Wolle Melkas Fernando
JF-Expert Member
- May 4, 2016
- 218
- 297
Salaam nyingi sana waungwana!
Tunaadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa kujitawala na kujifanyia maamuzi ya mambo yetu wenyewe.
Miaka 60 sio mchezo na haina kisingizio cha kusema sisi tuko nyuma kimaendeleo kwasababu bado wachanga katika masuala ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiteknolojia (We don't have an excuse).
Naangalia tenda za serikalini katika masuala mbalimbali hususan ya Miradi ya Ujenzi zinapewa Kampuni za Kigeni, ninachojiuliza kwahiyo miaka 60 yote sisi hatuna mainjinia wa kufanya hiyo kazi tukawalipa na pesa tubaki nayo hapa nyumbani?
Ndani ya Miaka 60 ya Uhuru Mainjinia wetu wamekuwa wakihitimu tu katika vyuo vikuu mbalimbali ndani na nje ya nchi lakini tenda kubwa kubwa za Constructions wanapewa wageni halafu wenyeji ambao ni mainjinia wetu wanaajiriwa na wageni na serikali inajitapa kuwa mradi huu umetengeneza ajira.
Mara nyingi kama sio zote Wenyeji hupewa tenda za kuziba viraka kwenye barabara zetu au kuweka makaravati, hiki ni kichekesho kinachoumiza.
Hivi kuna haja gani ya Taifa kusomesha wataalam mfano wa masuala ya madini, gesi, mafuta?
Mwalimu Nyerere aliwahi kuzuia uchimbwaji wa madini akisisitiza mpaka wazawa wasome waje wachimbe wenyewe, kilichopo sasa sote tunajua, wazawa wasomi na wataalamu wa Jiolojia wamebaki kuwa vibarua wa makampuni makubwa ya madini kutoka nje ambao hufanya utafiti kupata madini nchini mwetu na sisi tunaambulia kulamba asilimia chini ya kumi na tunajitapa tuna wataalam tunasonga mbele.
Serikali imekuwa ikipiga chapuo ya vijana kujiajiri na kusema vijana waende VETA ili wakimaliza wajiajiri, wapo wengi kwenye vikundi wengine useremala, wengine ushonaji n.k.
Lakini cha kushangaza serikali inaruhusu makampuni yaliyowekeza hapa nchini kuagiza nje Furnitures kwaajili ya ofisi zao hapa nchini huku yakiacha kuwaungisha vijana wetu, Makampuni yanaagiza uniforms za wafanyakazi wao kutoka nje, yanashindwa kununua hapa nchini kwa vikundi vizuri kabisa vya ushonaji, nina ushahidi wa haya.
Hivi huku ni kulogwa au tatizo ni nini waungwana, kuna maana gani ya kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru kama tunaruhusu Uhuru wa Kazi na Kipato kwa Vijana wetu kupokwa na Wageni kwa kile tunaita kuwapa Uhuru Wawekezaji?