Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,492
- 4,770
1)kwa tofauti kuona,kufikiri ni maono.
Siyo ya kakakuona,kwenye mila malumbano.
Ama macho yenye kona,yasiyo na shirikiano.
Ukidhani vile hivi,sivyo ndivyo udhanivyo.
2)jiti kavu japo fimbo,hata bichi nalo gogo.
Tone ziwa la urimbo,ndege ona kwa kisogo.
Japo lingu nao wimbo,ila kucheza mzigo.
Ukidhani vile hivi,sivyo ndivyp udhanivyo.
3)kipofu nae aona,mbali kama mwenye macho.
Kesho leo hata jana,hata bila ya kificho.
Tena bila ya kutuna,kusema kile ambacho.

4)kinyonga kama hatua,polepole mwendo wake.
Kama ndege akitua,humbeba nyuma yake.
Nyama kwenda kumlia,awapa vikinda vyake.

5)udhanivyo hivyo siyo,lakini iwe lakini.
Hata iwe sivyo ndiyo,wachoma mwiba wa tini.
Kwa yote yale yaliyo, ngoja ujue ni nini.

Shairi:HIVI VILE
0765382386