mambo_safi
Senior Member
- Jul 22, 2019
- 181
- 446
Hivi si ni viazi vitamu kila mahali vipo na tunavijua! Tunataka hiyo chakula mdau kaongelea anayejua utunagabalishe!Mbona vipo kibao tu Bukoba hadi Dar unavipata Sinza Mori kwa Kazaura. Sema siku hizi vimekuwa si vingi km kipindi cha nyuma.
Mimi leo nimetoa e'bitakuri anga e'mfuma.
Mkoa gani huo? Ni kawaida wengi tukienda nyumbani asili tulikotokea lazima to loose weight (tukonde) kutokana na kukosa dishes za kitown town hivi! Hahahah! Pole sana!Kuna mkoa nilienda mwaka jana,ni Tabutupu !!!kila siku asubuhi wanaenda shamba wanaleta vitu fulani vigumuuuuu vinachemshwa na magimbi....japo sikukaa hata wiki lakini nililose some weight ndani ya huo muda mchache tu
Tatizo vyakula vingi vya asili sio vitamu,viendelee kupotea hivyo hivyo asee
Mkoa gani huo? Ni kawaida wengi tukienda nyumbani asili tuliktokea lazima to loose weight (tukonde) kutokana na kukosa dishes za kitown town hivi! Hahahah! Pole sana!
Ulienda ukweni nini? HahahahMkoa fulani hivi nikitaja hapa nitaharibu,yani ni tabu kweli kweli upande wa vyakula nilishindwa kuzoea kabisaaa
Ulienda ukweni nini? Hahahah
Nimezaliwa na kulelewa Bukoba mpaka nilipoanza kidato cha kwanza ndo kama nilihama mkoa wangu mpaka sasa umri unasoma kula chumvi nyingi.
Tangu miaka hiyo sijawahi kukutana na vyakula hivi vya asili kwa majina ya kihaya vinaitwa:
"Amakongo"
"Ebira"
"Ebira ebilikweera"
"Amasoma"
"Enumbu"
AMAKONGO ni jamii kama mihogo vile lakini yenyewe ni mviringo na mmea wake unatambaa chini au juu kama utapata mahali pa kujishikiza. Ukiyapika yanakuwa magumu kiasi kwamba ukiwa unayatafuna yanalia kama muhogo mbichi.
EBIRA: vyenyewe ni vikubwa kama papai jamii ya mihogo na mmea wake unatambaa chini au juu kama utapata mahali pa kujishikiza. Ukiyapika yanakuwa malaini na yanakuwa na rangi rangi fulani hivi.
EBIRA Ebilikwela ni jamii moja ya Ebira isipokuwa hivi ni vyeupee na vinanukia nukia vizuri saana ukivipika mtaa wa pili lazima wanuse
AMASOMA tofauti na jamii hizo tatu juu ambazo ukulia ardhini jamii hii utokeza kwenye mmea juu ya ardhi na mmea huu utambaa ardhini au juu ya ardhi ukipata pa kujishikiza
ENUMBU ni jamii kama tangawizi mwonekano na kuzaliana kwake lakini zenyewe nyeupe na zikipikwa msosi mmoja matata.
Ebu wajuzi na wenyeji wa Bukoba tuelimishe tafadhari!
Shida siku hizi tunapenda vyakula vitamu vyenye sukari nyingi ndio maana magonjwa ya sukari na figo yameshamili. Mungu alikua na maana kuumba vyakula visivyo na sukari nyingi. Na mara nyingi vyakula visivyo na sukari ni dawa.Kuna mkoa nilienda mwaka jana,ni Tabutupu !!!kila siku asubuhi wanaenda shamba wanaleta vitu fulani vigumuuuuu vinachemshwa na magimbi....japo sikukaa hata wiki lakini nililose some weight ndani ya huo muda mchache tu
Tatizo vyakula vingi vya asili sio vitamu,viendelee kupotea hivyo hivyo asee
Shida siku hizi tunapenda vyakula vitamu vyenye sukari nyingi ndio maana magonjwa ya sukari na figo yameshamili. Mungu alikua na maana kuumba vyakula visivyo na sukari nyingi. Na mara nyingi vyakula visivyo na sukari ni dawa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Zinafananaje? Kama unakapicha tutupie!Enumbu isijekuwa ndo numbu hizi za mbeya ni mbaya hasa mdomoni ila kabila la wasafwa wanazipenda balaa