Hivi Vibali Vya Kuandamana Mmevitoa Wapi?

ZILLAHENDER MPEMA

JF-Expert Member
Apr 4, 2015
2,057
2,000
Wehu,wasio na Elimu na wote wanaofanana na hao ambao kwa mujibu wa utafiti wa TWAWEZA ndiyo wanaoiunga mkono ccm,hawahitaji kibali chochote,hao ukiwazuia unaweza kuwakuta wapo barabarani,acha tu waandamane kwa sababu ndiyo upeo wao unapoishia.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,509
2,000
Hii nchi ni ya ajabu sana.....

Mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya siasa vya upinzani ambavyo ni haki yao ya kikatiba Mkulu kapiga stop.

Akina Halima Mdee na Esther Bulaya ambao wamefukuzwa bungeni kinyume kabisa na kanuni za Bunge. Mkulu kampongeza Spika Ndugai kwa kitendo chake hicho na akaahidi kuwa wabunge hao wa majimbo ya Kawe na Bunda hata wakiitisha mikutano kwenye majimbo yao atawashughulikia!

Lakini wananchi mbalimbali nchini ambao wanaandamana kwa ajili ya kumpongeza Rais wetu kwa kile wanachokiita ushujaa na uzalendo wake, ingawa maandamano hayo hayana vibali vya Polisi, lakini kwa kuwa tu yanamsifu Mkulu, ni ruksa kuandamana!

Hii nchi hivi sasa haiendeshwi tena kwa misingi ya Katiba yetu ya nchi na sheria nyingine mbalimbali, Bali inaendeshwa kwa namna mtu mmoja anavyotaka kuiendesha atakavyo!

Naanza kuyaamini maneno yaliyowahi kutamkwa na Rais mstaafu wa awamu ya 2 Mzee Ruksa, aliposema kuwa nchi yetu hivi sasa inaendeshwa kama gari bovu ambapo dereva wake hajui analipeleka wapi hilo Lori!
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
22,566
2,000
Mimi nilivyo nafuraha nimeandamana kimya kimya kutoka kwangu mpaka kwenye uwanja wa uhuru peke yangu,niko bega kwa bega na raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania,hata kama tutavamiwa kijeshi nitaripoti jeshini haraka sana hata kama ni vita niko radhi damu yangu nyama yangu jasho langu mifupa yangu nivitoe kwa ajili ya nchi yangu.
 

dolevaby

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
10,889
2,000
Kila sehemu naona kuna vikundi vya watu na maandamano madogo madogo, hivi vibali wamevitoa wapi?
Mwanasiasa ni Mwanasiasa tu.. sikufikiri kama mtukufu nae angeingia kwenye mkumbo wakuzalisha Vikundi vya kumtukuza.... watu tulitegemea Kazi ndio imtukuze sio Vikundi pole kwa wanaotarajia Jipya!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom