Hivi TRC kweli wataweza kuendesha Treni za kisasa?

Unajua nchi nyingi walikwisha liona hili na serikali zao zikajiondoa kwenye biashara zikabaki kuwa regulator.

Tatizo letu sisi afrika tuna viongozi wanaokalili, wakiambiwa jiondoeni kufanya biashara kila mnachojaribu kufanya hakifanikiwi, mnaingiza mitaji lakini mkishaingiza mitaji mnawapa watu wasio na machungu na mitaji hiyo na miradi yenu inakosa tija wao wanatafuta ku "re invent the wheel". wanaanza ubishi eti kwa nini serikali isifanye? sasa ni shirika gani serikali yako inayoliendesha likafanikiwa kuliko sekita binafsi?

Tunahitaji sekita binafsi.

wapo watu wanamiriki mabasi yao na wanaweka utaratibu mzuri tu.

tatizo letu sisi ukisema kuweka sekita binafsi basi mtu anakwenda kutafuta marafiki zake, ndugu zake, au wajanja wa mjini wanaojua kupenyeza rupia na wakishindwa wanasema sekita binafsi iko wapi?

serikali tafuta ubia na watu binafsi wachange asilimia fulani ya mitaji na serikali iongezee alafu watu binafsi waendeshe.
Kwa kumbukumbu zangu ilishawahi binafsi shwa hii TRC kwa wahind walifel wapi,tuanze hapo.
 
Ngoja tujifunze kwa ATCL kwanza. Wakiweza basi na TRC wataweza tena kwa kishindo.
 
TRL
TBC
TTCL
ATCL
TANESCO

Hawa watoto wa baba mmoja na ndugu zao ambao sijawataja ni matatizo matupu
 
Naafikiana na wazo la kuwapa wanaoijenga kuiendesha,
Hivi reli ya zamani itaondolewa au wanaiacha kama historia
reli ya zamani itabaki na itakuwa inatumika, kwa mfano, stesheni ya dar itajengwa kwa mfumo wa ghorofa, treni ya sgr, itafika stesheni upande wa juu ghorofani, hivyo abiria watapanda na kushuka treni mpya wakiwa ghorofani na ile treni ya zamani itabaki upande wa chini, kuserve wale ndugu zetu wanaoendelea kwenda ubungo na pugu, itaserve maneo madogomadogo ya wakazi (commuters)
 
reli ya zamani itabaki na itakuwa inatumika, kwa mfano, stesheni ya dar itajengwa kwa mfumo wa ghorofa, treni ya sgr, itafika stesheni upande wa juu ghorofani, hivyo abiria watapanda na kushuka treni mpya wakiwa ghorofani na ile treni ya zamani itabaki upande wa chini, kuserve wale ndugu zetu wanaoendelea kwenda ubungo na pugu, itaserve maneo madogomadogo ya wakazi (commuters)

Nashukuru Mkuu, je vipi kuhusu reli hiyo kongwe kuanzia Pugu na kuendelea hadi Kigoma, Mpanda, Mwanza nk
 
Nashukuru Mkuu, je vipi kuhusu reli hiyo kongwe kuanzia Pugu na kuendelea hadi Kigoma, Mpanda, Mwanza nk
wa mikoani nao watapambanua waitumie vipi huko kote, naamini sehemu kama morogoro ama dodoma nao wataanzisha safari za ndani kwa ndani kutumia reli hiyo, naamini
 
Kama mtanzania anaweza kurusha ndege ndio hiyo treni?
Nyinyi mibavicha ni mivivu ya kufikiri na kila kitu walahi
Pathetic DNA
 
Kama mtanzania anaweza kurusha ndege ndio hiyo treni?
Nyinyi mibavicha ni mivivu ya kufikiri na kila kitu walahi
Pathetic DNA


Kwenye ndege kuna nidhamu kwasababu ya kanuni na sheria za kimataifa za usalama, lakini kwenye nchi kavu kwakuwa ni usafiri wa ndani basi kunakuwa na elements nyingi za uzembe mwingi
 
Ndio maana Wanatakiwa kunyooshwa

Hizi slogan za kuwanyoosha ni slogan za watu walewale wasiojua cha kufanya.

Huwezi kuniambia Vodacom, Airtel, Tigo yanafanya vizuri kuliko TTCL kwa sababu haya makampuni yanawanyoosha watumishi wao na TTCL haiwanyooshi.

Ki msingi mfumo mzima wa umma umeshakuwa corrupted ni vigumu kuunyoosha na ndio maana wanashauri serikali kujitoa kwenye shughuli za kiuchumi. jenga sekita binafsi wakopeshe mitaji wafanye wakurudishie mitaji yako kwa riba, wakulipe kodi na watengeneze ajira kwa watu wengine.
 
Hizi slogan za kuwanyoosha ni slogan za watu walewale wasiojua cha kufanya.

Huwezi kuniambia Vodacom, Airtel, Tigo yanafanya vizuri kuliko TTCL kwa sababu haya makampuni yanawanyoosha watumishi wao na TTCL haiwanyooshi.

Ki msingi mfumo mzima wa umma umeshakuwa corrupted ni vigumu kuunyoosha na ndio maana wanashauri serikali kujitoa kwenye shughuli za kiuchumi. jenga sekita binafsi wakopeshe mitaji wafanye wakurudishie mitaji yako kwa riba, wakulipe kodi na watengeneze ajira kwa watu wengine.
Huko Voda,Tigo na airtel unadhani wafanyakazi wakikosa tija au kuleta hasara unadhani wanaachwa kazini?
 
Wataalamu wanasema wanadamu hulka zao ni huwa hawataki mabadiliko, yaani mazoea aliyyoyazoea inachukua mda sana kumbadili fikra na kutenda kinyume na mazoea.

TRC wana treni wanayoita express "Deluxe" ikitokea Dar Kwenda kigoma, nimefuatilia utendaji wa shirika hili katika safari hizi za treni ya express kwa kweli nimejiuliza hivi hawa kweli tunaambiwa ikianza treni za kisasa Dar es Salaam mpaka Morogoro itakuwa saa 1 na nusu lakini nikajiuliza kwa hawa kweli haitakuwa masaa 3 mpaka 5 kutokana na mazoea walivyozoea kufanya kazi kwa miaka mingi.

Nilitaka kusafiri kutoka kigoma nikaenda Stesheni siku ya Ijumaa saa 10 jioni nikidhani treni hii ya deluxe bado inaanza safari siku ya Jumamosi saa 2 asubuhi kutoka kigoma. Saa kumi hiyo nikaambiwa treni ipo ijumaa hiyo hiyo usiku inaondoka saa 6 usiku ijumaa na kufika dar jumpili asubuhi. nikakata tiketi na katika safari hiyo niliona yafuatayo

1. Treni niliyoambiwa ijumaa saa 10 jioni kwenye ofisi za TRC kuwa inawasili saa tatu usiku na kuondoka saa 6 usiku, nimefika saa 3 usiku treni haipo, hakuna maelezo yoyote labda watumishi wa TRC kueleza wasafiri kinachoendelea, ubao wa matangazo umebaki na Tangazo lilelile la treni kuondoka saa 6, wasafiri hata wa palepale kigoma mjini wamelala stesheni ya treni maana mtu anawaza pengine itafika mda wowote, nisije kuondoka ikafika ikapakia na kuondoka.

Treni imefika siku ya juma mosi saa 3 asubuhi na kuondoka saa tano asubuhi. Yaani treni ilichelewa masaa 11.

Nilijiuliza hivi saa kumi jioni stesheni wanashindwa kujua treni inayotarajiwa kuwasili saa mbili usiku wake ilipo au mazingira yaliyopo na je itaweza kufika kwa mda au itachelewa? Huu ni uzembe wa hali ya juu. Sio watu wote wanasafiri kuzurura bali watu wengine wanasafiri kwa ratiba, kama mtu ana jambo la kufanya tabora jumamosi na ukamwambia treni inaondoka saa 6 ijumaa, mtu anaona masaa 10 ya kusafiri kigoma mpaka tabora kwa hiyo saa 4 jumamosi atakuwa tabora. Kumbe masaa 11 kutokea saa 6 hiyo treni litakuwa halijaondoka.

Kama mnataka kujikita kusafirisha wazururaji ambao unaweza kuchelewesha safari siku masaa kadhaa au siku kadhaa bila shida haina shaka "keep it up"

2. Nikiwa ndani ya treni nikabahatika kukaa karibu na wafanyakazi wa shirika hili "madereva wa treni" ambao wao walikuwa wakisafiri na treni kwenda kwenye safari zao. Katika maongezi wakawa wanaongelea baadhi ya sababu zinazochelewesha treni na wao walizungumza haya

a) Mpangilio mbaya wa "logistics" za safari za treni kuwa tatizo kubwa. Madereva hawa wanasema ili safari za treni za abiria ziweze kwenda kwa mda kunahitajika umakini mkubwa katika kupanga treni fulani itoke katika kituo fulani kwa mda gani ili ikapishane na treni nyingine katika kituo gani kwa mda gani. Wakasema treni za mizigo mwendo wake ni mdogo na pili breakdown ni nyingi sana.

Wakasema hakuna utaratibu, treni la mizigo linaruhusiwa tu kutoka kituo kimoja na likishaingia katikati itabidi zisubiriane kwenye vituo lakini wakasema katika hili abiria ndio wanatakiwa kupewa kipaumbele. safari zipangwe kwa jinsi ambavyo treni la abiria halitakaa kwenye kituo masaa kadhaa kusubiri kupishana na mengine. Walisema hili halifanyiki treni la mizigo linaweza kuondoka kwenye kituo kutangulia la abiria na ukipiga hesabu za mwendo na zinakokwenda la abiria litatangulia kufika lakini kuna sehemu litapita likiwa na kikwazo mbele yake maana lazima zikapishane kwenye vituo.

b) wakasema utovu wa nidhamu kwa watumishi: wao walitaja kuwa kuna kabila moja limejenga kibuli, dereva anaondoa treni kweye kituo hasikilizi na wala hakuna wa kumshauri akasikiliza kisa yeye ni kabila moja na mtu fulani. Mfano akasema treni la deluxe kuchelewa kufika kigoma siku ya tarehe 30/ 11/ 2018 ni pamoja na dereva mmoja kujenga kiburi na kuondoa treni kigoma ambayo haikuwa na haraka hivyo ililazimu treni ya abiria ikae kituo cha uvinza kusubiri kupishana.

Nilijiuliza hivi hawa kweli wataweza kuachana na hulka hizi walizozioea na kuendesha treni za kisasa kwa kasi ya kisasa? Haijalishi ugoi goi huu wanasababishiwa au wanajisababishia bali hoja watatokaje kwenye mazoea haya na kuendana na kasi mpya.

3. Ndani ya treni kuna vyoo lakini kwa bahati mbaya maji waliyojaza kigoma yalivyoisha hawakujaza maji tena, watu wanaingia vyooni hakuna maji!

4. Treni hili ambalo tuliambiwa ni la express limefika dar jumatatu saa 5 asubuhi, yaani limechelewa masaa 24.

Najua hawa watajitetea kuwa ni ubovu wa miundombinu na kila hoja lakini ki msingi hawa ndivyo walivyo na ukitaka kujua ndivyo walivyo utawasikia wakisema wana mpango wa kuendesha treni zote ya kisasa ikifanya kazi kutokea Dar na ya zamani ikifanya kazi kutokea Dar.

Kama treni ya zamani ingekuwa na matatizo makubwa basi wangekuwa wakisema labda treni ya kisasa ikifika morogoro basi ya zamani itaanzia morogoro kwenda mikoani.

FUNDISHO MOJA NILILOLIONA LINAWEZA KUFAA NI KUACHANA NA HII MANENO YA WANASIASA KWENDA WAKIWAHIKISHIA HAKUNA ATAYEPOTEZA KAZI.

JIFUNZENI KWA KENYA AIRWAYS ILIVYOKUWA IKIBADILISHWA KUTOKA MIFUMO YA ZAMANI KAMA YETU HII YA MASHIRIKA KWENDA USASA WAKE HUU, WALIFUTA AJIRA ZOTE, WAKATANGAZA NAFASI ZOTE NA WAKAAMBIWA KILA MTU AOMBE NAFASI ANAYODHANI ANAIWEZA BILA KUJALI ULIKUWA UNAFANYA NINI. KAMA ULIKUWA MFAGIAJI LAKINI UNAJIONA UNAWEZA KUWA MENEJA OMBA,

WALE WATAKAOPITA KWENYE USAILI NDIO WATAPATA AJIRA BILA KUJALI WALIKUWA NDANI AU NJE.

WALE WALIOKUWA NDANI WAKASHINDWA KWENYE USAILI HAO WANAPEWA RETRENCHMENT.

TUNAO UHURU WA KUCHAGUA SASA AMA TULINDE TRILIONI ZETU SABA TULIZOWEKEZA KWA KUWEKA MAZINGIRA BORA ILI ZILETE TIJA AU TULINDE AJIRA ZA WATU WACHACHE NA WAENDELEE NA MICHEZO YAO.

KUWAHAKIKISHIA WATUMISHI HAWA KUWA AJIRA ZAO NI UNTOUCHABLE "KUNAWEZA" KUWAJENGEA VIBURI VYA KUTOBARIKA LAKINI KAMA UNAFUTA AJIRA ZOTE KUTAWAFANYA WATAKAORUDI KUSTUKA KUWA WASIPOBADIRIKA WANAWEZA KUPOTEA
We jamaa njoo huku uchukue malalmiko ukaywasilishe Kwa Kadogosa
Tanzania Railways Co.
 
Kama mtanzania anaweza kurusha ndege ndio hiyo treni?
Nyinyi mibavicha ni mivivu ya kufikiri na kila kitu walahi
Pathetic DNA

Tatizo la nchi yetu ni vyama vya siasa kutengeneza wahuni wa propaganda ambao hawajui chochote kinavyoendelea bali kazi zao ni kukaa kwenye mitandao kutengeneza propaganda kwa maana ya kupinga au kusapoti.

ungekuwa ni mtanzania unayefanya kazi na umeona utendaji wa hizi taasisi, hata angalau umetumia mabasi ya watu binafsi kama abudi ukaona jinsi unavyokwenda kukata tiketi unavyopokelewa, unapewa tiketi kwa kutajiwa mda kamili na jinsi mtu anavyosafiri confortable. Sio swala la ugumu au technolojia ya hali ya juu bali commitment na nidhamu ambayo mtu binafsi mmoja amefanikiwa kuijenga kwenye biashara lakini

Lakini je hawa wahuni wametumia usafiri kama wa treni huu wanaoendesha TRC?

hapa tunachokizungumza ni kumpa mtu nafasi alafu anatangaza nafasi za ajira lakini wanaoajiriwa ni wenye "god father" na sio waliotoka kwenye usaili. Mtu anaanza kazi akijua mimi nimeletwa na mtu fulani basi anawadharau wote hasikilizi.

Hata sekita binafsi wana manapeana ajira kwa kujuana lakini kule wana machungu na mitaji hivyo wanasimiana ili wapate tija, mali za serikali huwa ni kama mali zisizo na mwenyewe hivyo watu hawana machungu.

Hebu tazama jengo la machinga complex limetumia shilingi ngapi? lakini kama hizo fedha angekuwa amekopa mtu binafsi kwanza kuzikopa angetakiwa kuweka mali zake rehani. hiyo tu ingemfanya kuwa makini tangu hatua ya mwanzo katika kupendekeza mradi kutazama mradi ambao una tija na angeusimamia uzalishe na sio kutumia mabilioni na kutengeneza kitu kisicho na tija.
 
Kwa kumbukumbu zangu ilishawahi binafsi shwa hii TRC kwa wahind walifel wapi,tuanze hapo.

Nadhani tatizo kubwa tulilo nalo sisi ni jamii yetu imekwisha jengeka vipi?

Sio kwamba "Serikali" haiwezi kuendesha vitu hivi kwa ufanisi bali tunapozungumza nchi yetu hapa tulipo hoja ni yeyote utakayempa kazi ya kuendesha shirika hili yale majukumu ya msingi anayaweka pembeni anabeba mengine.

mfumo wetu wa recruitment haulengi katika kutafuta yule ambaye ni bora vilevile hata katika kutafuta private operator tunafanya vimbwanga vilevile. Wahuni wasiojua kitu wanaojua kuhonga ndio wanaoshinda zabuni.

Wataalamu wanaokaa kuandaa proposal zao kitaalamu wanaishia kuzungushwa tu. Hivyo tusichukulie kuwa shirika hili lilikwisha binafsishwa na wahindi wakashindwa bali tutazame kutafuta au kutengeneza shirika la binafsi liendeshe.

Wauzieni tuwakusanye wanaoendesha mabasi yao kwa ufanisi hapa kwetu tuwauzie shea hata kwa kuwakopesha na wao ndio wawe operator.

Tuachane na upuuzi wa kumpa operator masharti eti ya kuchukua wafanyakazi wote wa mashirika haya ambayo wao wamekwisha zoea kuiba mafuta ya kuendeshea ndiyo njia baadhi wanajua inawatoa kimaisha sio mishahara, wamezoea kufanya ujanja kwenye mifumo ya tiketi.

ukifika kituoa cha treni unapima mzigo unawakabidhi lakini sasa wanakwambia eti mzigo ulio mikononi mwao wao hawapakii hivyo utafute wabebaji upatane nao ili hao wabebaji ndio wapakie na usipopatana nao mzigo wako hauji. Gharama ya kusafirisha mzigo kwa treni ukipiga mahesabu ya gharama za treni ziko chini kulinganisha na mabasi au magari lakini ukiweka gharama hizi za wapakiaji ambao ni binafsi gharama zinakuwa juu kuliko kutuma mzigo mdogo kwa magari.

Vipo vikorokoro vingi ambavyo ukimleta private operator unatakiwa umwachie huru ili akabiliane navyo na kubwa ni kuvunja mitandao iliyokuwa ndani ili atengeneze mifumo yake lakini serikali imekuwa "blind" kugangania kuwalazimisha waendeshaji kuchukua wafanyakazi wote wa zamani katika mashirika haya na ndiyo kimekuwa chanzo kikubwa cha kushindwa kuwadhibiti.

ATCL walileta mwekezaji kutoka afrika kusini wakampa masharti yale akashindwa

TRL walileta mwekezaji kutoka india matokeo yaleyale.

Yaani ni sawa na mtu amekuwa na shamba ana watumishi na kila akiingiza mtaji watumishi wanakula hapati mavuno alafu anatafuta mtu wa kuendesha shamba eti anampa masharti ya kuwabakiza watumishi wake hawa wote????? unategemea nini?
 

Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom