Hivi wale maharamia wa Somalia waliishia wapi?

Hivi wale maharamia wa Somalia waliishia wapi?

Wakuu, naomba niishie hapo, nami nina damu ...

Kumbukeni tu kuwa:- Dunia ni nzuri sana lakini... Walimwengu Sisi ,,, ndiyo Wabaya.
Yaani unaongea pumba tupu na bila shaka kuna mlengo unaushabikia ambao mmekalilishwa USA ndio adui yenu. Mnaiombea njaa USA alafu mkipigwa marufuku msiendeko mnaanza kulialia.
 
To the level of my invisibility inanifanya nishindwe kuelewa baadhi ya nongwa, poise hebu nidadavulie japo tongotongo linipungue.
Ivi hawa wanavopandikiza hayo makundi mfano USA na France forces unity kama unavyosema, hii ya kuchukua hiyo uranium inaingia ingiaje na wanaichukua kwa namna gani? Kuwepo tu kwa hayo makundi kunatosha kusema kwamba mfaransa na mmarekani wabebe uranium na Serikali ya somalia ikabaki inaangalia tu kama cinema??
Tililika .........................................

livafan ,

Mkuu, hiyo kitu hata Poise, nilipokuwa mdogo kwenye hizo medani za fitina niliuliza kama wewe uulizavyo.

Hii dunia ina mbinu nyingi sana.

Kwanza, wao wana kuja kuomba kuchimba madini /kununua sasa katika makubaliano inakuwa hamna tatizo kabisa.

Ila wanaanza kuwa na tamaa ya kila mtu ayamiliki madini na pia, mapato kwenye nchi nayo mmiliki halisi inakuwa tatizo kila mtu anataka hela ziwe zake binafsi au kundi fulani.

Sasa wazungu wao wanachokifanya ni kuwaweka kati Yaani, wanaoongea na serikali kwa makubaliano yote kisha wao ao hao wanatengeneza kundi lao nalo wanalipa mbinu za kuvuruga amani kwa ujumla ya nchi.

Hivyo, serikali ya nchi ikaomba mwekezaji ambaye ni USA wakati ule aliyekubaliana kuchimba madini/ kununua. Kuwa USA iipe serikali ilivyo madarakani ulinzi na silaha ili amani irudi nao waendelee kuchimba madini.

Sasa hapo, ndipo walipoleta silaha wakazigawa makundi mawili yaani kwa ajili ya serikali Halali ya Somalia na zingine kundi la kigaidi.

Basi, wao wakaendelea kujichotea madini bila malipo maana serikali inapambana na magaidi.

Sasa USA akamwalika msela wake France ambaye awali aliitawala sehemu ya Somalia anaelewa figisu zote za huko.
Baadaye , Israel naye akatimba uwanjani. Ila sasa ujue kuwa wanachukua udongo processing inafanyikia kwenye base zao za kijeshi walizoziweka Afrika kwenye baadhi ya nchi.

Kwa hiyo, ukifika Somalia hakuna plant yoyote ya uranium processing unit.

Sasa, Iran akataka aingie rasmi kwa kuchimba na kuweka mitambo kabisa ndiyo akapigwa figisu na USA na vikwazo vizito kutoka Washington DC kipindi cha Obama mwanzoni mwa 2009 hadi 2013 kisha vikalegezwa baada ya Iran kujiondoa Somalia kwenye hiyo deal.

Na wakamchafua zaidi Iran kuwa anauziwa uranium na makundi ya al-shabab wakishirikuana na al-qeuda ila ilikuwa ni kuichafua Iran na kuiongezea vikwazo.

Kumbuka, Somalia ina depost ya uranium yakuweza kuendesha mitambo ya USA, France, UK, Russia , China na Iran kwa miaka 50 mfululizo.

Au Ulaya nchi zote kwa Karne moja ( miaka 100)

Mwisho, makundi ya kigaidi na majeshi yanapigana hizo nchi zenyewe zinabeba mizigo.
 
Yaani unaongea pumba tupu na bila shaka kuna mlengo unaushabikia ambao mmekalilishwa USA ndio adui yenu. Mnaiombea njaa USA alafu mkipigwa marufuku msiendeko mnaanza kulialia.

jiwe la maji ,.
Mkuu .
Niombe radhi kwanza.

Binafsi siyo mfuasi au muumini wa dini za kigeni zozote zile kutoka nje . Siko kwenye, Ukristo, Uislam, Hindu, Buddha, Judaism, Freemason and the likes siko huko wala Mimi siyo mganga na siamini katika uchawi.

Naamini katika sayansi , teknolojia na tafiti , zaidi katika kufanya kazi kwa bidii, kwa umakini na uamininifu.
Porojo za dini uchwara za kigeni sifanyi kabisa.

Labda nikuulize swali moja tu ,, Vita ya DR Congo ni kweli Congo imeshindwa kuimaliza au kuna jambo nyuma yake tofauti hiyo vita!?

Ukijibu hilo utaelewa pia USA, France na Somalia kinachoendelea huko.

Asante
 
Kama miaka 2 hivi iliyopita headlines katika vyombo vya habari ilikuwa juu ya maharamia waliokuwa wakiteka meli kila siku.

Siku hizi sisikii kabisa.

Tatizo lilikuwa nini? Na limetatuliwaje?
Ulinzi bahari ya Hindi kipande cha Somalia umeongeza vile vile siku hizi meli zinasafiri na wanajeshi na meli zinaruhusiwa kuwa na silaha.
 
Somalia wanalima mirungi. Ni kule southern Somalia (El Beru Hagia) bordering Kenya (Wajir)....I saw them harvesting it wakati nafanya kazi na UN kwenye makambi ya wakimbizi huko. This is home of the great Thinkers, tuna ushahidi.

Jamaa_Mbishi ,

Mkuu ni kweli Somalia wanalima mirungi sana tu.
Ila zao hilo ,Wasomali wanasema walilitoa Ethiopia na Yemen tena miaka ya 1900s.

Ila zao hilo lilianzia Yemen, 1854 hivi kisha likaletwa Ethiopia, baadae likasambaa Sasa kuja Somalia, Sudan, Kenya, Tanzania, Congo, Zimbabwe, Uganda, Malawi, Zambia, hadi South Africa.
Sasa hivi mirungi inauzwa dunia nzima.

Ila ukumbuke kuwa mirungi zamani haikuwa kilevi bali dawa ya kutibu baadhi ya magojwa hasa nchini Misri karne nyingi sana waliitumia kutibia.

Pia tambua kuwa mirungi inaliwa zaidi Somalia kwa sasa kwa sababu ya makundi hayo.ya kiuhalifu kuamini kuwa mirungi hukata usingizi hivyo wanaitafuna sana ili kuwa sober na kuendelea na mapambano.

Mfano, Kenya inauza mirungi tani 20 kila siku yenye thamani ya dollar 800,000 ( mirungi export's to Somalia its worth of $800,000 per day)
 
nchi inayoongoza kwa fitina US hili linajulikana sema tu ndo mfadhili wa mambo mengi ndo mana tunatulia ili tule na kipofu vizuri
 
nchi inayoongoza kwa fitina US hili linajulikana sema tu ndo mfadhili wa mambo mengi ndo mana tunatulia ili tule na kipofu vizuri

Maxmizer ,
Mkuu,

Kabisa ila mtu akisema au kuandika anaitwa kuwa ni uchochezi au ni wa mlengo Fulani wa upande gani sijui kama huyu member mwenye hii ID jiwe la maji , anavyonituhumu na kunisakama kuwa nimeandika kwa kufuata mlengo Fulani.

Ila huo ndiyo ukweli kuwa USA na European Union (EU) kuna nchi zinatuharibia dunia.
 
Sasa kama Usa Anashabikia haya mambo mbona kila tunashuhudia ndege zisizo na ruban zikiua viongozi kadhaa wa haya makundi na vile vile hawa hawa jamaa wakikamata mtu wa USA anakua halali yao.

Sidhani kama Mataifa ya nje yanamkono hapa kati ya mataifa ambayo Usa hata kuyasikia ni Somalia baada ya Makomandoo wake kadhaa kukamatwa na wengine kutembezwa mtaani wakiwa wamefungwa kwenye gari na kuburuzwa.

Sema tu Ulinzi umeimarika pwani ya Somalia

bryan2,

Mkuu,
Kwa macho ya Nyama na Kusikia na Kuona kwenye Media ni kweli ulichoandika.

Ila soma comments zangu zote utaelewa vizuri wanavyofanya kazi.

Ila kwa ufupi tu, elewa kuwa duniani pana figisu nyingi sana.

Mbaya zaidi , ni kuwa wafanya figisu ndiyo wanaorudi tena kama watuliza ghasia na wakombozi huku akilini mwao wanaelewa kabisa wanachokifanya .

Ila sisi huku , nje tunakuwa tunawashangilia kuwa ndiyo msaada ila ukweli ni kwamba dunia hii ni kizungumkuti , ikitokea ukaona hata robo tu ya mambo yanayopangwa gizani//kwa kificho ili yatekelezwe utalia.
 
Wakuu, nimewaletea Uzi wa huyu member mwezentu GuDume , ili mjifunze kuhusu namna ambavyo dunia inaendeshwa kwa kutumia "invisible hands " huku "visible hands" wakikupepea kwa feni usikie usingizi while, invisible hands wanakumaliza.


Sasa, baadhi mliuliza kuwa inakuwaje USA na French intelligence service unit waliweza kuleta matatizo huko Somalia!?

Majibu yake ukisoma huu Uzi namna ambavyo USA chini ya CIA na rais wao wa kipindi hicho Gorge H. Worker Bush miaka ya 1985- 1990s (Baba yake na Rais George Bush ) walivyoiangusha Jumuiya ya Kikumunisti (USSR) utaelewa kazi ya Invisible hands katika kutengeneza UFA na kubomoa na wakati huo visible hands wanakusaidia kuziba UFA.

Kwa hiyo Somalia inachafuliwa na USA, French intelligence service unit ili wajimilikishe uranium na madini mengine yaliyopo Somalia.

Baadhi nimewa-tag ili msome hizo mbinu na baadhi ya hujuma na fitina wanazozifanya wakitaka kukuharibia ili muone mfano mmoja wapo.

Kumbuka hapo ilikuwa fitina ya kuiua USSR ila hiyo fitina hii vile vile hutumika wakitaka kuchukua madini au kuleta machafuko kwenye nchi yoyote wanayotaka kufanya hivyo.

livafan , Crimea , bryan2 , jiwe la maji , 1974hrs, Maxmizer , hashim mwamba ,

Kuanguka Soviet Union, Uhusika wa CIA/Marekani ulichangia kupiga Msumali wa mwisho kwenye Jeneza

Mkuu, GuDume , nimequote Uzi wako huo hapo juu ili kuelezea kwa njia nyingine ambavyo wazungu koko wanafanya fitina ili kuharibu amani za nchi nyingine, au kuleta fujo ili wao wabebe madini kwa urahisi.

Kama ambavyo, machafuko na kuanzishwa kwa kikundi cha ugaidi (Al-Shabab) na maharamia wa nchini Somalia walivyotengenezwa na CIA, yaani USA na French Intelligence Service Unit ya Ufaransa.
 
Mkuu,
Tema mate chini na endelea kuombea amani Somalia na Pwani yote hiyo kuanzia Djibouti hadi Mozambique.

Ile issue, ilitengenezwa maabara ya kijasusi na CIA, France Intelligence service Unit ila hao jamaa (USA and France) waweze kuiba rasmali ya Somali ambayo ni Uranium.

sasa nchi zingine zilipogundua ile game nzima zikatoa taarifa mahala salama huko Duniani.

Basi, kijana, hapo ndipo CIA na French intelligence service unit wakaamua kubadilisha uelekeo na kuimalisha Al-Shabab na Al-Quard ndani ya Somalia ambao wana mipaka ndani ya Somalia tu kuendeleza zile fujo ili raslimali ziendelee kuchotwa.

Sasa, Kenya inatumika kama chambo pasipo kujijua maana, USA na France wanamsupport Alshababu huku ao hao wanampa bichwa Kenya kuwa wanampa vifaa na fedha za kupambana na al-shabab.

Huku, technically, Kenya anapigana na USA and French intelligence service unit indirectly kwa sababu wote wale ni mapandikizi wa hizo nchi mbili ili wao wachote uranium.

Ila kwa.kuangalia taarifa za habari na kusoma kwenye net watu wengi wanaelewa kuwa kuna al-shabab huko somalia na Kenya while its USA and French intelligence service unit ndizo zinafanya yao huko ili waweze kuchota uranium kiurahisi.

Kumbuka kwenye, history ya ukoloni barani Africa hiyo Somalia ilitawaliwa na kuonewa na France na Britain.
Kwa hiyo French anaendeleza koloni lake kwa njia ya vita ili aendelee kuchota Mali za uranium huku Britain akimwachia Mjomba wake USA afanye yake.

Dunia inaendeshwa na invisible hands while, visible hands unazoziona zikikusaidieni ni kwa ajili tu ya kukupakeni mafuta kwa migongo ya chupa ila huko nyuma ya pazia invisible hands wanakutoboa moyo na mbavu.
Nilitegemea kuona uzi kma huu,Sjui CIA,Mara rasilimali,..Kila kutu lazima usa ahusike.
 
SirChief ,

Haya siyo maneno matupu bali hawa USA, CIA ni wachawi "white witchcrafts"

Mfano, soma hii ya CIA, USA under George H. Worker Bush na USSR.
Utaelewa kuwa ni wezi, wanafiki , wafitini na wauaji.

A thread by GuDume ,


Kuanguka Soviet Union, Uhusika wa CIA/Marekani ulichangia kupiga Msumali wa mwisho kwenye Jeneza
Ni sawa nakubali kwamba hawa mabepari wana njia nyingi za kujipatia mali,Lakini kusema tuu kwamba CIA wanahusika bila kuweka ushahidi haileti maana sana.
Kwani kuteka meli ya mizigo kuna kazi gani mpaka pirates washindwe kufanya wenyewe?.Mimi naamini binadamu yeyote anauwezo wa kufanya lolote anapopatwa na tatizo,wasomali pia baada ya kukosa ajira na jinsi ya kuendesha familia zao,wazo hili liliwajia na wakalichukua kama fursa.Njia walizokuwa wanatumia kuteka meli ni local sana,haihitaji technolojia ya namna yeyote,just ku sacrifice tu.Any thing is possible ukiwa na challenge.
 
Ni sawa nakubali kwamba hawa mabepari wana njia nyingi za kujipatia mali,Lakini kusema tuu kwamba CIA wanahusika bila kuweka ushahidi haileti maana sana.
Kwani kuteka meli ya mizigo kuna kazi gani mpaka pirates washindwe kufanya wenyewe?.Mimi naamini binadamu yeyote anauwezo wa kufanya lolote anapopatwa na tatizo,wasomali pia baada ya kukosa ajira na jinsi ya kuendesha familia zao,wazo hili liliwajia na wakalichukua kama fursa.Njia walizokuwa wanatumia kuteka meli ni local sana,haihitaji technolojia ya namna yeyote,just ku sacrifice tu.Any thing is possible ukiwa na challenge.

OK,

Ndiyo maana nikaandika vizuri kabisa kwenye comments zangu kuwa ; Kwenye msafara wa mamba huwa kenge hawakosekani. Nao huunga.

USA/ CIA na France secret agents walianzisha game kisha na hao maharamia fake nao wakaitumia fursa ile iliyotengenezwa.

Pia, kwenye Tasnia ya Ujasusi ukisubiria nikuwekee hapa ushahidi zaidi ya nilichokwisha kuandikia hapo awali wewe utakuwa ni Sawa na wewe unahitaji kwenda UK halafu unasubiria ndege huko Ubungo Bus Terminal.

Nilionesha kuwa hayo mambo yanapikwa kwenye labs za kijasusi, humo wanatoa pure road map to be followed during the missions though ; the approach to reach destination its always corrugated to avoid any trace of the mark in the field.
 
  • Thanks
Reactions: 30P
Back
Top Bottom