ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,544
Kwa haraka tu nayakumbuka baadhi ya matukio ya ajali hizi za chopa katika kipindi kifupi tu. Nakumbuka kuna mgombea mmoja Arusha wa CCM alinusurika kuanguka na chopa aliyokua ameikodi toka kwa Ndesamburo akidai kuwa ilikua mbovu na kutaka kumuua.
Pili ikatokea ajali ya chopa pale ilipokua inataka kuruka ikiwabeba viongozi wa mkoa wa Dar es salaam akiwamo Mkuu wa Mkoa, Kamanda Kova na Bw. Magufuli, hii ilianguka ingawa walipata majeraha kiasi.
Ikafuatia chopa ilioanguka maeneo ya Moshi Bar na kuua rubani, ikafuatia ajali ya chopa alionusurika mbunge kijana wa Arumeru mh Nassari baada ya kupata ajali mbaya na sasa imetokea hii iliochukua roho za watu 4, akiwamo kijana mpiganaji, mtetea wanyonge mh Deo Filikunjombe!
Napata shaka na ubora wa hizi chopa, hasa binafsi ikiwa kama zina ubora wa kutosha? Na vipi historia ya vyombo hivyo? Wapi na lini kimetoka na kufanya kazi kwa muda gani? Kweli kuna umuhimu wa kujua haya ili kuokoa roho za watu katika ajali hizi za kushtua.