fabinyo
JF-Expert Member
- Aug 5, 2011
- 2,991
- 2,109
Mimi ni mwanamke wa miaka 27, sijaolewa ila nina mchumba wangu amabye kashajitambulisha kwetu ametoa mahari na mwezi wa 10 mungu akipenda tutafunga ndoa. Mimi na mchumba wangu tuko vizuri, mimi nafanya kazi serikalini nayeye ni Mwanasheria, ananipenda, ananijali na kunihudumia kwa kila kitu. Lakini tatizo lake Kaka ni moja, yaani sijui kama ni mtu ambaye anafaa kwangua u ni mimi nakosea. Mchumba wangu ni mtu wa kunicontrol sana, sijui nisemeje lakini anataka kunisaidia kwa kila kitu.
Labda nikupe mfano Kaka ili unielewe, mchumba wangu anapenda nikipata shida nimuambie yeye ili anisaidie na si mtu mwingine. Kwa mfano labda nimeumwa na sina pesa, nikamuambia Dada yangu akanipa, akijua atakasirika kuwa namdharau eti kwanini sikumuambia yeye anipe, labda kodi ya nyumba imeisha nikaenda kukopa anakasirika kuwa kwanini namruka yeye naenda kukopa wakati yeye ana uwezo wa kunihudumia, hataki ndugu zangu wanisaidie kwa chochote anaona kama ninamdharau kwa kutokumuambia yeye matatiozo yangu.
Nikweli nikimuambia shida yoyote ananisaidia bila kinyongo wala nini, haninyanyasi lakini Kaka mimi nachoka nitamuambiaje mwanaume matatizo yangu kila siku. Sio kwamba hanipi pesa bila kumuomba, ananipa lakin tatizo lake nikuwa kwanini nikiwa na shida simuambii naenda kukopa au kuwaambia watu wengine. Mimi kaka wakati mwingine najisikia vibaya kumuambia kila kitu naona kama ataniona nina shida sana lakini nisiposema anakasirika, kaka naomba ushauri namna ya kuishi na mwanaume kama huyu kwani nampenda sana na yeye ananipenda.