Hivi ukiuza kitu chako na ukapeleka pesa benki usalama wake uko vipi?

OTG

New Member
Feb 24, 2017
0
1,363
Mimi nina mpango wa kuuza shamba langu mahali lakini nasikia kwenye vijiwe vya kahawa kwamba pesa ikiingia tu unakatwa kodi juu kwa juu je ina ukweli hii?
 
Mimi nina mpango wa kuuza shamba langu mahali lakini nasikia kwenye vijiwe vya kahawa kwamba pesa ikiingia tu unakatwa kodi juu kwa juu je ina ukweli hii?
Kwani una madeni ya kodi kwenye biashara/mishe zako nyingine?
 
huo huonevu mkuu, sioni chamaana kabisa. nasikia tuh pesa zinatoka ktk masector mbali mbali ila sioni kbs. .... ex. HOSPTAL ATA DAWA YA MTOTO UNAANDIKIWA UKANUNUE PHAMACNY TENA UKUTE HIYO HIYP PHAMA NI YAMZEE SHAYO.HAHAHAHA kwl watu weusi ni shida.
 
Kama akaunti yako ndio inapata hela nyingi kwa mara ya kwanza, benki lazima itoe taaarifa FIU ( Financial Inteligent Unit) wafuatilie chanzo cha mapato.

Wakati fulani unaweza pewa kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha kama hawajaridhika na maelezo ya chanzo cha mapato

Mwisho weka hela ktk benki inayofanya vizuri. Kwani benki ikifilisika, utapewa sio zaidi ya 1.5 milioni tu, zilizobaki itategemea na sheria za ufilisi kama kutakuwa na salio baada ya madeni na kodi za serikali kulipwa.
 
Kwa navojua mkuu benki wamewekewa maximum amount na BOT kwa individuals kuwekewa per transaction. kwahiyo ikitokea hicho kiwango kikazidi ni lazima benki wakuite utoe maelezo hela zimetoka wapi na supporting document. Mfano kitambo kidogo CRDB ulikua ukiwekewa zaidi ya 100M lazima wakupigie. Kwa sasa sifahamu, ila inawezekana hata hela mbuzi wakazitolea macho.
 
Mimi fedha zangu zitakuwa ni za halali maana nimeuza mali yangu halali ninazomiliki kisheria na nimewahi mara kadhaa huko nyuma kuweka/kupokea fedha kama hizo na hata pale walipotaka kujua uhalali wa fedha nimekuwa nikitoa vielelezo hivyo haikuwahi kuniletea tatizo lolote isipokuwa katika awamu hii hakuna kipindi nimefanya biashara ya kitu fulani na kwenda kuhifadhi fedha benki sasa huku mtaani kuna maneno mengi yanazungumzwa na pia niliwahi kusoma mahala fulani kuwa kule tarime kuna watu wamelipwa fidia na mgodi wa nyamongo ikasemakana watu wa takukuru au DPP wakawa wanawalazimisha kuziachia vinginevyo watafunguliwa kesi za uhujumu uchumi sijui ukweli wake ukoje.
Ndo ivyo mkuu, ndo mana hela zinapotea mtaani kwa sababu kila mtu anaficha pesa zake kuogopa mambo kama hayo
 
Back
Top Bottom