Hivi VAT huwa inakatwa kwenye mauzo au kwenye faida?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,657
20,940
Mfano nimenunua bidhaa 100,000, nikiweka gharama zingine inafika 103,000 na nimeuza bidhaa hiyo 120,000 na kupata faida 17,000.

Je, VAT itakuwa 18% ya 120,000, yaani 21,600?.

Au itakuwa 18% ya 17,000 yaani 3,060?

Sheria ya kodi ya nchi inasemaje kuhusu VAT?

Nchi zingine zinafanyaje?

Naomba kujuzwa.
 
Kwanza inatakiwa ujue kuhusu input na output tax.

Unapouza bidhaa unakata output tax na unaponunua unakatwa input tax.
Mwisho wa mwezi unachopeleka TRA ni tofauti kati ya input na output iwapo output tax ni kubwa.

Input ikiwa ni kubwa kuliko output hiyo tofauti unaenda ku claim tra.

Kwa hiyo VAT UNAKATAKA KWENYE MAUZO AU MANUNUZI
 
mfano nikinunua kitu 100,000 input tax itakuwa kiasi gani? nikiuza 120,00 output itakkuwa kiasi gani?.
 
Mfano nimenunua bidhaa 100,000, nikiweka gharama zingine inafika 103,000 na nimeuza bidhaa hiyo 120,000 na kupata faida 17,000.

Je, VAT itakuwa 18% ya 120,000, yaani 21,600?.

Au itakuwa 18% ya 17,000 yaani 3,060?

Sheria ya kodi ya nchi inasemaje kuhusu VAT?

Nchi zingine zinafanyaje?

Naomba kujuzwa.
Value added tax. Panga bei yako,yaani weka faida inayokutosheleza then ukiuza unaongeza 18%.

Kama umeona 100,000 ndio bei sahihi ya bidhaa yako kama uko VAT registered uza 118,000.

18,000 VAT....100,000 yako.
 
Unauza 120,000 + 18% VAT,Nasema hivyo kwakuwa nakumbuka mwaka juzi 2015 nilienda kukata insurance kwa 200,000 lakini mwaka jana 2016 walipoanzisha VAT katika huduma hiyo Nikalipa 236,000
mkuu hapo si ntakuwa nimeuza 141,600 na siyo 120,000?
 
Mfano nimenunua bidhaa 100,000, nikiweka gharama zingine inafika 103,000 na nimeuza bidhaa hiyo 120,000 na kupata faida 17,000.

Je, VAT itakuwa 18% ya 120,000, yaani 21,600?.

Au itakuwa 18% ya 17,000 yaani 3,060?

Sheria ya kodi ya nchi inasemaje kuhusu VAT?

Nchi zingine zinafanyaje?

Naomba kujuzwa.
Hiyo bidhaa ya TZS 100,000 kama umenunua kwa mfanyabiashara aliyesajiliwa tayari ndani yake kuna VAT TZS 15,254.

Endapo umeuza TZS 120,000 ikijumuisha VAT, VAT hapo ni TZS 18,305.

Utakacholipa TRA ni TZS 3,051 hii ndio kodi ya Ongezeko la thamani kati ya bei uliyouzia na ile uliyonunulia.

Ugumu kwenye VAT unakuja pale unaponunua kwa mtu ambaye hakusajiliwa VAT wakati wewe umesajiliwa VAT. Ili usipate shinda kwenye sheria ya VAT, kama wewe umesajiliwa VAT nunua bidhaa zako kwa mtu aliyesajiliwa VAT kwani ile VAT unayolipa kwenye manunuzi si gharama ya biashara yako, utajirudisha kwa kupunguza kwenye VAT uliyowatoza wateja wako.
 
Kama umenunnua kwa mtu ambae HAKUSAJILIWA VAT manunuzi yako hayatakuwa na VAT kwahio utakusanya 18% VAT na kuipeleka tra.
 
Value added tax. Panga bei yako,yaani weka faida inayokutosheleza then ukiuza unaongeza 18%.

Kama umeona 100,000 ndio bei sahihi ya bidhaa yako kama uko VAT registered uza 118,000.

18,000 VAT....100,000 yako.
kama nimekupata, wanakata kwenye mauzo. kwahiyo unapopanga bei inabidi uongeze faida na VAT?
 
Kama umenunnua kwa mtu ambae HAKUSAJILIWA VAT manunuzi yako hayatakuwa na VAT kwahio utakusanya 18% VAT na kuipeleka tra.
Ndio manake. Na inakuwaje anayekuuzia Jumla awe hajasajiliwa wakali wewe unaenda kuuza rejareja uwe umesajiliwa? Ina maana wewe biashara yako ni kubwa kuliko huyo anayekuuzia Jumla?
 
VAT ni 18% ya Bei ya Bidhaa uliyopanga kuuza, kwa kutumia mfano wako hapo juu kama umepanga kuuza bidhaa yako kwa Tshs.120,000/= basi unapaswa kujumlisha 18% ya 120,000/=

VAT ni Mzigo wa Mteja sio Muuzaji

Kama Wewe Muuzaji ni VAT registered unachopeleka TRA sio hiyo 18% Bali ni tofauti ya hiyo 18% ya VAT uliyokusanya kwa kuuza then unatoa kwa kumla ya VAT uliyolipa ulipokuwa unanunua hizo bidhaa kuja kuuza. Mf. Ulikuwa VAT tshs elf 10 Na Wewe uli charge elf 20 kwa Wateja wako hivyo TRA uta remmit only ten thousand
 
Mfano upo hivi
(1)Umenunua bidhaa 100,000
Jumlisha Vat 18%=18,000
Kwa hiyo jumla bidhaa umeinunua kwa 118,000
(2) Bidhaa unaiuza kwa 150,000 vat exclusive
Jumlisha vat 18%=27000
Kwa hiyo bei ya bidhaa itakuwa sh.177,000 vat inclusive
Ukicheki hiyo mifano miwili hapo juu;
Vat ilichajiwa mfano A ni Input tax (vat on purchase)
Vat iliyochajiwa mfano B ni Output tax(vat on sales)
Sasa ikitokea Output tax ni kubwa kuliko input tax tofauti unaenda kulipa Tra
Mfano:27,000-18,000=9,000

Na ikitokea Input tax ni kubwa kuliko Output tax tofauti ni refund/claim (Tra wanapaswa kukurudishia)
 
Ndio manake. Na inakuwaje anayekuuzia Jumla awe hajasajiliwa wakali wewe unaenda kuuza rejareja uwe umesajiliwa? Ina maana wewe biashara yako ni kubwa kuliko huyo anayekuuzia Jumla?
Biashara sio duka tu. Mfano una garage VAT registered, mara nyingi unanunua parts in retail kutokana na demand ya siku hio. Obviously utanunua kwa retailer ambao wengi sio vat registered.
 
Lakini inabidi kujua kuwa sio kila bidhaa ina VAT. Sheria inasamehe baadhi ya bidhaa katika makundi yafuatayo, special relief, exempt na zero rated. Bidhaa kama petrol na diesel hazitozwi VAT.
 
Ndio manake. Na inakuwaje anayekuuzia Jumla awe hajasajiliwa wakali wewe unaenda kuuza rejareja uwe umesajiliwa? Ina maana wewe biashara yako ni kubwa kuliko huyo anayekuuzia Jumla?

Ukichukua Boda boda kwenda kununua Mzigo wako wa Biashara hii ni gharama ya Biashara jee boda boda ni VAT registered kiasi cha kuweza ku deduct kutoka kwny VAT uliyocharge kwa Wateja ?

Ukinunua matunda gengeni kuja kutengeneza Juice kwny hotel yako Wewe uta charge VAT kwa Wateja wako japo material uliyonunua hayana VAT nadhan umeelewa kiasi Fulani?
 
Input tax hapo ni 100,000/1.18 zidisha kwa 0.18
input itakuwa 18000 na output 21600. kwa hiyo ntalipa 3,600? ni ikitokea nimeuza kwa hasara labda 90,000 na VAT ikawa 16200 inabidi niende TRA kudai (16200-18000) 1,800?. nafikiri nimekupata.
 
Back
Top Bottom