Hivi wanawake wote wako namna hii au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi wanawake wote wako namna hii au?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Prince Nadheem, Jul 1, 2012.

 1. Prince Nadheem

  Prince Nadheem JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 1,026
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Habari za jumapili tulivu na nzuri kama hii wanajamii? natumai wote mko safi na mnaendelea vizuri na mapumziko yenu ya leo.
  leo mi nimekuja na jambo naomba kupata experience na maoni yenu juu ya hili naloenda kuliwasilisha jamvini.

  Tangu nimesnza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanawake hadi nafikia maamuzi ya kufunga ndoa kuna tabia moja nimekuwa nikikutana nayo constantly kwa wanawake takribani watatu ambao nimekuwa nao katika mahusiano ya serious. Naomba msininukuu vibaya jamani mimi ni miongoni mwa wale watu ambao napenda mahusiano ya kudumu na naheshimu sana hisia za watu hasa katika mahusiano ya kimapenzi.ngoja nitoe angalau profile fupi kwa kila mmoja ili twende pamoja.

  msichana wa kwanza kuanza nae uhusiano ilikuwa ni form 5 nikiwa Mbeya,huyu alikuwa ni binti wa kichaga,alikuwa hapendi kabisa hata nikae discussion na wasichana wengine pale shuleni na ilikuwa hata akiona nimesimama tu na binti mwingine huo moto utakaowashwa bwenini huo usiku bweni zima watajua na muda mwingi alikuwa bize kupopularize uhusiano kiasi kwamba shule nzima kuanzia walinzi hadi headmaster walikuwa wanajua kuwa we are lovers.kutokana na sababu fulani mwaka wa kwanza chuo kikuu tuliachana.

  Msichana wa pili ilikuwa ni wa mwaka wa kwanza pale chuoni yeye alikuwa mngoni na ilikuwa mwaka wa kwanza second semista ambae nilidumu nae hadi mwaka wa tatu na miezi tano tangu kuhitimu masomo nae vile vile tuliachana kwa sababu fulani.tukirudi katika tabia naen alikuwa hapendi kabisa mimi kuwa karibu na wasichana napia alikuwa anapenda muda wangu mwingi niwe natumia na yeye tu kiasi kwamba nilikuwa nakosa hata muda wa kuwa na jamaa zangu wa karibu na hata nikwa bize na computer kwa kazi za chuo au binfasi malalamiko yalikuwa hayaishi kuwa simjali,niktoka kwenda club na jamaa zangu ndio kabisaa kesi nzito yaani full malalamiko.

  huyu wa sasa mnyamwezi nae hana tofauti na hao wa juu na ni mwaka wa tatu tangu niingie nae kwa uhusiano na sasa tangu nijiunge na JF akiwepo tu uhuru wote wa kuingia JF unapotea maana malalamiko hayaishi,nikienda kwa jamaa zangu hataki maana nae kamaliza chuo kikuu wiki 2 zilizopita na sasa naishi nae,nikitaka hata kwenda kwa jamaa zangu somewhere around here Ukonga anaanza kulalamika,wakija wafanyakazi wenzangu hapa home nikiwasindikiza tu kwa umbali fulani ni tatizo.

  samahani kwa uzi mrefu ila ni katika kuwa muwazi zaidi juu ya hili,so mwisho kabisa nabaki na swali kuwa kwa nini wanawake wengi wako so much possessive?au na wanaume wengine wako hivyo?kama wako hivyo mi kuna kitu nakosea kupenda uhuru namna hiyo? wanawake kwanini baadhi yao hawajiamni?nifanyeje ili kuendana na hali? natanguliza shukurani kwa michango yenu
   
 2. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama tatizo ni wanawake kutojiamini, bali ni kila abiria anachunga mzigo wake. Vijana wenyewe wa siku hizi mmekuwa vicheche kupita kiasi, hamuaminiki kabisaaa.
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  hongera bro,madem wengi siku hizi ni ving'ang'anizi. Nothing else.
   
 4. Candy kisses

  Candy kisses JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 293
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mayb una elements flani flani zinazofanya wadada wawe possesive,mayb una mazoea na wanawake au sio muwazi etc.kama ni hvyo mtoe out evn if ukiwa na ur frnz,af muweke wazi hata kwa v2 vdogo vdogo atazoea tu
   
 5. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  duh! mwana wanawake watatu wote design hiyo hiyo....hapana hapa hamna coincidence labda kuna kitu abt u that keeps attracting such kind of women. alafu wewe nawe bana yaani umekaa nae miaka mitatu eti sasa ndio waja kuona ni kero. usually mara nyingi wanawake wanakuwa possessive becoz either wewe nae ni mcharuko or it myt be that u too gud a man to let go bana hahaha
   
 6. k

  kisukari JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  kufanya hivyo,ni kutojiamini.na ukiwa unamchelewesha,mara atajibebesha mimba.sielewi kwa nini lakini maisha ya kukaa pamoja kabla hamjaoana naona kama mtachokana,kabla ya ndoa yenyewe,utajiuliza sijamuoa,vurugu ndani.jee tukiwa katika ndoa itakuwaje?na ndoa ni looooong commitment
   
 7. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ndo kupendwa huko jamani upendwe vipi. mwenzio wanatamani hayo. ila kiukweli si kuwa wasichana ndo wanatabia iyo ila hiyo hali ipo kwa wasichana hdi wavualana inategemea na tabia ya mtu na kipimo cha wivu wake.
   
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,700
  Likes Received: 12,750
  Trophy Points: 280
  Ni jambo la kawaida kwa wanawake walio wengi.
   
 9. DERICK2000

  DERICK2000 JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  You mit have some behavior that makes them to see u in a bad way,thats why,they want to possess..jichunguze.
   
 10. Binti Magufuli

  Binti Magufuli JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 7,455
  Likes Received: 756
  Trophy Points: 280
  kwa ufupi nilichogundua since niingie JF (kulingana na mawazo ya wanaume walio wengi )ni wanaume wengi kutopenda mwanamke anayewa-possess too much. wengi utasikia hawapendi kuulizwa ulizwa uko wapi, unafanya nini, uko na nani, simu za kila dakika, na kero zingine za kuchungwa chungwa na kuonewa wivu. sijajua sababu ya wao kutopenda kuwa possessed ni coz wana ugube gube au nini ila hyo ndo observation yangu.

  kwa mantiki hii mimi ninazo hizo tabia zote za kuwa too possessive. nikitaka nimpate wa kumatch nae ni lazima niwe kama kondoo yani mengine nijifanye tu mjinga na kufoji kuwa na vitu ambavyo kiukweli sina
   
 11. T

  Talklicious Member

  #11
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mie siamini kuwa tatizo ni la hao wanawake ILA ni lako. Mana tangu umeanza kudate serious inaelekea unaangukia kwa hao hao. Swala ni kwamba hiyo ni type ya wanawake ambao moyo wako umewaridhia. Inawezekana ukiwa na peer na sababu ya kusakamwa na wenzio inakuwia vigumu kuwa na kauhuru ambao una wish. Lakini all in all hizo drama ndio zinakukeep la sivyo kuwa na wanawake wenye tabia nyingine utaboreka ndio mana labda wamekuwa casual girlfriends na hawa wa wivu kupindukia wamekuwa real girlfriends. My take, your love instinct is what draws you to such kind of women.
   
 12. felinda

  felinda JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 351
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  anayemuonea wivu mpenzi wake ndo mwenye mapenz ya dhati.,asiye na wivu hana mapenzi ya kwl!!
   
 13. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wanawake wenye wivu wapo na unaweza ukute hata hakupendi kihivo
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  kuna ka ukweli hapa.

   
 15. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,277
  Likes Received: 3,008
  Trophy Points: 280

  mmh ya kweli haya?
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Ngoja siku ukutane na ambae hayuko possessive, utajuuta! Sasa asipokupossess wewe akampossess babake ama?
   
 17. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Well said mydia, ukiona mwanaume hataki kuwa possesed ujue huyo ni GUBE GUBE!
   
 18. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ni kawaida sana hyo katika mahusiano kwani hata wewe ukiona anaongea na mwanaume mwingine huingiwi na ka wivu?
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Hutaki? Sasa mie mfano ntakuonea wivu wewe wa nini, na ili iweje?
   
 20. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  binafsi napenda sana mwanamke possessive! anti possessive ni kibaka, ni kama paka mwizi, au kunguru, wamawake wanaokosa tabia hiyo ni snake, wameniumiza sana, pumbavu sina ham nao
   
Loading...