mageuzi1992
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 2,502
- 257
Ukiwa unakwenda tanga, mbele kidogo ya Muheza, kuna Kijiji kinaitwa Tanganyika! Kama una kiu na hilo jina, nenda kaishi hapo. la, huwezi, nenda kule magharibi kuna Ziwa Tanganyika. Leteni hoja za maana, kwani wewe utakula na kuishi kwa Tanganyika jina?
Tanganyika unayo ndani umeifungia hutaki kuifungulia iwe huru. Ni ujinga kuita Tanzania bara ni nchi wakati hakuna RAMANI yoyote hapa duniani yenye kuionesha!!!!!!!!!!!!!Huwa najiuliza sana , Tanzania ni muungano wa Nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar Zanzibar ipo lakini Tanzania imefunikwa!! Je ni nani anaweza kutuambia Tanganyika ilipo?! Kama ni hivyo basi je Tanzania ni Muungano wanchi ngapi..? Je nchi moja yaweza kuungana yenyewe? Zanzibar wana bendera yao wimbo wa taifa wao na rais wao. Je rais wa Tanganyika,wimbo wa taifa wa Tanganyika na bendera ya Tanganyika ni ipi? Nisaidieni jamani maana mimi huwa natatizwa sana.!!! Kwa mfano inapofikia kuadhimisha sherehe fulani kama uhuru au muungano Tunajua tarehe 9-12-1961 ilikuwa siku ya uhuru wa Tanganyika. Sasa ajabu kila tarehe sita inapoazimiswa utasikia ama viongozi au watangazaji wa habari wanasema tunakumbuka uhuru Wa Tanzania Bara!!!! Je kuna nchi ilikuwa inaitwa Tanzania bara? au ni unafiki huu? Wakati mwingine utasikia wakati wa sherehe za muungano wanasema leo tunakumbuka siku ya muungano wa Tanzania bara na Zanzibar......'' WHAT IS TANZANIA BARA ? IS IT A NATION?'' Nashauri katiba mpya iitambue Tanganyika.
Ukiwa unakwenda tanga, mbele kidogo ya Muheza, kuna Kijiji kinaitwa Tanganyika! Kama una kiu na hilo jina, nenda kaishi hapo. la, huwezi, nenda kule magharibi kuna Ziwa Tanganyika. Leteni hoja za maana, kwani wewe utakula na kuishi kwa Tanganyika jina?
ipo mioyoni mwetu;
Tume ya Warioba imo katika kukamilisha ukusanyanyi wa maoni hatujachelewa kudai iwekwe pia katika katiba mpya.
Itamkwe wazi wazi kuwa Tanzania ni Muungano. Muungano wenye wanachama wawili. Nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar.
Muungano huu wa Tanzania utashughulikia masuala ya muungano tu na yale yasiyo ya Muungano yatashughulikiwa na serikali za nchi wanachama wa muungano huu.
Kwa maoni yangu, mzizi wa malalamiko/ kiini macho utakuwa umepatiwa dawa. Pia hii itatoa nafasi ya kuvutia wanachama wengine kujiunga na kuona jina Tanzania linakua/linapanuka zaidi.
Kwa mfano, Rwanda akijiunga jina jipya litakuwa RwaTanZania(Rwatanzania) na Burundi akijiunga jina jipya la Muungano litakuwa BuRwaTanZania ( Burwatanzania)...Jina linazidi kuwa la kibantu na tamu zaidi kwenye ulimi.
CCM imeamua kuendelea kufanya Muungano kuwa ni agenda yake binafsi, imeshindwa kuifanya iwe agenda ya 'wananchi wa pande zote mbili', jambo ambalo lingewezekana kabisa, na tunge epuka misuko suko mingi inayokabili muungano wetu leo; Sijui, lakini it might be too late;