Kama Makonda ameshapokea Kero kwa Wananchi wa Mikoa 20 na Ripoti ataiwasilisha kwa Rais Samia, kuna haja ya Chadema kuandamana?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,018
142,058
Hili ni swali tu kwa wale wanaohusika na Utoaji wa vibali vya Maandamano

Kama ni kero wote tumeshuhudia Makonda akizikusanya na kama ni sheria za Uchaguzi Chadema walishapeleka malalamiko yao UN

Sasa Wananchi waachwe wachape KAZI

Sabato Njema 😄
 
Waandamane tu kwasababu hata maandamano yao yanaratibiwa na CCM. Pia ni faida kwa serikali ya CCM kimataifa kwamba inaendesha nchi kidemokrasia. Maandamano ya CHADEMA yana faida zaidi kwa CCM.
 
Waandamane tu kwasababu hata maandamano yao yanaratibiwa na CCM. Pia ni faida kwa serikali ya CCM kimataifa kwamba inaendesha nchi kidemokrasia. Maandamano ya CHADEMA yana faida zaidi kwa CCM.
Mnapenda kuipa sifa za kijinga CCM . Hii CCM ambayo inaibia wanachi viwanja au hii ambayo serikali yake inateka watu. Punguza kuropoka
 
Mimi najiuliza swali dogo: kama Mwenyekiti wa CCM asingekuwa Rais ,Je kitendo Cha Makonda kupita mikoani kukusanya maoni kingekuwa na nguvu kama Sasa? Naomba wataalamu na wajuzi wanieleweshe
 
Makonda anashughurika na matatizo ya mwanainchi mmoja, mmoja
Lakini CHADEMA anashughurika na chanzo kinachosababisha matizo kwa wanainchi, Kwa ajili ya kizazi Cha Leo na Cha kesho.
Je nani ana thamani kwangu/kwako.?
Tunataka mifumo imara, ambayo haitegemei mtu mmoja. Leo makonda yuko anashughurika na kero na dhuruma zitokanazo na serikali ya ccm, je Leo akija mwenezi mwingine, izo keroo hazitarudi tena? Ndo iyo tabia ya Magufuri, ambayo sasa imebaki kwenye mioyo ya wachache, hususani waliowahi kupewa Malaki na maelfu Kwenye Kila dhiara ya Magu, Wala sio Kwa watanzania wote.
Makonda ni serikali hii hii ya ccm, Leo wa kijani, kesho atakua mwekundu, hatowafaa watu tena.
pia ikumbukwe kuwa, Pepo hatoi Pepo mwenzie.
Makonda ni kurejea Kwa ccm ile ile ya Miaka 60 huru, kumpokea makonda, hakika ni kudanganywa na pipi, tutafute katiba mpya, uchaguzi imara na makini, kuongozwa Kwa haki, Sheria na katiba, kupambana na rushwa, watumishi wa uma kusimama katika kuwatumikia raia.
MIMI NATAKA MIFUMO IBADIRIKE, WALA SIMTAKI MAKONDA.
Je ni wangapi wamepatiwa haki yao kweli, katika ziara ya Makonda????!!
Jamani ziara ya Makonda, naifananisha na uwepo wa kamchape Kigoma, rukwa, na tabora. Ni matatizo tu, hamna jipya.
Makonda wa watoto walioterekezwa dar, vip wale watoto wako wapi mpaka sasa?
Mchezo wa Makonda ni Dimbadimba, upumbafu tu, ila Kwa kuwa watanzania hatuna akili Wala maono, tutamfanya makonda awe Mungu wa watanzania hususani wajinga. Mie Simo kati yao.
Katiba mpya, bunge imara, mahakama zenye kutenda, jeshi la polisi lisilo na double standard, kuongozwa Kwa haki, kufuata katiba na Sheria, kupambana rushwa, maendeleo ya kweli yenye athari ya moja Kwa moja Kwa watanzania. Hicho ndicho ninachotaka, sio makonda as a single unit
 
Back
Top Bottom