mzizimkuu1
Senior Member
- Apr 18, 2018
- 135
- 106
Kwa kumbukumbu zangu ilishawahi binafsi shwa hii TRC kwa wahind walifel wapi,tuanze hapo.Unajua nchi nyingi walikwisha liona hili na serikali zao zikajiondoa kwenye biashara zikabaki kuwa regulator.
Tatizo letu sisi afrika tuna viongozi wanaokalili, wakiambiwa jiondoeni kufanya biashara kila mnachojaribu kufanya hakifanikiwi, mnaingiza mitaji lakini mkishaingiza mitaji mnawapa watu wasio na machungu na mitaji hiyo na miradi yenu inakosa tija wao wanatafuta ku "re invent the wheel". wanaanza ubishi eti kwa nini serikali isifanye? sasa ni shirika gani serikali yako inayoliendesha likafanikiwa kuliko sekita binafsi?
Tunahitaji sekita binafsi.
wapo watu wanamiriki mabasi yao na wanaweka utaratibu mzuri tu.
tatizo letu sisi ukisema kuweka sekita binafsi basi mtu anakwenda kutafuta marafiki zake, ndugu zake, au wajanja wa mjini wanaojua kupenyeza rupia na wakishindwa wanasema sekita binafsi iko wapi?
serikali tafuta ubia na watu binafsi wachange asilimia fulani ya mitaji na serikali iongezee alafu watu binafsi waendeshe.