Hivi swala ni kuoana au kuzaana….?


Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000

Watu wanaoana kila siku kama siyo kila saa, duniani kote. Kuoana kunachukuliwa kama suala la kimaumbile, yaani ambalo lisipofanywa, maisha nayo yatasimama. Ukweli ni kwamba maumbile hayajui kuoana. Yanachojua ni kuzaana….! Maumbile yametengeneza mazingira ambapo binadamu ataendelea kuwepo, ambayo ni kile kitendo cha binadamu kujamiiana. Wanyama wanaendelea kuwepo kwa sababu wanapandana (siyo kupendana). Lakini wanyama ndio ambao wanafuata kanuni za maumbile, kwani hupandana pale tu wanapotaka kuzaa. Nje ya kuzaa, wanyama hawapandani. Kwao kupandana siyo starehe, bali wito au hitaji la kimaumbile. Kwa binadamu kujamiiana kumegeuzwa starehe na siyo hitaji la kimaumbile. Watu wanajamiiana ili kujisikia vizuri. Kuna wanaojamiiana sana wanapokuwa kwenye msongeko wa kiakili, yaani kujamiiana kunafikia mahali kunatumika kama tiba kwa matatizo ya kiakili ingawa haiponeshi. Lakini hili halikuwa lengo la maumbile au Mungu kama wengine wanavyoita.


Ndio maana ndoa inafunganishwa na kujamiiana na siyo watu wawili walioamua kuishi pamoja ili kusaidiana katika mambo mengi ya kimaisha na wakitaka, wapate watoto. Kama ukikagua kwa makini utabaini kwamba watu wengi huchukulia kujamiiana kama ndio kuoana kwenyewe. Watu wakizungumzia ndoa, wanazungumzia kujamiiana. Kwa hiyo kuoana kwa fasili yetu wengi, ni tendo la ndoa. Kuoana siyo kuishi pamoja ili kupeana nafuu kimwili, kihisia, kiakili na kiroho. Kwa sababu maumbile hayajui kuoana bali yanajua binadamu kupendana, bila kujali jinsia, ndipo tatizo linapoanzia. Maumbie yameunda mfumo ambao utawezesha binadamu kuwepo hata baada ya wengine kufutika kwenye uso wa dunia kwa kufa. Mfumo huu ni wa kuwa na mwanamke na mwanaume ambapo wanapojamiiana, binadamu mwingine anaweza kupatikana.

Hizi sheria zinazoitwa kuoana, kuzini na nyingine, siyo za maumbile, bali za binadamu. Ndio maana hata mitindo, mbinu na taratibu za kuoana zinatofautiana sana kutoka jamii moja hadi nyingine. Kule Pacific, kwa mfano, kuna kisiwa ambapo ndugu wawili wanaume wanaweza kuoa mke mmoja, au kule katika misitu ya Amazon ambapo kuna kabila moja linalojulikana kama Zoe ambalo mwanamke ndiye anayeoa na anaweza kuoa hata wanaume wawili mpaka wanne. Jambo la kimaumbile haliwezi kuwa na tofauti kutoka binadamu mmoja hadi mwingine. Kwa mfano, hakuna kufa kwa mtindo wa Uingereza na mtindo wa Tanzania, hakuna kuumwa njaa kwa mtindo wa Bolivia na mtindo wa Botswana.


Kutokana na ukweli kwamba, binadamu amefanya kuoana kama jambo la kimaumbile, halafu akalifungamanisha na tendo la ndoa, anajikuta akioa au kuolewa tu. Hana haja ya kujiuliza ni kwa nini anaoa au kuolewa. Kwa sababu watu wanaoana na kuolewana amefikia umri ambao jamii imepanga kwamba, ni wa kuoa au kuolewa, anaingia kwenye ndoa. Ukiwauliza watu wengi ni kwa nini wamo kwenye ndoa watakwambia ni kwa sababu wamefika umri wa kuoa au kuolewa. Ni ni nani amepanga umri wa kuoa au kuolewana ameupanga kwa vigezo gani? Je mtu akipitisha mri huo, kuna tatizo gani litamsibu?

Lakini sababu nyingine ambayo mtu atakupa ni kwamba, anaoa kwa sababu amempenda fulani. Kupenda hapa ina maana amemtamani mtu fulani. Hajui kwamba, amemtamani kwa sababu kila mmoja wetu amefundishwa kwamba, kutamani kunaitwa kupenda. Kama ingekuwa ni kweli watu wanaoana kwa sababu wanapendana, kusingekuwa na talaka kabisa. Kama talaka zingetokea, ingekuwa ni kama ajali mbaya sana na wanaoachana wanageendelea kuwa marafiki. Hii ni kwa sababu kupenda siyo jambo rahisi kiasi hicho. Kupenda hakutoki kwenye hisia bali bali hutoka rohoni na wengi hatujawahi kuishi maisha yanayohusisha roho.Mtu anasema amemwoa fulani kwa sababu wanapendana naye. Halafu baada ya mwaka hawaelewani kabisa na inafikia mmoja anamuwa mwingine. Huku ndio kupenda kwa namna gani? Watu hawa walitamaniana na kuamua kufunga ndoa, hawakuwa na sababu nyingine ya maana ya kuingia kwenye kuishi pamoja. Nijuavyo mimi kuoana ni suala la kibinadamu zaidi kuliko kuwa suala la kimaumbile. Kwa hiyo kila binadamu ana nafasi ya kujiuliza akiwa huru kabisa kama anataka kuoa au kuolewa. Akishajiuliza, inabidi ajiulize sababu ya kuoa au kuolewa. Ni vizuri sababu hiyo ikawa yake siyo ile ya kijamii, ya mazoea, kwamba, watu wengine wanaoa au kuolewa. Lakini isiwe ya tamaa ya tendo la ndoa. Kuoa kukishafungwa pamoja na tendo la ndoa ni lazima kuwe na mushkeli.

Kumbuka tu kwamba, hakuna mahali maumbile yanaposema ni lazima mtu aoe au kuolewa, kama ilivyo lazima kwa mtu kula akibanwa na njaa, au kama ilivyo lazima mtu kulala akiwa na usingizi. Kuoa au kuolewa ni taratibu za kibinadamu na wala siyo kimaumbile. Najua wale wenzangu ambao wamekariri maarifa ya aina mbalimbali, zikiwemo imani za dini zao wanaweza kubisha juu ya jambo hili. Lakini hiyo ni juu yao kwa sababu, najua pamoja na dini zao wanaishi kwenye ndoa zinazowaka moto.

Hebu chukulia kwamba, unatamani sana kuwa na watoto na hatokei mwanaume wa kukuoa, utafanyaje? Je kutotokea mwanaume wa kukuoa ni kosa lako? Kanuni ya maumbile inasema watu wazaane, haisemi watu waoane………… Fikiria, kila mwanamke ambaye unaamini ndiye anayeweza kukufaa kuwa mke, ukijaribu kumwomba muoane hataki, utafanya nini wakati unataka sana watoto? Si utamchukua usiyemtaka, angalau uweze kupata watoto, jambo ambalo ndilo la kimaumbile. Hapo kuna upendo au kuna ndoa kweli? Kuna kuzaana tu, ambayo ndiyo dhima ya maumbile

haya wale wahafidhina aka Ma-Conservative Kina, gfsonwin, nivea, nyumba kubwa, BADILI TABIA, farkhina, jouneGwalu, charminglady, Ciello, Madame B, MadameX, lara 1, Paloma, NATA, Neylu, Yummy, SnowBall, Mwita Maranya, platozoom, Eiyer, MwanajamiiOne, Angel Msoffe, fabinyo, King'asti, Arushaone, Mungi, Erotica, Natalia, Zinduna, matumbo, Jiwe Linaloishi Mentor, Kijino, Kaunga, BelindaJacob, HorsePower, Kongosho na wengineo nisiowataja waje hapa walete changamoto zao........
 
Last edited by a moderator:
J

jeneneke

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
752
Points
195
J

jeneneke

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
752 195
Sasa Mtambuzi mbona we hukuzaa tu?huku unakoelekea siku hizi babu siko naona unataka kutupotosha badala ya kutuelekeza
 
Last edited by a moderator:
NATA

NATA

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2007
Messages
4,512
Points
1,195
NATA

NATA

JF-Expert Member
Joined May 10, 2007
4,512 1,195
Mh kuna muasisi mmoja alisema kuoana ni kuhalisha ngono !

Kwa jamii nyingi hasa za kiafrica wanaamini mkioana , mkazaane .

Ndoa nyingi zinayumba kwa kukosa mtoto lakini kunazingine nyingi tu zinayumba hata pale manapokuwa na watoto tele.!

Lakini kwa sasa wa Afrika watoto katika ndoa ni muhimu sana!
 
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
Sasa Mtambuzi mbona we hukuzaa tu?huku unakoelekea siku hizi babu siko naona unataka kutupotosha badala ya kutuelekeza
Hebu soma hapa chini kisha nipe jibu...............

Hebu chukulia kwamba, unatamani sana kuwa na watoto na hatokei mwanaume wa kukuoa, utafanyaje? Je kutotokea mwanaume wa kukuoa ni kosa lako? Kanuni ya maumbile inasema watu wazaane, haisemi watu waoane………… Fikiria, kila mwanamke ambaye unaamini ndiye anayeweza kukufaa kuwa mke, ukijaribu kumwomba muoane hataki, utafanya nini wakati unataka sana watoto? Si utamchukua usiyemtaka, angalau uweze kupata watoto, jambo ambalo ndilo la kimaumbile. Hapo kuna upendo au kuna ndoa kweli? Kuna kuzaana tu, ambayo ndiyo dhima ya maumbile
 
HorsePower

HorsePower

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2008
Messages
3,613
Points
1,225
HorsePower

HorsePower

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2008
3,613 1,225
Mada nimeipenda. Mimi bado naamini kuwa ndoa ni kwa ajili ya kupeana nafuu kimwili, kihisia, kiakili na kiroho na si kuzaa na kuishi pamoja pekee yake. Vinginevyo tusingeweza kutofautishwa na wanyama ambao wao hukutana kwa kuzaa na si kwa starehe wala kufarijiana!
 
Blaine

Blaine

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2012
Messages
2,280
Points
0
Blaine

Blaine

JF-Expert Member
Joined Jan 11, 2012
2,280 0
kids need a stable environment to grow up na ndoa ina-provide that environment. kama huoni mtu wa kuoa na unataka mtoto then go adopt or use a surrogate
 
B

Babuyao

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2009
Messages
1,733
Points
1,225
B

Babuyao

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2009
1,733 1,225
Mwanadamu ni zaidi ya mnyama kama ng,ombe na mbuzi. Ni kiumbe mwenye akili na utashi ndo maana haongozwi na maumbile tu (instinct) bali pia na akili na utashi. Hapo ndo zinaingia values zingine ambazo strictly kwa ajili ya mwanadamu na si kiumbe kingine. Hapa ndipo inaingia ndoa na majukumu yake. Kumbe kwa mwanadamu ndoa ni ya lazima kama value ili mtu aweze kutumia tendo la ndoa na kutimiza matokeo yote ya tendo hilo na muumgano huo.
 
Arushaone

Arushaone

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2012
Messages
14,765
Points
2,000
Arushaone

Arushaone

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2012
14,765 2,000
Kuoana ni kutoana upweke ila kuzaa ni matokeo. Ukisoma Baibo Mwanzo kuna sehemu Mungu alipomaliza kumuumba Mwanaume alisema ngoja tumpe msaidizi wake ........... Matokeo wakaanza kuijaza NCHI nasi tunaijaza DUNIA.
Kwa kusema hivyo Mtambuzi, nakwepa kusema kuwa kila aoaye/aolewaye lazima azae....
 
Last edited by a moderator:
fabinyo

fabinyo

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2011
Messages
2,082
Points
1,225
fabinyo

fabinyo

JF-Expert Member
Joined Aug 5, 2011
2,082 1,225
me nathani ni kwa sababu ya akili na utashi wetu uliotofauti na viumbe wengine na hiyo ilikuwa ni kuleta ustaarabu hapa duniani ila kinachotokea kwa sasa ni kana kwamba tunarudi kwenye hayo uliyoyasema maana siku hizi tunazaa tu,hovyohovyo,wazee wanabaka vitoto hata vya miezi michache ya kuzaliwa!wanyama wamekuwa waungwana zaidi yetu sisi kwa sasa!!otherwise ilikuwa poa sana sisi kuendelea kuwa na utaratibu huo
 
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,701
Points
2,000
Age
47
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,701 2,000
Mtambuzi kuzaa ni matokeo ya kuwepo wawili, lakin sio sababu ya ninyi kuwepo wawili na iwapo itachukuliwa kama sababu basi kwa asiyeweza kuzaa hana haja ya kuwa na mwenza

kwangu mm ni vyema sana wenza wakibarikiwa kupata watoto, ingawa siwez kumlaumu mtu kama akikosa mtoto, na maisha yenyewe yanajua kwann yanampa A mtoto na kumyima B mtoto. kiukweli kabisa kuishi kwa wenza ni ili kutimiza makusudi ya kimwili tu na si ili kupata watoto peke yake ingekuwa ni hivyo watu asinge hangaika na kupanga uzazi.

pia naweza kuliogelea hili kwa namna ya kisayansi zaid, mwanamke hujiskia kufanya tendo la ndoa anapokuwa kwenye heat(ovulation), na hapa ndipo inapokuja lile swala la wanyama ambao hupandana wakiwa kwenye heat, wakati huu mwanamke huwa yuko prone to conception ila tu huwa anajizuia asipate kama iko nje ya ratiba yake. so unaweza kuona kwamba kuoana ni swala ambalo linatuweka sote pamoja katika mpangilio ama ratib maalum tofauti na kama kila mtu akiachwa afanye hovyo hovyo.
 
Last edited by a moderator:
Kimbweka

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2009
Messages
8,611
Points
1,225
Kimbweka

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2009
8,611 1,225
1 Wakorinto 7:8 -9
Basi, wale ambao hawajaoana na wale walio wajane nawaambia kwamba ni vema kuendelea kuwa kama mimi nilivyo. Hata hivyo, kama mtu hawezi kujizuia basi, na aoe; maana ni afadhali zaidi kuoa kuliko kuwaka tamaa.
 
Preta

Preta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
24,194
Points
2,000
Preta

Preta

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
24,194 2,000
asante sana Mtambuzi kwa mada yako nzuri.....nimeipenda.....lakini kuna mahali umenikatili......hii picha hapa chini.....unaweza kuipandisha pandisha kidogo nikaona mpaka kwenywe miguu ya hao watu........?.....japo basi hata magoti.......


 
Last edited by a moderator:
1PRESIDENT

1PRESIDENT

Member
Joined
Nov 5, 2012
Messages
36
Points
0
1PRESIDENT

1PRESIDENT

Member
Joined Nov 5, 2012
36 0
Umenifanya nifikiri kwa nini nataka kuoa kwani mwanzo nilikuwa na mawazo ya kutafuta mwanamke na kuzaa naye tu nichukue biashara watoto wangu niishi nao but mtazamo umebadilika kidogo...
 
jouneGwalu

jouneGwalu

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
2,688
Points
1,225
jouneGwalu

jouneGwalu

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
2,688 1,225
Nadhani nakuelewa kati ya mistari, kwamba ni muda mufaka sana kutoa changamoto kwa namna ya maisha iliyozoeleka miongoni mwetu....

Sawa kabisa!
Lakini pia kuna ukweli mwembamba kuwa mambo yapo hivi "KIMAZOEA" pia ni zao la huo uasili!

Soma vizuri post ya Babuyao.

Suala la ndoa ni namna ya kutafsiri tu naona ndio limekukwamisha we mzee, hata bila uwepo wa hichi cha sasa kwamba sijui sherehe na vikorombwezo vingine vya kiutaratibu vya kumtwaa mtoto wa watu kwako bado ndoa ingekuwepo tu.

Hebu suala la kupendana tuliache pembeni kidogo!

Katika utaratibu wa kuishi kama binadamu hata zama za ujima, inafika wakati kijana wa kiume atabalehe na wakike atavunja ungo, hapo mwili unabadilisha namna kutii tabia za maumbile na akili......
Huyu kijana wa kiume mwili wake utahitaji binti kwaajili ya kujamiiana naye, na binti mwili wake utahitaji mwanaume kwa ajili hiyo hiyo...... ie lengo kuu ni kuzaliana pia (rejea hoja yako ya harufu, na hapa nimetoa case kwenyemazingira ya uasilia kabisa hamna usasa)

Suala la ndoa linakuja hapo katikati kwasababu unakuja mda sasa kijana huyu haijalishi atajamiina na wanawake wangapi ila atatengeneza ngome sehemu, kiasilia binadamu anawivu kwa sehemu anayoipa umuhimu na kuijali, dhana ya umiliki inakuja hapo!

Unakuta kuwa yule mwanamke/wanawake w/anaye jamiiana naye/o anatamani w/awe w/ake peke yake..... je hii sio ndoa??

Hivi ndivyo mambo yanavyotokea kwenye ulimwengu wa asili kabisa chini ya elimu ya asilia tupu.

Huku kwenye ulimwengu wa kisasa tumeongeza mbwembwe kidogo ila bado dhana ni ileile.
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
asante sana Mtambuzi kwa mada yako nzuri.....nimeipenda.....lakini kuna mahali umenikatili......hii picha hapa chini.....unaweza kuipandisha pandisha kidogo nikaona mpaka kwenywe miguu ya hao watu........?.....japo basi hata magoti.......


Ha ha ha haaaaaaa............... Ama Kweli Preta unachemka ngono
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
Nadhani nakuelewa kati ya mistari, kwamba ni muda mufaka sana kutoa changamoto kwa namna ya maisha iliyozoeleka miongoni mwetu....

Sawa kabisa!
Lakini pia kuna ukweli mwembamba kuwa mambo yapo hivi "KIMAZOEA" pia ni zao la huo uasili!

Soma vizuri post ya Babuyao.

Suala la ndoa ni namna ya kutafsiri tu naona ndio limekukwamisha we mzee, hata bila uwepo wa hichi cha sasa kwamba sijui sherehe na vikorombwezo vingine vya kiutaratibu vya kumtwaa mtoto wa watu kwako bado ndoa ingekuwepo tu.

Hebu suala la kupendana tuliache pembeni kidogo!

Katika utaratibu wa kuishi kama binadamu hata zama za ujima, inafika wakati kijana wa kiume atabalehe na wakike atavunja ungo, hapo mwili unabadilisha namna kutii tabia za maumbile na akili......
Huyu kijana wa kiume mwili wake utahitaji binti kwaajili ya kujamiiana naye, na binti mwili wake utahitaji mwanaume kwa ajili hiyo hiyo...... ie lengo kuu ni kuzaliana pia (rejea hoja yako ya harufu, na hapa nimetoa case kwenyemazingira ya uasilia kabisa hamna usasa)

Suala la ndoa linakuja hapo katikati kwasababu unakuja mda sasa kijana huyu haijalishi atajamiina na wanawake wangapi ila atatengeneza ngome sehemu, kiasilia binadamu anawivu kwa sehemu anayoipa umuhimu na kuijali, dhana ya umiliki inakuja hapo!

Unakuta kuwa yule mwanamke/wanawake w/anaye jamiiana naye/o anatamani w/awe w/ake peke yake..... je hii sio ndoa??

Hivi ndivyo mambo yanavyotokea kwenye ulimwengu wa asili kabisa chini ya elimu ya asilia tupu.

Huku kwenye ulimwengu wa kisasa tumeongeza mbwembwe kidogo ila bado dhana ni ileile.

[FONT=&amp][FONT=&amp]Mkuu umenikumbusha kisa cha Mende na tendo la kujamiiana:

[/FONT]Mende dume anapoanzisha uhusiano na mende jike, kila anapomaliza kujamiiana, hutoboa tundu kwenye mgongo wa mende jike.[/FONT]
[FONT=&amp]Kwa kawaida mende dume, kila anapotaka kujamiiana na jike ni lazima kwanza aangalie kama kuna tundu lolote mgongoni kwa jike. Na jambo la pili ni lazima aangalia kama tundu limepona. Kama halijapona hawezi kujamiiana. Kama mende jike alishajamiiana mara hamsini ina maana atakuwa ametobolewa mara hamsini, atakuwa na makovu hamsini mgongoni. Hii ni kutaka kumiliki, ni kutaka awe peke yake. [/FONT]
[FONT=&amp]Ikitokea mende mwingine dume akataka kujamiiana na mende huyu, kabla hajajamiiana naye, ni lazima aangalie na kuhesabu matundu yaliyopo kwenye mwili wa mende huyu jike. Kama atakuta kuna matundu hamsini ataumia sana, na kuna uwezekano akaacha kujamiiana naye – ni wivu? Ni ubinafsi? Ni uchoyo?

Hali hii pia ipo kwa binadamu, kuna wanaume wengine hudiriki hata kuwanusa au kuwaapisha wapenzi wao ili kuhakiki kama hawajafanya mapenzi huko nje.

Kaaazi kweli kweli[/FONT]..................
 
J

JF Tanga one

Member
Joined
Nov 19, 2012
Messages
28
Points
0
J

JF Tanga one

Member
Joined Nov 19, 2012
28 0
Hapo atakuwa amestirika dogo tu!

Ila swala ni kuoana, kuzaa majaaliwa/ matokeo ya mechi zenu na maumbile!

asante sana Mtambuzi kwa mada yako nzuri.....nimeipenda.....lakini kuna mahali umenikatili......hii picha hapa chini.....unaweza kuipandisha pandisha kidogo nikaona mpaka kwenywe miguu ya hao watu........?.....japo basi hata magoti.......


 
Preta

Preta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
24,194
Points
2,000
Preta

Preta

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
24,194 2,000
Ha ha ha haaaaaaa............... Ama Kweli Preta unachemka ngono
jamani Mtambuzi....sio hivyo....ni kwamba huwa napenda zaidi full pictures na sio three quarter........
 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads 1,296,582
Members 498,672
Posts 31,252,965
Top