Hivi ufalme wa BB(Blackberry) umeishia wapi??

Hivi ufalme wa BB(Blackberry) umeishia wapi??

Ile iliyokuwa inajiua yenyewe? Yaani unaizima usiku ikiwa buheri wa afya,asubuhi unabonyeza kitufe cha kuwasha unashangaa hola!! Unabonyeza hadi dakika ya sabini hii hapa,hola!!!! Ndiyo imekufa hiyo!! Halafu ukipeleka kwa fundi anaiangalia kama vile ameona kiumbe kutoka sayari ya jupiter
hahahaha
 
Salam wakuu,
Habari za wakati huu? . Strait to the point, miaka ya nyuma kidogo simu Aina ya blackberry zilishika hatamu Sana. Wakati tuko vyuoni sifa ya pisi Kali au blazamen lazima umiliki BB. Pamoja na kwamba ilikua inakera hususani kwenye swala la kureboot unaweza ukalia mpaka simu iwake, lakini kilichowakamata wengi Ni BBM. Aisee, ile ilikua ndio swaga wakati huo. Manzi humuombi namba Bali BBM pin, mpaka kukawaga na ma BBM party etc. Sasa nashangaa saivi sizioni kabisa, nimejaribu kuingia play store naona hata BBM kutumia inabidi ulipie. Sasa sijui wakuu Kuna Nini kuhusu hii kampuni
Dunia inabadilika jamaa! Kuna nyakati ilikua ukikosa baiskeri ya Swala wewe ni maaikini,lakini leo kila mmoja mhangaikaji ana IST.
 
Haha hahaaa. Ati kinabonya bonya
Kweli mkuu ilikuwa imetengenezwa hivyo makusudi eti upate ile experience ya physical keyboard. Simu lilie lilinitia hasara nimechanganya boom na pesa nyingine inunue nionekani na mimi naenda na wakati kumbe simu haliconnect na internet za kibongo, hata huko duniani lilisumbua sana
 
Dah BB kitambo sana, sema these days siangalii brand ya simu kabisa as long as RAM>3 bac aina yyte ile me nnasepa nayo isipokuwa tecno
 
BB Bado ipo
Wana simu za Android zipo vizuri tu
Tatizo bei zao zipo juu, kwa hiyo simu zao ni za class ya executives
Tatizo lingine simu zao za Android hazina camera nzuri ingawa battery life ipo vizuri

Nimeweka hapa BB Priv (2015) n a BB Key 2 (2019)
Ukiangalia specs zake, ni simu nzuri sana
 

Attachments

  • BB Key2.jpg
    BB Key2.jpg
    9 KB · Views: 11
  • BB Priv.jpg
    BB Priv.jpg
    6.8 KB · Views: 11
BB Bado ipo
Wana simu za Android zipo vizuri tu
Tatizo bei zao zipo juu, kwa hiyo simu zao ni za class ya executives
Tatizo lingine simu zao za Android hazina camera nzuri ingawa battery life ipo vizuri

Nimeweka hapa BB Priv (2015) n a BB Key 2 (2019)
Ukiangalia specs zake, ni simu nzuri sana
Hawa ni Tcl ndio walitengeneza hizi simu.
 
Yap.. naona sasa hivi wanatengeneza za kwao. Nimechek Specs za TCL 10 Pro (2020), sio mbaya ingawa kama wanaiga sana Huawei
Siku hizi Ukitoa flagship midrange na low end nyingi zinatengenezwa na Odm Kina wingtech, ndio maana unaona simu nyingi sana zinafanana.
 
BB Bado ipo
Wana simu za Android zipo vizuri tu
Tatizo bei zao zipo juu, kwa hiyo simu zao ni za class ya executives
Tatizo lingine simu zao za Android hazina camera nzuri ingawa battery life ipo vizuri

Nimeweka hapa BB Priv (2015) n a BB Key 2 (2019)
Ukiangalia specs zake, ni simu nzuri sana
Ungese mwingine huu sasa ninunue cm 1m haina camera...sasa hata kwenye matukio muhimu hata kumbukumbu huchukui?
 
Nilizipenda sana, sio fan wa simu ila BB ndo nilikuwa nikitumia tangu shuleni, Nilikasirika sana walipoamia android. Bb Wanazitoa ila zina android. Mm nina BB passport ipo kabatini kama kumbukumbu tu. Now nshazoea misumsung.
Mkuu kama hutojali....naihitaji hiyo passport yako na Mimi nipate ladha ya BB. Pls am serious.
Nicheki pm Niko Mwanza
 
Ungese mwingine huu sasa ninunue cm 1m haina camera...sasa hata kwenye matukio muhimu hata kumbukumbu huchukui?
Kuna makampuni makubwa hawaruhusu kuingia na camera ofisini sababu unaweza leak siri za kampuni. Simu hizo zisizo na camera zina soko lake pia, ni Niche ila lipo.
 
Back
Top Bottom