Hivi ............Tuna mihimili mingapi katika nchi yetu.......??? Nauliza kwa sababu
1. ...............Jaji mkuu anateuliwa na raisi.......... hiyo haimnyimi uhuru wa maamuzi hasa inapotokea serikali inatakiwa ibanwe....???
2. ....... Raisi ana uwezo wa kuvunja bunge lililochaguliwa na wananchi ........... hiyo haiwezi ikamtisha mbunge katika utoaji hoja bungeni...........????
3. ..........Spika ............ anatoka chama tawala ambaye akifanya tofauti tu.......anaitwa kichama na kubanwa na ikiwezekana anaweza akafukuzwa uanachama...........
Kwa maana hiyo mihimili miwili bado kwa namna moja au nyingine inaripoti kwenye muhimili mmoja (serikali)............. sasa kama hali ndo hiyo kwa nini tunasema tuna mihimili mitatu....???
NAWASILISHA HOJA BINAFSI
Ngalikihinja, hii inaitwa the doctrine of state organs and the separation of powers.
Mihimili hii mitatu ya Bunge , Serikali na Mahakama, kila mmoja unatakiwa kuwa independence of another ili kuleta checks and balance zinazotakiwa, it is very unfortunate kwa Tanzania hizi checks na balance hizi hatuna, japo tunajidai kuwa tuna mihimili hii mitatu huru.
Bunge lina mamlaka ya kutunga tuu sheria, mahakama ina mamlaka ya kuzitafsiri hizo sheria na serikali ndio yenye mamlaka ya kuzitekeleza hizo sheria.
Kwa vile rais wetu sio tuu ni sehemu ya bunge, bali pia amepewa mamlaka ya kulivunja bunge likitunga sheria ambayo yeye hataipitisha, na sheria hata ikitungwa na bunge, haiwi sheria mpaka rais aipitishe, hivyo mwenye nguvu ya mwisho bungeni sio spika bali ni rais, na sasa tukina kwa mama Anna aliyeukwaa uspika kwa zawadi ya sadakalawe ya jinsia yake, ndio usiseme kabisa!.
Tukija kwenye mahakama, japo rais ana uwezo wa kumteua jaji mkuu lakini hana uwezo wa kumfukuza, lakini jaji mkuu hujikuta ana wajibu wa kulipa fadhili kwa aliyemteua, na huyu aliyepo kwa kigezo cha baraghashia ndio kabisa!.
Hata mahakama zikitoa adhabu ya capital punishment, adhabu hiyo haitekelezi mpaka rais aridhie, hivyo kwa mfumo wetu, hakuna cha the doctrine of separation of powers rais ndio kila kitu!.
Niwape mifano michache.
Mahakamu Kuu, ilipoamua kuwa haki ya mgombea binafsi ni ya kikatiba na haiwezi kufinyanywa na sheria yoyote, serikali ililitburuza Bunge, kubadili katiba na kuingiza kifungu cha mgombvea nafasi yoyote ya siasa lazima adhaminiwe na chama. Haya ni matumizi mabaya ya bunge kwa serikali.
Hata baada ya mahakama kuu kukazia hukumu ile, serikali ikakata rufaa, eti mahakama kuu haina uwezo, kuliamuru bunge kubadili kifungu cha katiba, mpaka bunge lenyewe, litakapoamua kubadili kifungu hicho kilichochomekezwa kwa shinikizo la serikali.
Na jopo la majaji saba wa ruffa, ambao ndio ngazi ya mwisho kabisa ya haki nchini ikiitwa 'full bench' ilipokubaliana na rufaa ya serikali, kwa jaji mkuu kujijua hiyo ndiyo hukumu yake ya mwisho, anastaafu akisubiri huruma ya serikali, hawezi kuiudhi kwa vile akitoa hukumu ya haki, mgombea huru ni haki ya msingi uamuzi huu ungeathiri uchaguzi kwa kukosa fedha, hivyo angekosa mafao yake ya kusataafu kwa amani, ikaamua in favour of serikali.
Hata ile richmond saga, Bunge lilipoiamuru serikali ifanye a,b,c,d,..kutekeleza maazimio ya bunge, serikali iligoma kwa kusema, bunge haliwezi kuiamuru, serikali, bali linaweza kuishauri tuu, na serikali ndio itaamua, itekeleze lipi na kuacha lipa. Wabunge walichachamaa na Sitta akafunika kombe mwanaharamu apite, akaufunga mjadala, serikali imeshinda, na ni ni kosa kisheria kuijadili tena richmond popote!
Mahakama haina lolote, Bunge halina lolote, mambo yote ni serikali, na ndio maana tunataka katiba mpya!..