala si serikali nyingine yeyote ile. Je huku ni kuhadaa wananchi kwamba wao ccm ni tofauti na serikali? Au wanadhani kwamba Wananchi ni mbumbumbu kiasi ambacho hawajui kwamba serikali ndio inayoendeshwa na ccm?
Siku hizi za karibuni tumekuwa tukiwasikia kina Nape, Kinana na Mwigulu wakilaumu watendaje wa serikali kwa kazi zao mbovu, kana kwamba watendaje hao ni wa serikali ya chama tofauti. Kwa mawazo yangu, huu ni mkakati wa kuwahadaa wananchi ili wafikirie kuwa ccm inawajali sana. Vilevile, ni mkakati wa kuwanyima maneno washindani wao kwa vile hayo ndiyo maneno wanayowaambia wananchi dhidi ya serikali ya ccm.
Hata hivyo, mkakati huu hautafanikiwa kwa sababu moja kubwa. Wananchi si wajinga kiasi hicho. Wanatambua fika kuwa ccm ndio chanzo cha machungu yao, na hata kama watalia na kutoa machozi katika majukwaa, hayo ni machozi ya mamba tu.
Ni wakati sasa umefika kwa washindani kuwaelimisha wananchi juu ya unafiki huu mkubwa unaofanywa na ccm kupitia kwa Nape, Kinana na Mwigulu na wengineo. Ni unafiki mkubwa kwani wao ndio wanashikilia dola, na kama wangekuwa na uchungu na Wananchi wangeweza kabisa kuleta hayo mabadiliko kwenye serikali na si katika majukwaa.