Hivi vyote hana, JK aliupataje Urais?

Usisahau udini. Wako watu wengi ambao wanaamini kuwa yote yanayompata Kikwete kutopendwa ni kutokana na dini yake. Kwa hali hiyo waislam wengi wakiongozwa na maneno na hoja za viongozi wao walikuwa nyuma ya nguvu ya kiislam kumtetea Kikwete. Wakumbuke kuwa hata Mkapa alipofanya madudu aliandamwa na shutma bila kujali dini yake. Pia uwepo wa Slaa na uambukizo kuwa yuko kwa ajiji ya Wakatoliki umechangia Waislam kumtetea na kumpa kura Kikwete.

kwenye udini sio hoja ya msingi kwa sababu ni kweli udini ulitawala baadhi ya maeneo sio kwa kikwete tu bali hata kwa slaa na akina zito. Rejea kauli ya zitto kuhusu udini wakati wa uchaguzi.
 
Yule Gbagbo wa kule Ivory Coast aliupataje? Nadhani Kikwete aliupata kwa namna inayofanana na Gbagbo. Kule Ivory Coast Kamati ya Katiba ilimpa ushindi wakati Tume ya uchaguzi ilikuwa imeonyesha kuwa Gbagbo kashindwa. Kwetu Tanzania kwa vile Tume ya uchaguzi ilikuwa sambamba na Kikwete waliamua kumpa moja kwa moja bila kumumunya maneno.
 
Back
Top Bottom