Hivi TCRA mko wapi juu ya haya?

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
WanaJF wenzangu habari za jioni natumai mu wazima wa afya njema.Niko hapa kuwajuza juu ya hii kero inayonikera sana mimi na hata watumiaji wengine kama mimi.

Kero yenyewe ni hii ya kupokea matangazo ya televisheni kwa njia ya satelite na hii ni kwa chaneli za hapa nchini ambazo ni ITV, EATV, CAPITAL, TBC1, CH10 na STAR TV ambazo zote ziko ktk band C-BAND. Yaani jamani imekuwa kero saana leo ziko sawa kesho asubuhi zinagoma keshokutwa ziko sawa hadi najiuliza kwa uelewa wangu mdogo kuwa wamiliki hao wa vituo hivyo vya kurushia matangazo huwa wanachajiwa gharama ya juu tena kwa masaa katika satelite wanayotumia kurushia matangazo.

Sasa swali langu najiuliza kama satelite wanayotumia haina nguvu kwa nini wasiiame wakaamia satelite yenye nguvu.Au ndio ile desturi yetu watanzania ya kuchakachua na kununua vitu chakavu kila siku matengenezo Mko wapi TCRA na baraza la ushindani.
 
Back
Top Bottom