Hii nchi ni ya ajabu sana.....
Mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya siasa vya upinzani ambavyo ni haki yao ya kikatiba Mkulu kapiga stop.
Akina Halima Mdee na Esther Bulaya ambao wamefukuzwa bungeni kinyume kabisa na kanuni za Bunge. Mkulu kampongeza Spika Ndugai kwa kitendo chake hicho na akaahidi kuwa wabunge hao wa majimbo ya Kawe na Bunda hata wakiitisha mikutano kwenye majimbo yao atawashughulikia!
Lakini wananchi mbalimbali nchini ambao wanaandamana kwa ajili ya kumpongeza Rais wetu kwa kile wanachokiita ushujaa na uzalendo wake, ingawa maandamano hayo hayana vibali vya Polisi, lakini kwa kuwa tu yanamsifu Mkulu, ni ruksa kuandamana!
Hii nchi hivi sasa haiendeshwi tena kwa misingi ya Katiba yetu ya nchi na sheria nyingine mbalimbali, Bali inaendeshwa kwa namna mtu mmoja anavyotaka kuiendesha atakavyo!
Naanza kuyaamini maneno yaliyowahi kutamkwa na Rais mstaafu wa awamu ya 2 Mzee Ruksa, aliposema kuwa nchi yetu hivi sasa inaendeshwa kama gari bovu ambapo dereva wake hajui analipeleka wapi hilo Lori!