Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Watu wanaoana kila siku kama siyo kila saa, duniani kote. Kuoana kunachukuliwa kama suala la kimaumbile, yaani ambalo lisipofanywa, maisha nayo yatasimama. Ukweli ni kwamba maumbile hayajui kuoana. Yanachojua ni kuzaana….! Maumbile yametengeneza mazingira ambapo binadamu ataendelea kuwepo, ambayo ni kile kitendo cha binadamu kujamiiana. Wanyama wanaendelea kuwepo kwa sababu wanapandana (siyo kupendana). Lakini wanyama ndio ambao wanafuata kanuni za maumbile, kwani hupandana pale tu wanapotaka kuzaa. Nje ya kuzaa, wanyama hawapandani. Kwao kupandana siyo starehe, bali wito au hitaji la kimaumbile. Kwa binadamu kujamiiana kumegeuzwa starehe na siyo hitaji la kimaumbile. Watu wanajamiiana ili kujisikia vizuri. Kuna wanaojamiiana sana wanapokuwa kwenye msongeko wa kiakili, yaani kujamiiana kunafikia mahali kunatumika kama tiba kwa matatizo ya kiakili ingawa haiponeshi. Lakini hili halikuwa lengo la maumbile au Mungu kama wengine wanavyoita.
Ndio maana ndoa inafunganishwa na kujamiiana na siyo watu wawili walioamua kuishi pamoja ili kusaidiana katika mambo mengi ya kimaisha na wakitaka, wapate watoto. Kama ukikagua kwa makini utabaini kwamba watu wengi huchukulia kujamiiana kama ndio kuoana kwenyewe. Watu wakizungumzia ndoa, wanazungumzia kujamiiana. Kwa hiyo kuoana kwa fasili yetu wengi, ni tendo la ndoa. Kuoana siyo kuishi pamoja ili kupeana nafuu kimwili, kihisia, kiakili na kiroho. Kwa sababu maumbile hayajui kuoana bali yanajua binadamu kupendana, bila kujali jinsia, ndipo tatizo linapoanzia. Maumbie yameunda mfumo ambao utawezesha binadamu kuwepo hata baada ya wengine kufutika kwenye uso wa dunia kwa kufa. Mfumo huu ni wa kuwa na mwanamke na mwanaume ambapo wanapojamiiana, binadamu mwingine anaweza kupatikana.
Hizi sheria zinazoitwa kuoana, kuzini na nyingine, siyo za maumbile, bali za binadamu. Ndio maana hata mitindo, mbinu na taratibu za kuoana zinatofautiana sana kutoka jamii moja hadi nyingine. Kule Pacific, kwa mfano, kuna kisiwa ambapo ndugu wawili wanaume wanaweza kuoa mke mmoja, au kule katika misitu ya Amazon ambapo kuna kabila moja linalojulikana kama Zoe ambalo mwanamke ndiye anayeoa na anaweza kuoa hata wanaume wawili mpaka wanne. Jambo la kimaumbile haliwezi kuwa na tofauti kutoka binadamu mmoja hadi mwingine. Kwa mfano, hakuna kufa kwa mtindo wa Uingereza na mtindo wa Tanzania, hakuna kuumwa njaa kwa mtindo wa Bolivia na mtindo wa Botswana.
Kutokana na ukweli kwamba, binadamu amefanya kuoana kama jambo la kimaumbile, halafu akalifungamanisha na tendo la ndoa, anajikuta akioa au kuolewa tu. Hana haja ya kujiuliza ni kwa nini anaoa au kuolewa. Kwa sababu watu wanaoana na kuolewana amefikia umri ambao jamii imepanga kwamba, ni wa kuoa au kuolewa, anaingia kwenye ndoa. Ukiwauliza watu wengi ni kwa nini wamo kwenye ndoa watakwambia ni kwa sababu wamefika umri wa kuoa au kuolewa. Ni ni nani amepanga umri wa kuoa au kuolewana ameupanga kwa vigezo gani? Je mtu akipitisha mri huo, kuna tatizo gani litamsibu?
Lakini sababu nyingine ambayo mtu atakupa ni kwamba, anaoa kwa sababu amempenda fulani. Kupenda hapa ina maana amemtamani mtu fulani. Hajui kwamba, amemtamani kwa sababu kila mmoja wetu amefundishwa kwamba, kutamani kunaitwa kupenda. Kama ingekuwa ni kweli watu wanaoana kwa sababu wanapendana, kusingekuwa na talaka kabisa. Kama talaka zingetokea, ingekuwa ni kama ajali mbaya sana na wanaoachana wanageendelea kuwa marafiki. Hii ni kwa sababu kupenda siyo jambo rahisi kiasi hicho. Kupenda hakutoki kwenye hisia bali bali hutoka rohoni na wengi hatujawahi kuishi maisha yanayohusisha roho.
Mtu anasema amemwoa fulani kwa sababu wanapendana naye. Halafu baada ya mwaka hawaelewani kabisa na inafikia mmoja anamuwa mwingine. Huku ndio kupenda kwa namna gani? Watu hawa walitamaniana na kuamua kufunga ndoa, hawakuwa na sababu nyingine ya maana ya kuingia kwenye kuishi pamoja. Nijuavyo mimi kuoana ni suala la kibinadamu zaidi kuliko kuwa suala la kimaumbile. Kwa hiyo kila binadamu ana nafasi ya kujiuliza akiwa huru kabisa kama anataka kuoa au kuolewa. Akishajiuliza, inabidi ajiulize sababu ya kuoa au kuolewa. Ni vizuri sababu hiyo ikawa yake siyo ile ya kijamii, ya mazoea, kwamba, watu wengine wanaoa au kuolewa. Lakini isiwe ya tamaa ya tendo la ndoa. Kuoa kukishafungwa pamoja na tendo la ndoa ni lazima kuwe na mushkeli.
Kumbuka tu kwamba, hakuna mahali maumbile yanaposema ni lazima mtu aoe au kuolewa, kama ilivyo lazima kwa mtu kula akibanwa na njaa, au kama ilivyo lazima mtu kulala akiwa na usingizi. Kuoa au kuolewa ni taratibu za kibinadamu na wala siyo kimaumbile. Najua wale wenzangu ambao wamekariri maarifa ya aina mbalimbali, zikiwemo imani za dini zao wanaweza kubisha juu ya jambo hili. Lakini hiyo ni juu yao kwa sababu, najua pamoja na dini zao wanaishi kwenye ndoa zinazowaka moto.
Hebu chukulia kwamba, unatamani sana kuwa na watoto na hatokei mwanaume wa kukuoa, utafanyaje? Je kutotokea mwanaume wa kukuoa ni kosa lako? Kanuni ya maumbile inasema watu wazaane, haisemi watu waoane………… Fikiria, kila mwanamke ambaye unaamini ndiye anayeweza kukufaa kuwa mke, ukijaribu kumwomba muoane hataki, utafanya nini wakati unataka sana watoto? Si utamchukua usiyemtaka, angalau uweze kupata watoto, jambo ambalo ndilo la kimaumbile. Hapo kuna upendo au kuna ndoa kweli? Kuna kuzaana tu, ambayo ndiyo dhima ya maumbile
haya wale wahafidhina aka Ma-Conservative Kina, gfsonwin, nivea, nyumba kubwa, BADILI TABIA, farkhina, jouneGwalu, charminglady, Ciello, Madame B, MadameX, lara 1, Paloma, NATA, Neylu, Yummy, SnowBall, Mwita Maranya, platozoom, Eiyer, MwanajamiiOne, Angel Msoffe, fabinyo, King'asti, Arushaone, Mungi, Erotica, Natalia, Zinduna, matumbo, Jiwe Linaloishi Mentor, Kijino, Kaunga, BelindaJacob, HorsePower, Kongosho na wengineo nisiowataja waje hapa walete changamoto zao........
Last edited by a moderator: