Vibwengo vya JF members mi hoi!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vibwengo vya JF members mi hoi!!!

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by fiksiman, Apr 25, 2009.

 1. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Jamani sina nia ya kumtusi mtu ila tuache tabia ya kuweka picha zinazofanana na zeutamu....nimekuwa nikitalii kwenye thread mbalimbali lakini kikubwa si kupata maoni bali kuona namna wanaJF wanavyoshindana kuweka vibwengo kwenye profile picha zao. Kuna zingine zinamwelekeo wa kuwavunjia watu tena wazito heshima zao...kwa mfano nimekutana na picha ya komrade mugabe, bush, obama na wengine wakiwa katika mazingira tata.

  Cha kushangaza hata hao wanaojiita masenior na premiure wa JF nao ndo kabisa aibu tupu...kwa mfano kuna mdau mmoja kaweka picha nyani ana gitaa, njiwa anasoma kitabu yaani nisiseme mengi. Ila kiukweli inatoa burudani kusoma post huku kibwengo kikitia mbwembwe...siku nilijisahau na kuanza kufuta scree ya laptop yangu nikidhani kimdudu kinatembea kumbe picha ya mdau wa JF.

  Nimeonelea nitoe angalizo hili hasa kwa kile kilichotokea hivi karibuni kwenye ile blog chafu ya zeutamu....asiyeijua imekula kwake. JF ni jukwaa lenye heshima kubwa na kila anaetaka kuingia humu anajua kuwa ameingia kwenye ulimwengu mwingine yaani ukikosea unapewa adhabu na ukizubaa unakumbushwa sasa chonde chonde hili jamvi liendelee kuwa la heshima badala ya kutegana na picha zenu za ajabu ajabu..ooops nitaitoa ile ya kwangu pia..tehethehtehe
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ama kweli kuku mgeni akosi kamba mguuni, Kamanda jaribu kupita hapa upate taarifa zaidi kuhusu hilo.
   
 3. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Unalako jambo e antaka utuzulie huku
   
 4. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nafahamu sana rules za humu ndani ndo maana nikaileta hii thread huku kwenye matani kaka...pamoja na yote bado naamini si vema kuweka vibwengo vinavyoonyesha picha za watu wakiwa wamefanyiwa manipulation kwani zitaleta hoja nyingine..sijui moderator anazingatia nini nachojua huwezi kuweka picha ya mtu unless ni role model au ameridhia mwenyewe, zaidi ya hapo ni kuvunjiana heshima tu.
   
 5. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35

  Ha ha ha I thought I was the only one, it was funny though. I dont see no harm in it.
   
 6. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Ha ha ahaaaaaaaaaaaaa, mkuu nilikuwa sijasoma footnote yako teh teh imenifurahisha sanaaaaaaaaaaaaa.
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Nyani ana gitaa au njiwa akisoma kitabu kuna tatizo gani?

  Humu kuna watu wanajichukulia too serious, JF kuna characters za kila aina, na almuradi avatar haiko offensive clearly, in which case you will need to report them with details on an individual avatar basis, utakuwa unataka ku impose unnecessary censorship.

  Whats next? Utasema watu wanamkosea heshima Kikwete kwa sababu hawamuiti muheshimiwa rasi Kikwete?

  Hayo mambo ya kuja ku apply standards za gazeti la chama "Uhuru" au gazeti la kanisa katoliki la "Lengo" kwenye new media kama JF inarudisha nyuma freedom of speech.
   
 8. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nasema hivi kama wewe unaoraha mbona hujaweka ya kwako ituchekeshe? New media inamipaka sio kila eneo ni freedom of speech...kama maneno sema utakavyo lakini sio picha bwana mbona hao jamaa wa ze...nani hiii mliwapigia kelele. Mi nachosema tusivuke mipaka linapokuja suala la uhalisia na mimi sipeleki report kokote kila mtu anaintegrity yake humu ndani afteral sijasema ni vibaya kufanya hivyo ila inachekesha na kufurahisha. NDO MAANA YA UTANI JAMANI EEE!:)
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mimi napenda kuona watu wanaovaa T-Shirts zenye maneno ya kuchekesha, je hiyo ina maanisha ni lazima na mimi nivae T-Shirts zenye maneno ya kuchekesha?

  Wewe ni lazima ufanye kila kitu unachopenda kukiona?

  Lete malalamiko on a case by case basis, tuone kweli hii ina merit intervention, ama sivyo utaonekana puritanic inhibitionist tu, hatutaki unnecessary infringement on our freedoms hapa, lest you turn JF into some online Taliban republic, complete with some sharia like code of conduct.
   
Loading...