Hivi uchaguzi wa 2020 CCM wakiulizwa na wananchi kwanini hamkuhamia Dodoma watasema nini?

viwanda

JF-Expert Member
Nov 16, 2016
697
749
Ndugu zangu natafakari naona uchaguzi wa 2020 maswali mengi yatakosa majibu hasa ile issue ya kuhamia dodoma

wakati mwingine najiuliza kwanini viongozi wa Ccm ni waongo kweupe mchana bila aibu, eti PM anatuaga Dar kwakhelini mimi narudi dom masikini wa Mungu kumbe yupo Dar!!
 
Aibu kubwa sana Mkuu..

Aibu ya kujitakia.

Mpaka hivi sasa kwa PM kuendelea kukaa Dar ni aibu.

Haya.. Mawaziri walitakiwa wawe nao wameshahamia Dodoma by this time lakini wapo Dar, aibu.

Waziri Tizeba alisema yeye alikuwa ahamie Dodoma baada ya wiki toka serikali itangaze kuhamia Dodoma, lakini mpaka kesho yupo pale Ofisi za Wizara ya Kilimo, Tazara-Veterinary.. Aibu.. Aibu.
 
Hizi promo za siasa bhana..! yani hizi mambo za nchi hii unaweza kuomba uwe unaota ili ukizinduka ukute mambo shwari
 
Hivi kwanini wanasuasua kuhamia Dodoma?. Mh. Rais ana nia njema na nzuri, ila hawa watendaji wake?. Sijui ni lini majengo ya Dar yatapigwa mnada ili wakose pa kuingia na kukimbilia Dodoma?
 
Tunaomba Mh. Rais awabadilishe wote na kuwachagua waliopo Dodoma yaani Maprofessors wa UDOM kuwa wabunge wa kuteuliwa and then mawaziri.
:):):)
 
Ndugu zangu natafakari naona uchaguzi wa 2020 maswali mengi yatakosa majibu hasa ile issue ya kuhamia dodoma

wakati mwingine najiuliza kwanini viongozi wa Ccm ni waongo kweupe mchana bila aibu, eti PM anatuaga Dar kwakhelini mimi narudi dom masikini wa Mungu kumbe yupo Dar!!

Mkuu tunaoweza kuhoji hilo ni sisi wachache tulioko mjini. Walio wengi wako huko vijijini ambao wakati wa kampeni huwa wanahutubiwa bila kupewa nafasi za kuhoji. Huko huwa wanaambiwa wananchi hawana shida serekali kuhamia Dodoma, bali wana shida ya umeme, maji, shule nk. Zitatolewa takwimu za uongo na za ukweli ambazo wananchi hawazielewi vizuri kisha wataambiwa wapinzani wataleta vita. Wakipewa wali na tshirt business as usual. Sisi tuendelee tu kuhoji huku jukwaani mpake wakose usingizi lakini ukitegemea wapiga kura wenye uelewa finyu ni kupoteza mda.
 
Ndugu zangu natafakari naona uchaguzi wa 2020 maswali mengi yatakosa majibu hasa ile issue ya kuhamia dodoma

wakati mwingine najiuliza kwanini viongozi wa Ccm ni waongo kweupe mchana bila aibu, eti PM anatuaga Dar kwakhelini mimi narudi dom masikini wa Mungu kumbe yupo Dar!!

Serikali inayo nia ya kuhamia Dodoma, lakini yapo ya mambo ya muhimu zaidi kuliko hilo, aidha hakuna madhara yoyote ya kuchelewa kuhamia Dodoma (ni mtizamo wangu)
 
HIVI KILE KIPINDI CHA MARIN HASSAN CHA SAFARI YA DODOMA BADO KIPO? HUWA NASIKILIZA ULE WIMBO TU "JAMANI DODOMA EEEEEEE, DODOMA YA WATANZANIA........" BAADA YA HAPO NABADILISHA KITUO. NAONA MARINI HASSAN ANAUKWAA U-DC SI MUDA MREFU KWA KUSHUPALIA SAFARI YA DODOMA.
 
Back
Top Bottom