Hivi TRC kweli wataweza kuendesha Treni za kisasa?


E

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Messages
1,295
Likes
633
Points
280
E

ego

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2013
1,295 633 280
Wataalamu wanasema wanadamu hulka zao ni huwa hawataki mabadiliko, yaani mazoea aliyyoyazoea inachukua mda sana kumbadili fikra na kutenda kinyume na mazoea.

TRC wana treni wanayoita express "Deluxe" ikitokea Dar Kwenda kigoma, nimefuatilia utendaji wa shirika hili katika safari hizi za treni ya express kwa kweli nimejiuliza hivi hawa kweli tunaambiwa ikianza treni za kisasa Dar es Salaam mpaka Morogoro itakuwa saa 1 na nusu lakini nikajiuliza kwa hawa kweli haitakuwa masaa 3 mpaka 5 kutokana na mazoea walivyozoea kufanya kazi kwa miaka mingi.

Nilitaka kusafiri kutoka kigoma nikaenda Stesheni siku ya Ijumaa saa 10 jioni nikidhani treni hii ya deluxe bado inaanza safari siku ya Jumamosi saa 2 asubuhi kutoka kigoma. Saa kumi hiyo nikaambiwa treni ipo ijumaa hiyo hiyo usiku inaondoka saa 6 usiku ijumaa na kufika dar jumpili asubuhi. nikakata tiketi na katika safari hiyo niliona yafuatayo

1. Treni niliyoambiwa ijumaa saa 10 jioni kwenye ofisi za TRC kuwa inawasili saa tatu usiku na kuondoka saa 6 usiku, nimefika saa 3 usiku treni haipo, hakuna maelezo yoyote labda watumishi wa TRC kueleza wasafiri kinachoendelea, ubao wa matangazo umebaki na Tangazo lilelile la treni kuondoka saa 6, wasafiri hata wa palepale kigoma mjini wamelala stesheni ya treni maana mtu anawaza pengine itafika mda wowote, nisije kuondoka ikafika ikapakia na kuondoka.

Treni imefika siku ya juma mosi saa 3 asubuhi na kuondoka saa tano asubuhi. Yaani treni ilichelewa masaa 11.

Nilijiuliza hivi saa kumi jioni stesheni wanashindwa kujua treni inayotarajiwa kuwasili saa mbili usiku wake ilipo au mazingira yaliyopo na je itaweza kufika kwa mda au itachelewa? Huu ni uzembe wa hali ya juu. Sio watu wote wanasafiri kuzurura bali watu wengine wanasafiri kwa ratiba, kama mtu ana jambo la kufanya tabora jumamosi na ukamwambia treni inaondoka saa 6 ijumaa, mtu anaona masaa 10 ya kusafiri kigoma mpaka tabora kwa hiyo saa 4 jumamosi atakuwa tabora. Kumbe masaa 11 kutokea saa 6 hiyo treni litakuwa halijaondoka.

Kama mnataka kujikita kusafirisha wazururaji ambao unaweza kuchelewesha safari siku masaa kadhaa au siku kadhaa bila shida haina shaka "keep it up"

2. Nikiwa ndani ya treni nikabahatika kukaa karibu na wafanyakazi wa shirika hili "madereva wa treni" ambao wao walikuwa wakisafiri na treni kwenda kwenye safari zao. Katika maongezi wakawa wanaongelea baadhi ya sababu zinazochelewesha treni na wao walizungumza haya

a) Mpangilio mbaya wa "logistics" za safari za treni kuwa tatizo kubwa. Madereva hawa wanasema ili safari za treni za abiria ziweze kwenda kwa mda kunahitajika umakini mkubwa katika kupanga treni fulani itoke katika kituo fulani kwa mda gani ili ikapishane na treni nyingine katika kituo gani kwa mda gani. Wakasema treni za mizigo mwendo wake ni mdogo na pili breakdown ni nyingi sana.

Wakasema hakuna utaratibu, treni la mizigo linaruhusiwa tu kutoka kituo kimoja na likishaingia katikati itabidi zisubiriane kwenye vituo lakini wakasema katika hili abiria ndio wanatakiwa kupewa kipaumbele. safari zipangwe kwa jinsi ambavyo treni la abiria halitakaa kwenye kituo masaa kadhaa kusubiri kupishana na mengine. Walisema hili halifanyiki treni la mizigo linaweza kuondoka kwenye kituo kutangulia la abiria na ukipiga hesabu za mwendo na zinakokwenda la abiria litatangulia kufika lakini kuna sehemu litapita likiwa na kikwazo mbele yake maana lazima zikapishane kwenye vituo.

b) wakasema utovu wa nidhamu kwa watumishi: wao walitaja kuwa kuna kabila moja limejenga kibuli, dereva anaondoa treni kweye kituo hasikilizi na wala hakuna wa kumshauri akasikiliza kisa yeye ni kabila moja na mtu fulani. Mfano akasema treni la deluxe kuchelewa kufika kigoma siku ya tarehe 30/ 11/ 2018 ni pamoja na dereva mmoja kujenga kiburi na kuondoa treni kigoma ambayo haikuwa na haraka hivyo ililazimu treni ya abiria ikae kituo cha uvinza kusubiri kupishana.

Nilijiuliza hivi hawa kweli wataweza kuachana na hulka hizi walizozioea na kuendesha treni za kisasa kwa kasi ya kisasa? Haijalishi ugoi goi huu wanasababishiwa au wanajisababishia bali hoja watatokaje kwenye mazoea haya na kuendana na kasi mpya.

3. Ndani ya treni kuna vyoo lakini kwa bahati mbaya maji waliyojaza kigoma yalivyoisha hawakujaza maji tena, watu wanaingia vyooni hakuna maji!

4. Treni hili ambalo tuliambiwa ni la express limefika dar jumatatu saa 5 asubuhi, yaani limechelewa masaa 24.

Najua hawa watajitetea kuwa ni ubovu wa miundombinu na kila hoja lakini ki msingi hawa ndivyo walivyo na ukitaka kujua ndivyo walivyo utawasikia wakisema wana mpango wa kuendesha treni zote ya kisasa ikifanya kazi kutokea Dar na ya zamani ikifanya kazi kutokea Dar.

Kama treni ya zamani ingekuwa na matatizo makubwa basi wangekuwa wakisema labda treni ya kisasa ikifika morogoro basi ya zamani itaanzia morogoro kwenda mikoani.

FUNDISHO MOJA NILILOLIONA LINAWEZA KUFAA NI KUACHANA NA HII MANENO YA WANASIASA KWENDA WAKIWAHIKISHIA HAKUNA ATAYEPOTEZA KAZI.

JIFUNZENI KWA KENYA AIRWAYS ILIVYOKUWA IKIBADILISHWA KUTOKA MIFUMO YA ZAMANI KAMA YETU HII YA MASHIRIKA KWENDA USASA WAKE HUU, WALIFUTA AJIRA ZOTE, WAKATANGAZA NAFASI ZOTE NA WAKAAMBIWA KILA MTU AOMBE NAFASI ANAYODHANI ANAIWEZA BILA KUJALI ULIKUWA UNAFANYA NINI. KAMA ULIKUWA MFAGIAJI LAKINI UNAJIONA UNAWEZA KUWA MENEJA OMBA,

WALE WATAKAOPITA KWENYE USAILI NDIO WATAPATA AJIRA BILA KUJALI WALIKUWA NDANI AU NJE.

WALE WALIOKUWA NDANI WAKASHINDWA KWENYE USAILI HAO WANAPEWA RETRENCHMENT.

TUNAO UHURU WA KUCHAGUA SASA AMA TULINDE TRILIONI ZETU SABA TULIZOWEKEZA KWA KUWEKA MAZINGIRA BORA ILI ZILETE TIJA AU TULINDE AJIRA ZA WATU WACHACHE NA WAENDELEE NA MICHEZO YAO.

KUWAHAKIKISHIA WATUMISHI HAWA KUWA AJIRA ZAO NI UNTOUCHABLE "KUNAWEZA" KUWAJENGEA VIBURI VYA KUTOBARIKA LAKINI KAMA UNAFUTA AJIRA ZOTE KUTAWAFANYA WATAKAORUDI KUSTUKA KUWA WASIPOBADIRIKA WANAWEZA KUPOTEA
 
M

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2018
Messages
780
Likes
1,240
Points
180
M

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2018
780 1,240 180
Sio TRC 9sijui TRL) tu Mkuu; SEKTA ZOTE ZA UMMA NCHI HII NI MAJANGA TU.
 
Eli79

Eli79

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Messages
21,220
Likes
15,090
Points
280
Eli79

Eli79

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2013
21,220 15,090 280
Nina wasiwasi hiyo treni itauwa watu, sio kwa man management tuliyonayo, tumefeli kwa almost kila kitu.

Pilot project iliyotakiwa itupe mwanga ni DART, kama Ile imeshindwa, tena imeshindwa kabisa, usitegemee kuona treni ikifanikiwa, labda wapewe watu makini zaidi, sio watanzania wenye ngozi nyeusi. It hurts but truth must be said.
 
Joselela

Joselela

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Messages
2,773
Likes
2,629
Points
280
Joselela

Joselela

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2017
2,773 2,629 280
Akiwagusa mtaanza kusema aaah tunataka kazi na bata....
 
dist111

dist111

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2012
Messages
3,130
Likes
1,489
Points
280
dist111

dist111

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2012
3,130 1,489 280
Mwendo kasi tu inawashinda, wataweza hizo nyingine.

Yaani inahitaji fukuza fukuza ya kila sehem
 
koyola

koyola

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
1,749
Likes
1,018
Points
280
koyola

koyola

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
1,749 1,018 280
Sio TRC 9sijui TRL) tu Mkuu; SEKTA ZOTE ZA UMMA NCHI HII NI MAJANGA TU.
Sekta za umma ni mzigo na ni mitaji ya wachache mifano mingi sana ilivokufa kwa hizi sababu
1 hakuna mwenye uchungu
2 kuwekana kindugunaizeshen hufanya watu kuajiriwa bila taaluma
Kwamaana hiyo kupata maendeleo kwa mashirika ni muda mchache tu kisha huzima kama kibatari.
 
Dindira

Dindira

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2016
Messages
2,368
Likes
2,463
Points
280
Dindira

Dindira

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2016
2,368 2,463 280
Labda CEO awe msambaa, mpare, mchagga au mmasai ndio ufanisi wa TRL utakapooneka. Makabila tajwa yako serious sana na kazi.
 
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
10,205
Likes
4,676
Points
280
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
10,205 4,676 280
Hii ya sasa itakuwa na vibao vinavyoonyesha muda ambao train inaingia kwa kila kituo na mfumo huo una uwezo wa kujua imekwama wapi na kama ni technical fault itaandika ni eneo gani la machine ili kurahisisha utengenezaji.

Kama kutatokea changamoto za hayo usemayo basi itakuwa ni uhujumu wa watendaji, ila nijuavyo ni kwamba sehemu kubwa ya uendeshaji ni digially controlled and monitored, anyway yamkini tabia za makabila zitaingilia mifumo hilo siwezi kulisemea.
 
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
10,205
Likes
4,676
Points
280
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
10,205 4,676 280
Labda CEO awe msambaa, mpare, mchagga au mmasai ndio ufanisi wa TRL utakapooneka. Makabila tajwa yako serious sana na kazi.

Ngosha je!?
 
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Messages
30,919
Likes
17,776
Points
280
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2014
30,919 17,776 280
Subirini ya mwndokasi inatokea huko TRC

Ova
 
E

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Messages
1,295
Likes
633
Points
280
E

ego

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2013
1,295 633 280
Hii ya sasa itakuwa na vibao vinavyoonyesha muda ambao train inaingia kwa kila kituo na mfumo huo una uwezo wa kujua imekwama wapi na kama ni technical fault itaandika ni eneo gani la machine ili kurahisisha utengenezaji.

Kama kutatokea changamoto za hayo usemayo basi itakuwa ni uhujumu wa watendaji, ila nijuavyo ni kwamba sehemu kubwa ya uendeshaji ni digially controlled and monitored, anyway yamkini tabia za makabila zitaingilia mifumo hilo siwezi kulisemea.
Ndugu yangu watu ndio wanao drive digital na sio digital kudrive.

ukiwa na watu wanaotamani kukimbia sana lakini kufanya kazi kwa manual kukawachelewesha hao ukiwapa digital watakimbia kwelikweli.

Lakini ukikaa na watu wazembe, wanafanya mambo kwa mazoea, goi goi ukadhani ukawapa digital utawabadirisha waende kasi???? hakuna kitu kama hicho.

Compyuta haifanyi mtu akimbie bali mtu anayetumia kompyuta ndiye mambo yake huenda haraka. Usiwaze kuondoa uzembe na uvivu ni kwa kuweka kompyuta bali watu wanaoelemewa na kazi ndio wakipewa kumpyuta huwarahisishia.
 
nasrimgambo

nasrimgambo

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2017
Messages
361
Likes
286
Points
80
nasrimgambo

nasrimgambo

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2017
361 286 80
hawatoweza, wawaulize wezao wa udart, walivyofeli kuendesha mwendokasi
 
nasrimgambo

nasrimgambo

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2017
Messages
361
Likes
286
Points
80
nasrimgambo

nasrimgambo

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2017
361 286 80
yani hili taifa hahah, tunajidai kujisifia mbele za wageni tu ila wenyewe ndani kwa ndani tunafahamu madudu yetu, ila cha kusikitisha hayo madudu ni kazi sana kuyamaliza tunabaki kuyatazama tu na mwishowe tunabaki kuyazoea
 
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
10,205
Likes
4,676
Points
280
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
10,205 4,676 280
Compyuta haifanyi mtu akimbie bali mtu anayetumia kompyuta ndiye mambo yake huenda haraka. Usiwaze kuondoa uzembe na uvivu ni kwa kuweka kompyuta bali watu wanaoelemewa na kazi ndio wakipewa kumpyuta huwarahisishia.

Mkuu nimegusia human behaviour pale chini kabisa, sorry kama sikuweka maelezo katika sura unayoielewa
 
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
10,205
Likes
4,676
Points
280
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
10,205 4,676 280
yani hili taifa hahah, tunajidai kujisifia mbele za wageni tu ila wenyewe ndani kwa ndani tunafahamu madudu yetu, ila cha kusikitisha hayo madudu ni kazi sana kuyamaliza tunabaki kuyatazama tu na mwishowe tunabaki kuyazoea

Mkuu, shida tuliyo nayo ni maslahi binafsi, nikupe mfano mdogo miaka ya nyuma TAZARA ilikuwa njia nzuri sana ya usafiri iliyopendwa na watu wengi mno, ilipoanza kuhujumiwa ikageuka kero kwa kila mtumiaji, TAZARA ya leo hii inasikitisha mno, ukitazama kiini cha yote hayo ni ubinafsi
 
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
10,205
Likes
4,676
Points
280
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
10,205 4,676 280
Nina wasiwasi hiyo treni itauwa watu, sio kwa man management tuliyonayo, tumefeli kwa almost kila kitu.

Pilot project iliyotakiwa itupe mwanga ni DART, kama Ile imeshindwa, tena imeshindwa kabisa, usitegemee kuona treni ikifanikiwa, labda wapewe watu makini zaidi, sio watanzania wenye ngozi nyeusi. It hurts but truth must be said.

Naafikiana na wazo la kuwapa wanaoijenga kuiendesha,
Hivi reli ya zamani itaondolewa au wanaiacha kama historia
 
E

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Messages
1,295
Likes
633
Points
280
E

ego

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2013
1,295 633 280
Naafikiana na wazo la kuwapa wanaoijenga kuiendesha,
Hivi reli ya zamani itaondolewa au wanaiacha kama historia
Unajua nchi nyingi walikwisha liona hili na serikali zao zikajiondoa kwenye biashara zikabaki kuwa regulator.

Tatizo letu sisi afrika tuna viongozi wanaokalili, wakiambiwa jiondoeni kufanya biashara kila mnachojaribu kufanya hakifanikiwi, mnaingiza mitaji lakini mkishaingiza mitaji mnawapa watu wasio na machungu na mitaji hiyo na miradi yenu inakosa tija wao wanatafuta ku "re invent the wheel". wanaanza ubishi eti kwa nini serikali isifanye? sasa ni shirika gani serikali yako inayoliendesha likafanikiwa kuliko sekita binafsi?

Tunahitaji sekita binafsi.

wapo watu wanamiriki mabasi yao na wanaweka utaratibu mzuri tu.

tatizo letu sisi ukisema kuweka sekita binafsi basi mtu anakwenda kutafuta marafiki zake, ndugu zake, au wajanja wa mjini wanaojua kupenyeza rupia na wakishindwa wanasema sekita binafsi iko wapi?

serikali tafuta ubia na watu binafsi wachange asilimia fulani ya mitaji na serikali iongezee alafu watu binafsi waendeshe.
 

Forum statistics

Threads 1,238,170
Members 475,830
Posts 29,311,897