Hivi vibwengo kweli vipo?

New finding, of coz with hypothesis
Vibwengo = Wajumbe wa bunge la Katiba excluding UKAWA!
 
Umenikumbusha O Level boarding school.

Kuna mabweni ambayo, wanafunzi walikuwa wanadai kuwa vibwengo walikuwa wanaingia humo na kuwachapa vibao.

Wengine waliokuwa wanaogopa hata kutoka nje usiku kama kwenda chooni kwa kuogopa kukutana na vibwengo.

Kwenye bweni langu kuna jamaa alitoka nje usiku kujisadia akarudi nduki huku akipiga kelele kuwa vibwengo vilikuwa vinamfukuza.

Mie sijawahi kukutana navyo; kuna siku tulitoroka na washkaji wakati tunarudi usiku tukakutana na "vidude" fulani tukaamua kukomaa navyo, kumbe vilikuwa vitoto vya nguruwe. Shuleni kwetu tulikuwa tunafuga nguruwe.

Siku hizi wapo baadhi ya "watumishi wa Mungu" huwa wanaombea siyo tuu mapepo bali pia vibwengo na dudumizi.
 
Waliosoma Jitegemee(Jiteute) enzi za Massawe watakumbuka jinsi vibwengo vilivyokuwa vinasumbua baadhi ya watu.
Kuna jamaa mmoja alikuwa hawezi lala mwenyewe lazima aombe mtu alale nae coz alikuwa anasumbuliwa sna na hv vibwana.
Kwenda chooni mwenyewe usiku mbinde lazima uombe kusindizwa.
Tisa kumi kuna njemba moja ilikuwa baunsa imepanda hewani halafu ni mbavu nene kishenzi.Alikuwa akisema/kukutuma kitu lazima uache mambo yko utekeleze anachokuagiza.Siku moja aliamka kama saa tisa usiku kwenda class kupiga msuli.Akapitia kwanza bombani anawe uso kuondoa wenge la usingizi.Alipoanza kuinama ili afungue maji alipigwa bonge la kelbu ya mgongoni,akasimama wima ila hakuona kitu;wkt anatafakari alistukia bonge la kelbu kisogoni;hapo ndo mbio kama za Usain bolt zilipoanza tukastukia mlango wa bweni upo chini huku njemba ikipiga mayowe kama kafukuzwa na simba.
Mwingine alistuka usingizini akaona kibwengo kimelala pembeni yke;akarusha ngumi ikatua ukutani.Hakuweza kufanya shughuli yoyote kwa mwezi mzima kwa maumivu aliyoyapata.
 

Mwingine alistuka usingizini akaona kibwengo kimelala pembeni yke;akarusha ngumi ikatua ukutani.Hakuweza kufanya shughuli yoyote kwa mwezi mzima kwa maumivu aliyoyapata.

Hahaha nmecheka sana hyo sentensi..

Kimsingi waTZ huwa hatuaminig mambo mpaka yatutokee,m nmewahi kusumbuliwa na vibwengo nilipokuwa nasoma HAPPY SKILFUL INTERNATIONAL SCHOOL,iliyopo tabata segerea..
Nilisumbuliwa sana kias kwamba usiku ukiingia tu napata hofu,had pale nilipo omba ruhusa shuleni na kurud nyumbn nikapelekwa kwa mganga tatzo likaisha kabsa..
 

nimecheka sana huku nikitengeneza stori picha hii kitu.
 

Hahahahahahahhhh....jamani nimecheka sana umeniua braza..!mwaka gani huo?
 
Jamani jamani jf kuna maneno aisei story za vibwengo ni hatari binafsi nasikiaga watu walikutana na vibwengo hasa watu waliosoma shule za pwani nasikiafa mbezi beach high school vibwengo vilikuwa vinawabwenga sana boys na girls.
 

Vibwengo ni aina Ya Majini wanaopenda kutembea usiku na Vijinga vya moto

haswa pembezoni mwa bahari ni kweli Mashetani hawa wapo hswa katika miji yenye Bahari kwamfano Mji ya

Dar,Tanga na Mtwara

wanapatikana kwa wingi Mashetani wa aina hiyo ya Vibwengo. Na haswa wakati wa usiku kandoni kandoni

mwa ufukweni mwa bahari

unaweza kuwaona wakati wa usiku mwingi ukiwa wewe ni mtembezi mwa ufukweni mwa bahari kwa wakati

huo ni Mashetani

wanaopenda sana kuwachezea Wavuvi wakati wa usiku baharini. Wavuvi wengi wanawajuwa hao Mashetani

wa Vibwengo ni wafanyaji wa

vituko vingi nyakati za usiku haswa ukiwa baharini au ufukweni mwa bahari wanakujia na kijinga cha moto

kukuchezea akili yako na wanapenda sana kuwachezea binadamu Nyamuleha jr
 
Last edited by a moderator:

Hahahahahh' dah mwana hyo stori ya njemba imenifanya nicheke hadi michoz imentoka' boading kulikua na vituko sana' jamaa alichezea kelbu za kutosha tuu
Hahah
 

Hahahahahah. Story za vibwengo zilikuwa zinachekesha. Yaani jinsi walivyokuwa wanasimulia waliokutana navyo ilikuwa kama inatisha vile lakini ilikuwa ni vunja mbavu.

Noma unakuta bonge la mtu, form two linapenda kuwachimba mkwara wa kufa mtu au kuwapiga form one halafu unatonywa kesho yake asubuhi eti lilitolewa nduki na vibwengo usiku wa jana. Mtu unatamani uliambie wee fisi tuu kaa kweli mwanaume mbona ulitolewa nduki na vibwengo lakini unaogopa kipigo.

Au eti unatonywa lijamaa "lilitembelewa" na vibwengo jana yake usiku. Yaani "msimu" wa vibwengo watu walikuwa wanalala huku wamevaa jeans mbili kwa kuogopa "kutembelewa" na vibwengo. Joto kaliiiiiii watu wamelala na jeans mbili kisa vibwengo. Walinzi wakizima taa tuu watu hao vitandani. Unakukumbua vitanda vya double decker eti kulala kitanda cha chini ilikuwa risky "kutembelewa" na vibwengo.

Kuna jamaa walikuwa wanadai kuwa kuna vibwengo vilikuwa vinaingia bwenini usiku vinatembea kuanzia mwanzo wa corridor mpaka mwisho na viatu vya skuna vile vya kike vikidunda kwa kwa kwa madaha bila kuonekana. Nahisi kama vile pamoja na "ukame" wooote, nanii za watu zilikuwa zinasinyaa fasta kila waliposikia midundo ya skuna ikikatisha corridor. lol

Msandawe Halisi nae anadai hakufanikiwa kuviona na kuhisi yalikuwa tuu mastori ya uongo. Lakini Frank Wanjiru anadai kuwa "wale waliosoma shule za Msingi kongwe miaka ya tisini kurudi nyuma,Temeke Pr School na Madenge Pr School hii mambo wanaelewa sana sababu ndio ilikuwa mazoea na desturi yetu ukiwahi shule mapema kukutana na vibwengo kwenye miti, darasani na vyooni. kitu ninachojiuliza tangu kuingia karne ya hii 21 haya mambo sijayasikia tena yakitokea Mashuleni zaidi ya mtindo wa siku hizi ya Wanafunzi kukumbwa na Mapepo karibu Shule nzima,sasa sijui yamebadilika na kuja na mbinu hii?"

Hata hivyo, wapo wanaodai vibwengo wapo mpaka kwenye karne hii. Mfano, Mshomba anasema "Waulize waliosoma Kirokomu pale Rombo miaka ya 2003 watakupa jibu maana kila siku ilikua ni vituko mara kwenye vyoo hadi kupelekea wanafunzi kwenda kujisaidia kwenye mto unaitwa kururu huko nako wanakutana navyo ilikua si mchezo".

Lameck Dunia nae anadai kuwa "vibwengo kweli walikuwepo hasa shule kama IYUNGA BOYZ TECHN SEC SCHOOL..MBEYA.. mi menyewe nshamuona kibwengo mwaka 2004 alikuwa toilet ilikuwa kama sa7 nimetoka kula gambe wikiendi ila kwa sku hzi cjawasikia tena hawa wadudu aka ndondocha."

Nae MR.NOMA anasema "jf raha sana,watu wanaomba mpaka picha za vibwengo. bas haya,mi nakumbuka tu mastory ya walinzi pale Kwiro sec,mahenge moro eti Usiku walikuwa wanasikia kengele na wakicheki parade gnd wanakuta vibwengo,na maticher wao."

Yaani hizi story nacheka hapa mpaka mbavu zinauma sasa. Zinanikumbusha mbali sana. Yaani nilikuwa nataka nione vibwengo wanafananaje, but I never saw a single one. Mara kukaja sijui popobawa sijui nao waliishia wapi. Siku hizi sana sana utasikia tuu wanafunzi wa shule fulani wamekumbwa na mapepo.
 
nimecheka sana huku nikitengeneza stori picha hii kitu.
fiksiman alishaandika kuhusiana na vibwengo vya JF:

 
Hahahahaah,,,,,,,hii thread imenivunja mbavu kwa kweli.

Binafsi sijawahi kutana na vituko vya hawa vibwengo zaidi ya kusikia tu stori zao vijiweni.
 

Nimecheka sana alfajiri hii daah fikiria hiyo ngumi ilivyo toka kwa hasira halafu ikakutana na ukuta ha ha ha full maumivu duuh.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…