Hivi una maanisha nini?.........

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,562
Unaposema, Madaktari wameitikia amri ya Waziri Mkuu??? je kuitikia wito ni kuonekana maeneo ya vituo vya kazi?

kuzungumza na wagonjwa,je tuna uhakika gani kuwa prescriptions zinatolewa, na zinatolewa ipasavyo??
 
Hawa TBC na Clouds ni wapuuzi wa hali ya juu kabisa. hii ni tabia ya siasa za CCM, hawasemi ukweli.

kama katika hospitali ya Muhimbili madaktari wote wamegoma mpaka emergencies, Dodoma hospital madaktari wame-sign lakini hawatoi huduma, Amana hospital na Mbeya the same story, then Hospitali ya Kigoma peke yake ndo wanaonekana kufanya kazi, hospitali ambayo haikugoma in the first place; Halafu wanasema madaktari wameitikia wito wa waziri mkuu..........upuuzi huu, chombo gani cha habari hiki sasa.

Hizi kauli zinazoonyesha kwamba hali ni shwari, halafu watu wanakufa mahospitalini ni hatari sana kwa usalama wa nchi........Upuuzi wa namna hii ukiendelea, these meat heads will live to see it, I am telling you me.

Huu ni ukenge, tungeona waziri wa Afya akionyesha srikali imelifanyiaje tamko la Waziri mkuu leo, watuonyeshe hao madaktari wa majeshi yetu yakifanya kazi; instead, asubuhi na mapema, wanapeleka FFU Muhimbili. Does that make any sense? No body has uttered a word since PM's long boring lecture yesterday, not even the minister in charge....and yet, they call themselves leaders!!!

pambaf na nusu!!
 
Inasikitisha sana! Na mbaya zaidi kuna watu na akili zao timamu wameamini hii brainwashing ya Pindua!
 
Hizi ni propaganda...
hawa wanaleta propaganda kwenye maisha ya wananchi? for whose benefit? matumbo yao? tamaa yao ya kuwa madarakani bila kuwahudumia wananchi?

Hawa viazi hawa.........there will come a day!!!
 
Hivi unapopeleka FFU hospitali unategemea nini? Je, FFU wanaweza kuwalazimisha madaktari kutibu wagonjwa? Na watawalazimisha kwa njia gani? Watapiga mabomu ya machozi? Maana wakijaribu tu wagonjwa waliopo wodini watapata ugonjwa mpya wa macho! Je, Watamwaga maji ya kuwasha? Je, watasimama nyuma ya madaktari kuhakikisha kuwa wanawapima wagonjwa na ku prescribe dawa?
Yaani unaweza kujiuliza maswali 100 na usipate jibu!

Masikini watawala wetu wanadhani kila tatizo linaweza kutatuliwa kwa kutumia FFU. FFU nao bila kufikiria huwa wanabeba silaha na kudandia landrover! Ni kama walivyoenda jangwani wakiwa wamevaa kivita badala ya kuwa na vifaa vya kuokoa wahanga wa mafuriko! Mh, akili ni nywele kila mtu ana zake!
 
Back
Top Bottom