Hivi wale maharamia wa Somalia waliishia wapi?

Hivi wale maharamia wa Somalia waliishia wapi?

Crimea

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
26,840
Reaction score
38,930
Kama miaka 2 hivi iliyopita headlines katika vyombo vya habari ilikuwa juu ya maharamia waliokuwa wakiteka meli kila siku.

Siku hizi sisikii kabisa.

Tatizo lilikuwa nini? Na limetatuliwaje?
 
Patrol ship zilizidi sana hapo Somali waters so wameona bora watulie kwanza. Na pi tujue Mali zinazoibwa huko majini zipo Mombasa na majiji makubwa ya pwani ya EA ambapo hao wasomali wanafanya buashara sasa ukiangalia East Africa nzina haijatulia so wanaweza kuwa wanapima upepo
 
Mkuu,
Tema mate chini na endelea kuombea amani Somalia na Pwani yote hiyo kuanzia Djibouti hadi Mozambique.

Ile issue, ilitengenezwa maabara ya kijasusi na CIA, France Intelligence service Unit ila hao jamaa (USA and France) waweze kuiba rasmali ya Somali ambayo ni Uranium.

sasa nchi zingine zilipogundua ile game nzima zikatoa taarifa mahala salama huko Duniani.

Basi, kijana, hapo ndipo CIA na French intelligence service unit wakaamua kubadilisha uelekeo na kuimalisha Al-Shabab na Al-Quard ndani ya Somalia ambao wana mipaka ndani ya Somalia tu kuendeleza zile fujo ili raslimali ziendelee kuchotwa.

Sasa, Kenya inatumika kama chambo pasipo kujijua maana, USA na France wanamsupport Alshababu huku ao hao wanampa bichwa Kenya kuwa wanampa vifaa na fedha za kupambana na al-shabab.

Huku, technically, Kenya anapigana na USA and French intelligence service unit indirectly kwa sababu wote wale ni mapandikizi wa hizo nchi mbili ili wao wachote uranium.

Ila kwa.kuangalia taarifa za habari na kusoma kwenye net watu wengi wanaelewa kuwa kuna al-shabab huko somalia na Kenya while its USA and French intelligence service unit ndizo zinafanya yao huko ili waweze kuchota uranium kiurahisi.

Kumbuka kwenye, history ya ukoloni barani Africa hiyo Somalia ilitawaliwa na kuonewa na France na Britain.
Kwa hiyo French anaendeleza koloni lake kwa njia ya vita ili aendelee kuchota Mali za uranium huku Britain akimwachia Mjomba wake USA afanye yake.

Dunia inaendeshwa na invisible hands while, visible hands unazoziona zikikusaidieni ni kwa ajili tu ya kukupakeni mafuta kwa migongo ya chupa ila huko nyuma ya pazia invisible hands wanakutoboa moyo na mbavu.
 
mkuu James Comey amedokeza vizuri na uhalisia japo sheria za mitandao zinatubana kuongeaongea mambo haya ila juu juu tu, wapo waliowekeza kwenye majiji makubwa haswa Mombasa, pia wapo walioamua kuacha ila wapo waliojiwa juu na wazee wa kimila wa kisomali wakatiwa neno likawaingia wakaach mfano mmoja wapo ni tolu,,,,,,,, naishia hapa
 
Japo, sasa baada ya hali kuwa vile huko somalia ndiyo wakajitokeza na vikundi vya kiharamia navyo vikatumia ule usemi wa kuwa kwenye msafara wa mamba kenge nao wamo.

Sasa, hawa vikundu vya kiuharamia viliacha hiyo game ila ni baada ya USA na French intelligence service unit kuingiza tena mkono wao kuwaondoa vikundi vyao (vikundi vilivyokuwa financed na USA na France).

Hivyo, na vile vikundi vilivyojianzisha kwa mgongo wa fujo zile nao wakaondoka maana, nguvu ilikuwa kubwa ya kuwaondoa.

Lakini kwa ujumla, hii dunia haiko kama unavyoona mambo yanatangazwa kwenye vyombo vya habari au kusoma kwenye net.

Ikitokea , labda siku moja ukafunuliwa, na kuona yanayofanywa na serikali za mataifa makubwa (invisible hands) nakuhakikishia hutakaa umuamini kamwe Mzungu koko wala kucheka naye.
 
Kama miaka 2 hivi iliyopita headlines katika vyombo vya habari ilikuwa juu ya maharamia waliokuwa wakiteka meli kila siku.

Siku hizi sisikii kabisa.

Tatizo lilikuwa nini? Na limetatuliwaje?


Siku hizi meli nyingi hazipiti ukanda ule, hivyo hawana hela. Wao kwa sasa wako wanalima mirungi tu na kuwasubiri wabongo wajinga wanaokwenda kujiunga nao kwa kujivalisha mabomu mwilini.
 
Wakuu, naomba niishie hapo, nami nina damu ...

Kumbukeni tu kuwa:- Dunia ni nzuri sana lakini... Walimwengu Sisi ,,, ndiyo Wabaya.
 
Siku hizi meli nyingi hazipiti ukanda ule, hivyo hawana hela. Wao kwa sasa wako wanalima mirungi tu na kuwasubiri wabongo wajinga wanaokwenda kujiunga nao kwa kujivalisha mabomu mwilini.
Somalia hawalimi mirungi, hujui ulichokiandika.
 
Somalia hawalimi mirungi, hujui ulichokiandika.


Somalia wanalima mirungi. Ni kule southern Somalia (El Beru Hagia) bordering Kenya (Wajir)....I saw them harvesting it wakati nafanya kazi na UN kwenye makambi ya wakimbizi huko. This is home of the great Thinkers, tuna ushahidi.
 
game changer wakubwa wameibadilisha hapo

ze-dudu ,

Hicho ndicho wanachokifanya mara zote.

Vita yoyote ile.hapa duniani haijatokea tu kwa sababu imetokea zote zinawaanzilisha.

Na ambao ni hao mbwa koko wa huko duniani.

Angalia, vita za kugawana makoloni nchi zilizotawaliwa, vita mbili za dunia (WW 1 & WW 2) vita za wenyewe kwa wenyewe kwenye nchi mbalimbali, vita za kigaidi zote, vita za kuondoa serikali za nchi zingine hapa duniani hasa middle east na baadhi ya nchi za Afrika na huko Latin America.

Hivi karibuni hii, vita inayoanzishwa huko peninsula ya China, north Korea//south Korea kote huko ni hao mbwa koko ndiyo waanzilishi.

Halafu, madhara yake Afrika tunabebeshwa.

Any way, we need to open up our eyes and brains in order to clean up this mess and shits from our land and lives.
 
Japo, sasa baada ya hali kuwa vile huko somalia ndiyo wakajitokeza na vikundi vya kiharamia navyo vikatumia ule usemi wa kuwa kwenye msafara wa mamba kenge nao wamo.

Sasa, hawa vikundu vya kiuharamia viliacha hiyo game ila ni baada ya USA na French intelligence service unit kuingiza tena mkono wao kuwaondoa vikundi vyao (vikundi vilivyokuwa financed na USA na France).

Hivyo, na vile vikundi vilivyojianzisha kwa mgongo wa fujo zile nao wakaondoka maana, nguvu ilikuwa kubwa ya kuwaondoa.

Lakini kwa ujumla, hii dunia haiko kama unavyoona mambo yanatangazwa kwenye vyombo vya habari au kusoma kwenye net.

Ikitokea , labda siku moja ukafunuliwa, na kuona yanayofanywa na serikali za mataifa makubwa (invisible hands) nakuhakikishia hutakaa umuamini kamwe Mzungu koko wala kucheka naye.
To the level of my invisibility inanifanya nishindwe kuelewa baadhi ya nongwa, poise hebu nidadavulie japo tongotongo linipungue.
Ivi hawa wanavopandikiza hayo makundi mfano USA na France forces unity kama unavyosema, hii ya kuchukua hiyo uranium inaingia ingiaje na wanaichukua kwa namna gani? Kuwepo tu kwa hayo makundi kunatosha kusema kwamba mfaransa na mmarekani wabebe uranium na Serikali ya somalia ikabaki inaangalia tu kama cinema??
Tililika .........................................
 
Sasa kama Usa Anashabikia haya mambo mbona kila tunashuhudia ndege zisizo na ruban zikiua viongozi kadhaa wa haya makundi na vile vile hawa hawa jamaa wakikamata mtu wa USA anakua halali yao.

Sidhani kama Mataifa ya nje yanamkono hapa kati ya mataifa ambayo Usa hata kuyasikia ni Somalia baada ya Makomandoo wake kadhaa kukamatwa na wengine kutembezwa mtaani wakiwa wamefungwa kwenye gari na kuburuzwa.

Sema tu Ulinzi umeimarika pwani ya Somalia
 
Back
Top Bottom